li uweze kufanikiwa, ni lazima kujiwekea misingi imara ya kimafanikio  itakayokuwa ikukuongoza kila siku. Bila kuijua misingi hii mapema  sitashangaa kuona maisha yako yakibaki kuwa yaleyale bila ya kubadilika  sana. Kwa kujiwekea misingi hii, inauwezo wa kufanya maisha yako  kubadilika kwa sehemu kubwa sana.     Kama misingi hiyo ipo, ni nini kinachokuzuia wewe kufanikiwa sasa? Bila  shaka hakuna. Unachohitajika kukifanya ni kutumia misingi hiyo mpaka  kufanikiwa. Uwezo na nguvu za kubadilisha maisha yako kwa kadri  unavyotaka unao. Kwa kuijua misingi hii, kwako itakuwa chachu ya  kukusaidia kuweza kusonga mbele na kujijengea maisha ya mafanikio  makubwa:-   Je, misingi hiyo ni ipi?    Hii Ndiyo Misingi 6 Muhimu Ya Kujiwekea, Ili Kujenga Mafanikio Ya Kudumu   1. Kaa mbali na watu hasi   Kama vile ambavyo ilivyo kompyuta inaweza ikaharibiwa na virusi na  kuharibika kabisa, hata wewe maisha yako yanaweza kuharibiwa vivyohivyo  lakini ikiwa una watu hawa hasi wengi wanaokuzunguka. Unapok...