NAFASI ZA KAZI : MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III - NAFASI 14
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Tabora Uyui anawatangazia nafasi za kazi kwa wananchi wote wenye sifa za kuomba nafasi hizo kama inavyoonyesha hapo chini MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III - NAFASI 14 SIFA ZA MWOMBAJI Awe amehitimu elimu ya kidato cha Sita/Nne na Mafunzo ya Astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma, au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali. KAZI ZA KUFANYA - Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji. - Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao. - Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji. - Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji. - Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu. - Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na Kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuond...