taarifa kwa vyombo vya habari     taarifa kwa vyombo vya habari     JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA   KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU     Simu : +255-22-2114512, 2116898   Email :  press@ikulu.go.tz   Tovuti :  www.ikulu.go.tz   Faksi : 255-22-2113425       OFISI YA RAIS,   IKULU,   1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   11400 DAR ES SALAAM,   TANZANIA       Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Watanzania na taasisi mbalimbali kutumia takwimu sahihi zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kujiepusha na takwimu za upotoshaji zinazosambazwa na baadhi ya watu kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.   Mhe. Rais Magufuli amesema hayo tarehe 20 Desemba, 2017 katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu inayojengwa katika eneo la Makulu Mjini Dodoma.   Pamoja na wito huo Mhe. Rais Magufuli ameitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu pamoja na vyombo vingine husika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mt...
Machapisho
Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba 20, 2017