CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) jana tarehe 18.02.2016 lilitangaza matokeo ya Mitihani ya kidato cha NNE na kuleta taharuki kwa wadau mbalimbali kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi kushindwa kufaulu kwa kupata ufaulu wa chini. Nimesikia watu wengi wakieleza kuwa wanafunzi wengi walikuwa na ufaulu usiostahili wakati walipofanya Mitihani ya kuingia kidato cha tatu mwaka 2013 na hivyo kujikuta wakishindwa kumudu masomo ya kidato cha tatu 2014 na hivyo kutahiniwa kwao kidato cha Nne kulikuwa hakustahili kwa kuwa hawakuweza kumudu hata masomo ya kidato cha kwanza na pili ili kuendelea na kidato cha tatu. Aidha yapo maswali mengi yanayoulizwa kuhusiana na matokeo hayo.Nini kifanyike? Mitihani ya kidato cha pili iheshimiwe ili kupata wanafunzi wenye kumudu stadi mbalimbali katika nyanja za uchumi,siasa na jamii. Masuala ya Kitaaluma yaendeshwe kitaalamu pasipo kubadilishwa pasipo tija kama ilivyokuwa kutoka Division mara GPA. Suala la michepuo kwa wanafunzi liwekewe kanuni na m