UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI
Na, Rev. Innocent Kamote SEHEMU YA 1: KITABU CHA DANIELI. SOMO LA 1: KUPITIA YA KITABU CHA DANIELI : A; D A N I E L I: Lengo la 1; - Eleza Historia fupi ya Danieli. Danieli – jina lake lina maana “ Mungu ndiye Hakimu wangu ”. Alikuwa mmojawapo wa mateka waliochukuliwa na mfalme Nebukadneza katika mwaka 605 KK. Kutoka Yerusalemu na kupelekwa Babeli. Aliishi kipindi chote cha utumwa cha miaka 70 huku akiwa nabii na mwandishi wa Kitabu cha Danieli. Tunamfahamu Danieli jinsi alivyokuwa mcha Mungu, tu...