MCHANGO WA JAMII KATIKA MAENDELEO
Tupo katika harakati za kulijenga Taifa letu ili kulifanya lifurahiwe na watu wetu.Rais wetu wa awamu ya tano anayo nia ya dhati kutufikisha kule tunakotaka.Ninawaomba wadau mbalimbali tusaidiane katika kuchangia na kupongeza jitaihada hizi. Mashirika ya dini na Umma tuungane pamoja katika kufikia azma hiyo. Mfano Wakristo tukitenga siku moja ya kutoa sadaka na michango kwa ajili ya Madawati si tutafungua madirisha ya mbinguni ? au Wasanii maarufu watafanya maonesho mangapi kupata madawati ya Mkoa ? au Timu maarufu zitafanya mipambano mingapi ili kumaliza suala hili ? Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi juu ya namna bora ya kuiletea Nchi yetu maendeleo hasa namna ambavyo wanajamii wanavyoshirikishwa.Yapo mengi tunaweza kuyafanya kama nia yetu ni kupata maendeleo.Fuatilia maoni na mapendekezo yangu juu ya hili. MADHEHEBU. Hili ni kundi linalokusanya fedha nyingi na pengine hata kodi hazilipiwi.Kama viongozi kupitia Umoja wao watakaa na kuazimia ifanyike ibada ...