UENDESHAJI WA VIKAO
Ni jambo zuri kuwa na vikao vya ndugu,jamaa,jumuiya,kikundi,Taasisi n.k Fuatilia somo hili kwa makini. UENDESHAJI WA VIKAO Na, AYOUB LEO VIKAO Ni mazungumzo yanayofuata utaratibu maalum kwa ajili ya kupata azimio/maamuzi ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu/mipango. Uongozi shirikishi una tabia ya kujali vikao ili kuweka mipango na mikakati inayowezesha kundi/jamii kuwa katika umoja.Hivyo uongozi wa kidemokrasia huwa na vikao ili kupata ushauri na maoni ya wajumbe juu ya mipango. SIFA ZA VIKAO · Vikao vinatakiwa kuwa na agenda/mada ya kujadili. · Viwe na muda maalum wa kuitishwa mfano.Wiki/Mwezi/miezi mitatu na hata mwaka .(Hii hutegemea aina ya vikao) · Kuwa na wajumbe( idadi ya wale waliokubalika). · Kuwepo na mwenyekiti, katibu na wajumbe wengine. · Agenda zifafanuliwe kwa kina kabla ya wajumbe kuchangia.(Taarifa kwa kina itolewe juu ya agenda iliyopo mezani ili kuwapa mwanga wajumbe wajue undani wake) ·