KUKUA NA KUIMARIKA ROHONI
“ Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli ” (Luka 1:80) “ Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima na neema ya Mungu ilikuwa juu yake ” (Luka 2:40) “ kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiogoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu ” (1Petro 2:2) Mtu anahitaji kukua rohoni na kuongezeka nguvu kwa sababu :- anazaliwa akiwa mchanga rohoni (immature). Mistari hii inatuonesha wazi kwamba mtu anatakiwa kukua sio tu mwili bali na roho yake pia, kuongeza hekima ndani ya mtu na neema juu yake. Ili awe na msingi wa mafanikio katika kila Nyanja . “ Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama roho yako ifanikiwavyo ” (3 Yoh 1:2) Kusudi la Mungu ni tufanikiwe katika maeneo yote ya maisha sio tu machache, sio unafanikiwa maswala ya kiuchumi halafu ndoa inakushinda, au unafanikiwa kielimu halafu sehemu ya...