MCHANGO WA JAMII KATIKA MAENDELEO
Tupo katika harakati za kulijenga Taifa letu ili kulifanya lifurahiwe na watu wetu.Rais wetu wa awamu ya tano anayo nia ya dhati kutufikisha kule tunakotaka.Ninawaomba wadau mbalimbali tusaidiane katika kuchangia na kupongeza jitaihada hizi.
Mashirika ya dini na Umma tuungane pamoja katika kufikia azma hiyo.
- Mfano Wakristo tukitenga siku moja ya kutoa sadaka na michango kwa ajili ya Madawati si tutafungua madirisha ya mbinguni ? au
- Wasanii maarufu watafanya maonesho mangapi kupata madawati ya Mkoa ? au
- Timu maarufu zitafanya mipambano mingapi ili kumaliza suala hili ?
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi juu ya namna bora ya kuiletea Nchi yetu maendeleo hasa namna ambavyo wanajamii wanavyoshirikishwa.Yapo mengi tunaweza kuyafanya kama nia yetu ni kupata maendeleo.Fuatilia maoni na mapendekezo yangu juu ya hili.
Hili ni kundi linalokusanya fedha nyingi na pengine hata kodi hazilipiwi.Kama viongozi kupitia Umoja wao watakaa na kuazimia ifanyike ibada moja kwa ajili ya kutafuta madawati kwa wanafunzi si itakuwa rahisi kuyapata .Kama wamekuwa wakifaulu kuwa na maombi ya pamoja kuliombea Taifa je itashindikana nini kuandaa ibada moja tu kwa miezi sita au hata mwaka ili kutafuta fedha za kununua madawati ? Mimi ninaona inawezekana kupata madawati hayo.Viongozi wa TEC,PCT,ADVENTISTA WASABATO,WAISLAMU,CCT N.K tafakarini hili ?
WASANII MAARUFU
Hili ni kundi kubwa linaloweza kukusanya fedha nyingi kwa wakati mmoja.Hapa ninamaanisha waimbaji maarufu wa nyimbo za Injli,Bongo fleva,Taarabu,Filamu,Vichekesho,Katuni na wengine wengi.Jamani ninyi ni kundi muhimu sana katika Nchi yetu.Tunajua mnaweza kuwahamasisha watu kufanya jambo lolote na likafanikiwa.
Kupitia mawakala wenu waliotapakaa Nchi nzima kwa nini msilitakafari hili ?
TIMU MAARUFU ZA MICHEZO
Hakuna asiyejua kuwa Timu kubwa na zenye majina zikikutana fedha nyingi hupatikana .Mimi ninaona kama Timu hizi zikiandaa mchezo mmoja wa Dakika 90 fedha za madawati zinaweza kupatikana .Sasa wadau wa michezo angalieni wanafunzi wanavyoteseka.Rais wetu ana nia njema.Tuache malumbano na badala yake tulisaidie Taifa.
HITIMISHO
Kama tukifanya mema tutalipwa kuliko tunavyo fikiria,tuungane pamoja kulitafakari hili kama njia muhimu na rahisi kuifanikisha ElimuMsingi Bure.Tuache lawama badala yake tuungane katika mambo ya msingi.
Imeandaliwa.
Na,
AYOUB J.LEO
Maoni