SOMO : UTATAKA KUTUBU LAKINI TOBA YAKO ITAKATALIWA.
MCH. BOAZ ANASI FPCT UJIJI KIGOMA Kuna mambo yanaonekana kana kwamba Mungu ana ugomvi na wewe. Mambo haya yanakwamisha au kukufanya ushindwe kumwona Mungu katika maisha yako. Isa 1:19,Yak 4 :7a,Kut 19 : 3-8 3 Musa akapanda kwa Mungu, na BWANA akamwita toka mlima ule, akisema, Utawaambia nyumba ya Yakobo, na kuwaarifu wana wa Israeli, maneno haya; 4# Kum 32:11; Isa 63:9; Ufu 12:14 Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. 5# Kum 4:20; 7:6; 10:14; 14:2; 26:18; 32:8; 1 Fal 8:53; Zab 50:12; 135:4; Tit 2:14; 1 Kor 10:26 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, 6# Ufu 1:6; 5:10; 20:6; 1 Pet 2:5,9; Law 20:24; Kum 7:6; Isa 62:12; 1 The 5:27 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli. 7 Musa akaenda akawai...