WOKOVU NI KUWA NA USHIRIKA
Sehemu ya pili K WELI KUU: Maisha yetu ya wokovu hayana maana kabisa kama hatutakuwa na ushirika na Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, na sisi kwa sisi kama kanisa la Kristo ambalo ni mwili wa Kristo. Mstari wa Msingi (Kukumbuka): 1 Wakorintho 1:9 Mungu ni mwamainifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe , Yesu Kristo Bwana wetu. UTANGULIZI Katika utangulizi, sehemu ya kwanza ya somo letu tuliangalia maana ya “ ushirika ” na maana ya “ uhusiano au mahusiano ” na pia tulipata kubainisha na kuainisha kwa kifupi sana viini (essences) vya ushirika. Leo katika utangulizi wetu nataka twende mbele kidogo kwa kuangalia ni nini maana ya “wokovu”; usisahau somo letu ni “ Wokovu Ni Kuwa Na Ushirika ” na bado tupo kwenye utangulizi ambapo tunaangalia maana ya maneno muhimu; wokovu, uhusiano na ushirika. WOKOVU MAANA YAKE NINI? Wokovu ni ukombozi wa mwanadamu kutoka katika vifungo vyote vya mauti na kuzimu kwa kusamehew