Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 29, 2015

UENDESHAJI WA VIKAO

UENDESHAJI WA VIKAO Vikao ni mahali ambapo muafaka juu ya mambo mbalimbali huweza kufikiwa au kutofikiwa.Aidha Vikao ni mahali ambapo mipango na njia za kufikiwa kwa malengo hujadiliwa,huwekwa wazi na kila mjumbe hupewa jukumu la kufanya(maamuzi hufikiwa).Katika mada hii nitajikita katika kueleza mambo ya msingi ambayo kila mjumbe anapaswa kuzingatia ili kuleta ufanisi wa yaliyokusudiwa katika kikao.Si hivyo tu bali nitaeleza wahusika katika kikao na nafasi (majukumu) zao. Nini maana ya kikao?    Kikao ni majadiliano yanayofanywa baina ya wadau au kundi au jamii ya watu wenye kuwa na mlengo wa kushirikiana jambo fulani.Majadiliano hayo hufanywa kutokana na mada au agenda iliyowakusanya wahusika.Hii ina maana kwamba bila agenda hakuna kikao na kikao bila agenda ni kupoteza muda .  Ni majadiliano ambayo huwa na lengo la kupata maamuzi au maazimio ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu.Uongozi unaojali ushirikishwaji wa jamii ya watu lazima ujenge utaratibu wa kuwa ...