UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI

Na,

Rev. Innocent Kamote

       SEHEMU YA 1:  KITABU CHA DANIELI.
                                         SOMO LA 1:  KUPITIA  YA KITABU CHA DANIELI:
A;           D A N I E L I:
                Lengo la 1;  - Eleza Historia fupi ya Danieli.
Danieli – jina lake lina maana “Mungu ndiye Hakimu wangu”.  Alikuwa mmojawapo wa mateka waliochukuliwa na mfalme Nebukadneza katika mwaka 605 KK. Kutoka Yerusalemu na kupelekwa Babeli.  Aliishi kipindi chote cha utumwa cha miaka 70 huku akiwa nabii na mwandishi wa Kitabu cha Danieli.  Tunamfahamu Danieli jinsi alivyokuwa mcha Mungu, tukisoma Eze.14:14-20.  Inavyoonekana alitokea na ukoo wa daraja la juu huko Yerusalemu.  Danieli hakuwahi kuoa, inawezekana alifanywa towashi kwa sababu alifanya Kazi katika  Kasri la mfalme.
B.            KITABU CHA DANIELI:
                Lengo la 2 :  Taja tarehe na makusudi ya kuandikwa kitabu hiki.
     Kitabu hiki kiliandikwa kati ya mwaka 536 – 530 KK. Kikiwa na makusudi mawili.
1.        Kuwatia moyo mabaki huko Babeli kuwa utumwa ulikuwa sio mwisho wa taifa lao.
2.        Kuwaonyesha watu wa Mungu kuwa Mungu ndiye mtawala wa mataifa yote.
-Yesu amekithibitisha kitabu kuwa kiliandikwa na Danieli.
                Lengo la 3:  Eleza mgawanyo wa Kitabu hiki:
                     Kitabu hiki kimegawanyika katika sehemu kuu tatu:
1.        Historia fupi ya Danieli toka Yerusalemu hadi Babeli –(Dan. 1:1-21)
2.        Ujumbe wa Danieli kuhusu utawala wa Mungu juu ya mataifa yote (2:1)
3.        Maono ya Danieli (8:1  -  12:13)
Sura ya kwanza iliandikwa kwa lugha ya Kiebrania wakati sura zingine zimeandikwa kwa lugha ya Kiaramu.
Lengo la  4:  Eleza mambo maalum ya kipekee yaliyomo katika Kitabu cha Danieli
     Kitabu cha Danieli kina mambo ya kipekee nane.  Nayo ni:-
    1. Kitabu kifupi kuliko vitabu vya Manabii wote ambacho watu wanasoma na kujifunza mno.
    2. Unabii wa Danieli umenukuliwa sana katika A/Jipya.
    3. Ni kitabu cha Apokilasi cha A/Kale kinachoelezea mambo ya siku za mwisho.
    4. Ni kitabu pekee kinachoelezea ujio wa kwanza wa Masihi katika Dan. 9:24-27
    5. Kinaelezea zaidi maisha ya Mwandishi, Tabia, Hekima na Maombi yake.
    6. Kina maombezi ambayo ni mfano wa maombezi ya kuwasamehe watu wa taifa lake kwa kumkumbusha Mungu ahadi zake.
    7. Habari za Danieli na rafiki zake zinapendwa mno.
    8. Maandishi yaluiyoandikwa na kutangaza yamekuwa methali inayotumiwa sana leo.
Lengo la 5: elezea Dola na mji wa Babeli na makusudi ya huduma ya Danieli.
     Mji wa Babeli ulijengwa Kusini kando ya mto Efrata.  Hali ya hewa na maumbile ya asili yalifanya mji wa Babeli uwe na watu wengi.  Mfalme Nebopolasa alikuwa ndiye mwanzilishi wa Dola ya Babeli na kukuzwa sana na mtoto wake aitwaye Nebukadneza.
                Dola ya Babeli ilipokuwa na nguvu ikaiangusha Ashuru na kuteka Palestina na Misri.  Kutokana na 2Nyak. 36:15-17, Yuda ilichukuliwa uhamishoni kwa sababu waliacha sheria ya Bwana.  Mungu akawahukumu watu wake kwa kuwaweka katika utumwa mikononi mwa Wakaladayo.  Danieli aliinuliwa kuwa Nabii ili awatie moyo mabaki waliokata tamaa kuwa Mungu ndiye anamiliki na kuiongoza historia.
MASWALI:
  1. Kitabu cha Danieli kiliandikwa mwaka gani?
  2. Makusudi ya kuandikwa kwa kitabu hiki ni:
(a)     _____________________________________
(b)     _____________________________________
  1. Kitabu hiki kimegawanywa katika sehemu ngapi?.  Zitaje.
  2. Taja mambo manne ambayo ni ya kipekee katika Kitabu hiki.
  3. Dola ya Babeli ilikua zaidi katika kipindi cha mfalme _______________
SOMO LA 2: UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI.
PAMBANO LA KWANZA MAPAMBANO DHIDI YA MASWALA YA IMANI (11-21)
                Lengo la 1: Eleza pambano la kwanza la Imani la Danieli na rafiki zake. 
                                       Je, walishindanaje?, nini matokeo ya kushinda kwao?
Baada ya Danieli kufika Babeli, mfalme Nebukadneza aliamua Danieli na wenzake  wapate elimu ya Ukaldayo kuhusiana na lugha na mila za Babeli. Hii itawafanya watumike vizuri.  Ili kutimiza kusudi hili, mfalme Nebukadneza alifanya mambo yafuatayo:-
Kwanza:  Aliwapa uraia wa Babeli kwa kubadili majina yao kama ifuatavyo:
Kiebrania:
    1. Danieli (Mungu ni Hakimu wangu – Belteshazzar (Mwana wa Bel)
    2. Hanania (Mungu ni mwenye Neema) –Shadrack (Uvuvio wa Rachi)
    3. Mishaeli (Nani kama Mungu) – Meshaki (nani kama Shaki)
    4. Azaria (Mungu anasaidia) – Abdinego (mtumishi wa Nebo)
Pili:  Aliamua kuwapa vyakula ambavyo vilitolewa kwa miungu, ili wawe na afya nzuri.  Katika hili, Danieli na wenzake waliamua kutojitia unajisi kwa kula vyakula vilivyotolewa kwa miungu.  Wakaomba wale mboga na maji kwa muda wa siku kumi.  Mungu akawajalia wakaonekana wana afya nzuri zaidi kuliko wenzao.  Kwa ajili ya kumcha Mungu,  Mungu aliwapa hekima na ufahamu katika masomo yao.
Je, tunajifunza nini kutokana na tabia, mwenendo, na Imani ya Danieli?               
     Msingi wa jaribu lao la kwanza ilikuwa ni kuwafanya hao Vijana waikane imani yao na kuishi kama Wababeli.  Hawa vijana hawakukubali.  Mara nyingi Jumuiya tunazoishi zinataka tufanane nazo bali kama watu wa Mungu tuishi kati yao tukiwa tunamcha Bwana.
PAMBANO LA PILI: UCHAWI DHIDI YA HEKIMA YA MBINGUNI (Dan. 2:1-49)
Lengo la 2: Tambua vitu vilivyokuwemo katika sanamu aliyoiona mfalme Nebukadneza.
Mungu alimwonyesha mfalme Nebukadneza ndoto iliyohusiana na falme  mbalimbali  zenye nguvu.  Hizi falme zingehusika sana kwa Taifa la Israeli.
1.        Kichwa cha Dhahabu – Dola ya Babeli (mamlaka) – Dan. 2:37
2.        Kifua na mikono ya fedha – Dola ya Uajemi na Umedi (Serikali ya Seri) – Dan. 2:39.
3.        Tumbo na viungo vya shaba – Dola ya Uyunani (utamaduni ) – 2:39
4.        Miguu ya chuma – Dola ya Rumi – 2:39
5.        Nyayo zilizo nusu chuma na nusu udongo – Jumuiya ya Mataifa 10 chini ya mpinga Kristo – 2:40
6.        Jiwe lisilochongwa na mwanadamu – Ufalme wa miaka elfu wa Yesu Kristo – 2:42.
Lengo  la 3:  Eleza umuhimu wa ndoto ya Nebukadneza na Nyakati za Mataifa.
                Sanamu hii inaelezea mambo yatakayotokea katika historia.  Kipindi hicho ni kuanzia mfalme Nebukadneza hadi kurudi mara ya pili kwa Yesu Kristo.  Nyakati za mataifa ni wakati nchi ya Israeli itakapokaliwa na mataifa mengine. 
Pili, Ndoto hii ni muhimu kwani lilikuwa shindano kati ya uchawi dhidi ya Hekima ya Mungu.  Mfalme Nebukadneza alitaka kukumbushwa  ndoto aliyoota kwanza halafu aambiwe tafsiri.  Wachawi walipoitwa walishindwa kuielezea na kuhukumiwa kifo. Katika mistari ya 17-28 tunaona hali nzuri ya Kiroho ya Danieli na rafiki zake.
-          Walimwomba Mungu ili afunue ndoto hii  (17,18)
-          Walimshukuru Mungu baada ya kupata jibu (19-23)
-          Walimpa utukufu Mungu katika yote (27,28)
Matokeo yake:-
(a)     Mfalme Nebukadneza alitambua uwezo wa Mungu wa Danieli
(b)     Danieli alipewa zawadi kubwa nyingi.
(c)      Akapandishwa cheo cha Uliwali
(d)     Rafiki zake nao wakaongezewa cheo.
Je, Tunajifunza nini katika pambano hili?

PAMBANO LA TATU: KUABUDU SANAMU DHIDI YA KUMWABUDU MUNGU

(Dan. 3:1)
Lengo la 4: Eleza matokeo ya ushindi wa vijana watatu wa Kiyahudi:
                Mfalme Nebukadneza badala ya kunyenyekea na kumwabudu Mungu aliyemwonyesha ndoto hii, anaamua kutengeneza sanamu.  Anaamuru watu wote waisujudie.  Watu wote wanasujudu isipokuwa Shadrack, Meshaki na Abednego.  Matokeo yanakuwa hivi.
-          8-12 – Viongozi wenzao wanawashtaki
-          13-15 – Mfalme Nebukadneza anawapa nafasi ya kutekeleza agizo ili kuepuka hukumu.
-          16-23 – Hukumu inatekelezwa kwa kutupwa kwenye tanuru la moto.
-          24-27 – Bwana anajifunua na kuwaokoa watu wake.
Matokeo ya ushindi huu unaleta mema:
(a)     Mfalme Nebukadneza anamtambua Mungu kuwa ndiye amewaokoa.
(b)     Watu wanaamriwa kutomnenea lisilopasa Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abednego.
(c)      Vijana hao watatu wakabandikwa vyeo.
Je, tunajifunza nini katika vita hivi?
Kuwa tayari kufa kwa ajili ya Yesu Kristo kuliko kumwasi Mungu kwa kuogopa mateso.  Mungu mwenyewe ana uwezo wa kutuokoa katika mateso hayo.
PAMBANO LA NNE:  KIBURI CHA MFALME DHIDI YA UTAWALA WA MUNGU.(Dan. 4:1-37)
Lengo la 5:  Je, tunapata kweli gani katika Dan. 4?
Katika sura hii mfalme Nebukadneza anaeleza ushuhuda wake.
4:18                      Anaelezea ndoto yake ya mti uliokua sana na baadaye kukatwa.
19-27  -                   Danieli anaeleza tafsiri ya ndoto kuwa mfalme Nebukadneza  kuondolewa ufalme na kula majani kama mnyama wa porini kwa miaka saba.
28-36   -                  Mfalme anaelezea kutimia kwa ndoto aliyoota
37         -                  Mfalme anamtambua Mungu.
Ukweli tunaopata hapa ni kuwa Mungu anahusika katika kung’oa na kuweka
Wafalme na viongozi mbalimbali.  Je, tunapata fundisho gani?
(a)     Kabla Mungu hajaleta hukumu humpa maonyo ili ajirekebishe
(b)     Mungu hapendi mtu aliye na kiburi, hivyo humshusha.
PAMBANO LA TANO:  KUFURU YA MWANADAMU DHIDI YA UTAWALA WA Mungu (Dan. 5:1-31)
Lengo la 6:  Eleza dhambi ya Belshazzar.
                Karamu hii ilifanyika mwaka 539 KK, wakati  wa mfalme Belshazzar.
Alitawala Babeli wakati baba yake Naboduis alikuwa anaongoza vita sehemu nyingine.  Wakati huu mji ulikuwa umezingirwa na majeshi ya  Wamedi na Waajemi.  Matukio  wakati wa karamu:
-          Karamu  yaandaliwa na watu wasifu miungu yao – 5:1,2
-          Akiwa amelewa aagiza vyombo vya hekalu la Yerusalemu viletwe na kutumiwa –(Mst. 2-4)
-          Kitanga chaandika maneno na wenye hekima kujaribu kusoma (Mst.5-8)
-          Danieli aletwa kusoma na kutafsiri maandishi (Mst. 9-31)
Maandiko: MENE, MENE TEKELI , NA PERESI
MENE – Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha.
TEKELI – Umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.
PERESI – Ufalme wako umegawanyika nao wamepewa Waamedi na Waajemi.
Dhambi ya Belshazzar ilikuwa ni kufanya dhambi kwa makusudi kutumia vyombo vitakatifu vya hekalu la Yerusalemu.  Alikuwa amesikia na kumfahamu Mungu huyo.
Je, tunajifunza nini? Tusifanye dhambi kusudi kwani tutakuwa tunamkufuru  Roho Mtakatifu.
PAMBANO LA SITA:  WIVU DHIDI YA BARAKA ZA MUNGU JUU YA MTU WAKE.(Dan. 6:1-28)
Lengo la 7: Eleza jinsi Mungu anavyowatetea watu wake.
                Danieli anapewa uongozi tena katika ufalme wa Dario huko Babeli.  Huyu Dario siyo yule mfalme mkuu anayetajwa katika Agano la Kale,  huyu inawezekana alikuwa kiongozi aliyewekwa na mfalme Koreshi kusimamia utawala.  Wawili waliomo katika Baraza la uongozi wanamwonea wivu Danieli kutokana na utendaji mzuri wa kazi.  Matukio yanakuwa ifuatavyo:
-          Wanamshawishi mfalme kuandaa sheria ya kutokuomba kwa Mungu ila kwa mfalme kwa siku 30. (4-9)
-          Daniel aendelea kuomba na akamatwa na kutupwa katika tundu la simba(10-17)
-          Mungu amwokoa Danieli na maadui kuadhibiwa (18-24)
Matoke ya ushindi wa Danieli mfalme Dario anawataka watu kumheshimu Mungu wa Danieli.  Pia Danieli akaendelea kufanikiwa.
Je, tunajifunza nini katika sehemu hii?
Mtu anapomtegemea Mungu, Mungu humfanikisha na kukutana mahitaji yake.
MASWALI:
  1. Lengo la jaribu la kwanza lilikuwa lipi ?. Je, walishindaje jaribu?
  2. Taja maana ya vitu vilivyomo katika sanamu aliyoiona mfalme Nebukadneza.
  3. Matokeo ya ndoto aliyoota mfalme Nebukadneza ni:-
(a)     _____________________________
(b)     _____________________________
(c)      _____________________________
(d)     _____________________________
  1. Nini matokeo ya ushindi ya vijana watatu katika Danieli sura ya 3?
  2. Unapata fundisho gani kutokana na adhabu ambayo Mungu anayoitoa kwa mfalme Nebukadneza? (4:1-37)
  3. Ni dhambi gani aliyoifanya mfalme zbelshazar? (Dan. 1:1-3)
  4. Kuna faida zipi za mtu kumtegemea Mungu?
  5.  
                  SOMO LA 3 :  MTAWALA WA ULIMWENGU ANAYEKUJA:
A.             MAONO YA WANYAMA WANNE (Dan. 7:1-28)
                Lengo la 1:  Linganisha ndoto ya Nebukadneza (2) na Maono ya Danieli – sura  7:
               
Kichwa cha Dhahabu Dan.2:37
Simba mwenye mabawa matatu ya tai Dan.7:4
Babeli Dan.2:37
Kifua na mikono ya fedha Dan. 2:39
Dubu na mifupa mitatu ya mbavu kinywani – Dan. 7:5
Uajemi 
Ilizishinda Misri, Ashuru, Babeli. Dan. 2:39
Tumbo na viuno vya shaba 2:39
Chui mwenye mabawa manne  7:6
Uyunani
Miguu ya chuma 2:40
Mnyama wa kutisha 7:7
Rumi  - 7:23
Nyayo nusu chuma, nusu udongo –2:41
Pembe 10 na pembe ndogo 7:8
Mataifa na Mpinga Kristo – 7:24
Jiwe lisilo kazi ya mwanadamu – 2:42
Mfano wa Mwanadamu –7:13-14
Yesu Kristo na Ufalme wa miaka elfu – 7:26-28
Maono haya yalionwa na Danieli wakati wa mfalme Belshazar.  Maono haya yanayoonyesha kuwa mfumo wa utawala wa kibinadamu utatoweshwa na ufalme wa Mungu utasimamishwa milele.  Kabla ya Yesu kutawala atakuja mpinga Kristo na kujitangaza kuwa mungu na kuwatesa watakatifu.  Atatawala kwa miaka mitatu na nusu baada ya kuwaondoa  wafalme 3 kati ya 10.  Baada ya hapo ataangamizwa na Kristo kutawala pamoja na watakatifu .
B.             MAONO YA KONDOO MUME NA BEBERU (MBUZI DUME) – Dan. 8:1-27.
Lengo la 2:  Elezea vitu na mifano katika maono haya. Eleza umuhimu wake katika
                        unabii  wa Kibiblia.
Maono ya yalionwa wakati wa mfalme Belshaza. Sura hii inaonyesha kuinuka na kuanguka kwa Dola za Uajemi na Uyunani.
1.        KONDOO MUME – 539-333 KK – Ana pembe mbili ndefu ambazo ni Uajemi
  na Umedi.  Pembe ndefu zaidi ni Uajemi – utawala ulikuwa mkubwa.
2.        BEBERU  - 33 – 165 KK – Huyu ana pembe moja kati ya macho yake.  Hii ni
Dola ya Uyunani ikiongozwa na Alexander- iliangusha ufalme wa Uajemi.  Pembe nne zilizozuja ni wafalme waliozuka baa ya Alexander kufa.
(a)     Kasanda - Makedonia
(b)     Lysichus – Asia ya Kati
(c)      Seleucus – Syria
(d)     Ptolemy – Misri
3.        Mfalme anayetokeza mwisho wa ufalme wa Uyunani ni Antonio Epifawe ambaye  mkali, jeuri, mdanganyifu na mwenye nguvu.  Alilinajisi hekalu la Mungu kwa kutoa vitu najisi.  Lakini baada ya siku 2300 za dhabihu ya asubuhi na jioni (siku 1150) Antonio alitimuliwa katika mwaka 165 KK, hekalu likatakaswa.
C.            MAOMBEZI YA DANIELI (Dan. 9:1-23)
                Lengo la 3:  Eleza umuhimu wa kuombea yale Mungu aliyoahidi kutimiza.
Katika mwaka wa kwanza wa kutawala mfalme Dario mwaka 539 KK. Danieli kwa kusoma vitabu aligundua kuwa myda wa utumwa wa miaka 70 umeisha kama alivyotabiri Nabii Yeremia, ili yatokee.  Danieli anaomba na kutubu dhambi za watu wake.  Matokeo ya maombi yake, Mungu anampa maono na maelezo ya majima Sabini.
                Je, tunajifunza nini?  Inatupasa kuombea mambo yale Mungu aliahidi kutufanyia ili yapate kutokea na kuonyesha zaidi yaliyoko mbele yetu.
D.            MAJUMA SABINI  -9:24-27
                Lengo la 4:  Fafanua haya Majuma Sabini:
1.        Tangu kutolewa amri ya kujengwa mji na kuujenga itachukua majuma saba ambayo ni miaka 49 (Ezra na Nehemia)
2.        Kipindi cha pili ni cha majuma 62 kutoka mji kujengwa hadi kukataliwa kwa Masihini miaka 434.
3.        Kipindi cha mwisho ni juma moja lijalo wakati wa mpinga Kristo ambapo Mungu atashughulika na Israeli kama taifa.  Israeli wataumiliki mji mtajkatifu katika kipindi cha kwanza cha miaka 3 na nusu na kipindi xha pili kitamilikiwa na watu wa mataifa (Ufu. 11:2).  Israeli itateswa sana.
4.        (a)    Dan. 9:24-27 inahusika na watu wa Danieli na mji Mtakatifu maana yake
Israeli na mji wa Yerusalemu.
                     (b)   Majuma Sabini ni miaka 490 iliyogawanywa sehemy kuu tatu:
                                Majuma 7 (miaka 49), majuma 62 (miaka 434), na juma moja (miaka 7)
     (c)  Kuangamizwa kwa mji na patakatifu pake ni mwaka 70 AD., ambapo
                Warumi waliuangamiza Yerusalemu na hekalu lake.
    (d)  Danieli hakioni kipindi cha Kanisa kwa sababu Mungu alitaka aonyeshwe
                mambo yanayohusiana na taifa la Israeli.
5.        Katika Juma la 70 Wana-Israeli
(a) Watafanya agano na mpinga Kristo
(b) Baada ya miaka 3 na nusu agano litavunjika, mpinga Kristo ataondoa
        uhuru wa kuabudu.
(c) Kutokana na mateso mwatamhitaji Masihi.
6.        Katika Majuma 70 mambo haya yatafanyika kwa ajili ya Yerusalemu na Israeli
(a) Kukomesha dhambi
(b) Kusamehe uovu
(c) Kuleta haki ya milele
(d) Kutia mhuri maono na unabii
(e) Kupaka mafuta patakatifu sana.
  1. MARUDIO NA MAPIITIO:
Lengo la 5:  Eleza jinsi maendeleo ya Ufunuo katika Dan. 2,7,8,9,na umuhimu Wake.
Maendeleo ya ufunuo katika Dan. Sura 2,7,8,9, inaanzia kwenye maelezo ya jumla katika sura ya 2 na katika sura zingine tunaelezwa kwa undani zaidi jinsi mambo yatakavyokuwa.  Umuhimu wa maendeleo ya ufunuo hatua kwa hatua unatufundisha kuwa ili tuipate kweli lazima tusome na kupiitia sura yote.
MASWALI:
  1. Chora jedwali na ulinganishe ndoto ya mfalme Nebukadneza (Dan. 2:1-42) na maono ya Danieli katika sura ya saba.
  2. Katika Dan. 8:1-27
(a)     Kondoo mume ni nani?
(b)     Beberu ni nani?
  1. Je, kuna umuhimu gani wa kuombea mambo ambayo Mungu ameahidi kutufanyia?
  2. Chora mchoro unaofafanua majuma Sabini.
SOMO LA  4:  SIKU ZIJAZO ZA TAABU:
A.             UTUKUFU WA YESU KRISTO.
               
                Lengo la 1:  Taja vitu vinavyofanana na maono aliyoyaona Yohana katika Ufunuo na yale ya Dan.10:5,6.
               
VITU
DANIELI
UFUNUO
MAANA
Mavazi
Nguo za Kitani (Mst.5)
Vazi lililofika miguuni (Mst.13)
Hekima
Mshipi
Dhahabu (Mst.5)
Dhahabu (Mst. 13
Thamani mno.
Macho
Taa za moto (Mst.6)
Mwali wa moto (Mst.14)
Ana uwezo wa kuona
Sehemu ya chini
Rangi kama ya shaba (Mst.6)
Shaba iliyosuguliwa (Mst.15)
Imara
Sauti
Kama ya umati wa watu (Mst.6)
Ya maji mengi (Mst.15)
Mamlaka na Nguvu
                Umuhimu wa maono haya yalikuwa na lengo lifuatalo:
1.        Kuwatia moyo na kuwapasha watu wa Mungu juu ya mambo yajayo
2.        Maono haya yalimpa kuelewa yale yaliyotabiriwa muda yatakapotimia.
3.        Maono haya yalikuwa jibu la maombi ya Danieli ya muda wa siku 21.
Maono haya Danieli aliyapata mnamo mwaka wa tatu wa utawala wa mfalme Koreshi wa Uajemi.
B.             MAPAMBANO  YA  KIROHO –Da. 10:13-21.
                Lengo la 2:  Elezea vita vya Kiroho vinavyofunuliwa katika sura hii.
Sura hii inatoa mfano wa upinzani dhidi ya Mungu unaotawala katika anga hili.  Majibu ya maombi ya watumishi yanacheleweshwa kutokana na upinzani wa wakuu wa giza wanaowapinga malaika watakatifu waletao majibu.  Asifiwe Bwana kwani hakuna mamlaka inayoweza kuzuia maombi yetu kwenda kwa Mungu.  Tukivumilia majibu yanaweza kuletwa.  Katika sura hizi tunajifunza kuwa kuna malaika wa Mungu wanaosimama kwa niaba ya mataifa wakiongozwa na Mikaeli.
C.            MTIRIRIKO WA HISTORIA KUTOKA DOLA YA UAJEMI NA UMEDI HADI MWISHO WA NYAKATI.
1.        UAJEMI NA UYUNANI (Dan.11:1-4)
Lengo la 3: Onyesha mambo muhimu katika unabii kuhusiana na Uajemi na  Uyunani.
Wafalme wane:
(a)     Koreshi – 539 –529 KK – miaka10 (Ezra 1:1)
(b)     Artashasta – 529 – 522 KK – miaka 7 (Ezra 4:7.)
(c)      Ahasuero (Xerxes)
(Dario Hystaspes) – 521 – 486 KK – miaka 35 (Esta 1:1)
(d)     Eexes I – 486 – 468 KK – miaka 18.
(Huyu ndiye aliyekuwa tajiri kuliko wafalme wote.  Utajiri wake na jeshi la watu 800,000 lilimchochea kupigana na Wayunani.  Katika vita hivi alishindwa vibaya na Wayunani au Wagriki.  Dola ya Uajemi ilidumu kwa miaka 200 (Mst.3,4) – 538 – 333 KK.Mfalme hodari ni Alexander wa Ugriki aliyeupindua na kuangusha dola ya Uajemi katika mwaka 333.  Alifariki mwaka 323 KK bila kuwa na wana wa kutawala.  Dola ya Ugriki iligawanyika katika sehemu kuu nne chini ya wakuu wa majeshi:
(i) Kasanda              - Makedonia
(ii) Lysmauhus – Asia
(iii) Selukia – Syria
(iv) Ptolemy – Misri
  N.B:  Katika unabii wa sura wafalme wawili wanahusika:
                -Selukia wa Syria  (Mfalme wa Kaskazini)
                -Ptolemy wa Misri (mfalme wa Kusini)
2.        FALME ZA PTOLEMY NA SELUKIA HADI ANTIOKIA EPIFANE –Dan.11:5-20.
Lengo la 4: Eleza umuhimu wa Ptolemy na Selukia katika historia ya Biblia.
                       Hawa ni muhimu kwa sananu Israeli ilikuwa kati ya Falme hizi mbili,  hivyo ilihusika sana katika historia yao.  Kati ya 323 –178 KK Israeli ilitawaliwa na Ptolemy mfalme wa Kusini.  Hivyo tuangalie unabii ulivyotumia.
Mst. 5:             Ptolemy I lagus au Soster ni mfalme wa Kusini aliyetawala Misri, Arabia, Libya, Ethiopia n.k.  Selukia I (mshindi) Nikano alikuwa mfalme wa Kaskazini.
Mst. 6:             Ptolemy II Philadephus alimwoza binti yake Berenise kwa Selukia Antiokia II Theoss mwenye mke aitwaye Laodice, ili  kuleta mapatano.  Baada ya kifo cha mfalme wa Kusini, Antiokia alimtaliki Berenice na kumrudia mkewe Laodice.  Baadaye Laodice akamuua mume wake kwa sumu na kuwuua Berenice na mtoto wake.  Hivyo mtoto wa Laodice Seleukia Callinicus akatawala.
Mst. 7-9           Ptolemy III Euergette akamshambulia Seleukia Callinicus na kumshinda na kuteka mateka ili kulipiza kisasi.
Mst.10-12        Wana wa mfalme wa Kaskazini ni Selecus (mkubwa aliyeuwawa kwa sumu na Antiokia aliyetawala kwa miaka 37.  Akashambulia Misri akashindwa na Ptolemy Epifanes.
Mst.13-16        Akishirikiana na waasi wa Kiyahudi, Antiokia akamshinda mfalme wa Kusini na kuimiliki Israeli.
Mst. 17            Antiokia III baada ya ushindi alimpa Ptolemy Epifane dada yake Cleoptra awe mkewe.
Mst.18-19        Antiokia III alitanua ufalme wake hadi Asia ya Kati na kushindwa na Warumi wakiongozwa na Seipto.
Mst. 20:           Seleukia Philopater alitawala na kutoza Kodi kwa ukatili akauwawa kwa sumu na mtumishi wake Heliodorus.
                        Je, tunajifunza nini?  Mungu ndiye anaweka na kung’oa wafalme atakavyoYeye.
3.        ANTIOKIA EPIFANE –Dan.11:21-45
Lengo la 5:  Eleza mambo muhimu ya unabii kuhusiana  na Antiokia Epifane
                          aliyotumia katika Historia.
        Mst. 21 – Tabia yake Antiokia Epifane alikuwa mdanganyifu, mwenye kiburi na mjanja.  Yeye alikuwa amewekwa ndani huko Rumi.  Alipata ufalme kwa hila alimfanya mtoto wa kaka yake Demeterio kuwa mfungwa badala yake.  Akatawala Syria kwa kujidai anamshikia madaraka kwa kitambo kidogo.
        Mst. 22-24 – Hata shika mapatano yake bali akishirikiana na watu wachache atavamia Mikoa tayari na kuteka mali ambayo aliwahawia rafiki zake.
        Mst. 25-28 – Antiokia Epifane atakusanya majeshi na kumshambulia mfalme wa Kusini na kumshinda Ptolemy Philometer na kufanya mkataba ambao haukudumu.
        Mst. 29-30 – Alivamia tena ufalme wa Kusini, lakini wakati huu alishindwa kwa Ptolemy Philometer akisaidiwa na Warumi.  Warumi walimwamuru Antiokia kuondoa majeshi yake.
        Mst. 31-35 – Baada ya kurudi kutoma Misri huku ameshinea, hasira zake alizielekeza kwa Wayahudi na kuondoa shughuli za Ibada katika Hekalu.  Alifanya hivi akisaidiwa na Wayahudi waasi.  Akalinajisi  hekalu kwa kutoa vitu  vilivyonajisi.  Wayahudi wengine waliowaaminifu walishikilia Imani yao, Wengi kati yao waliuawa.
        Mst. 36-39 – Antiokia Epifane alimkufuru Mungu Aliye juu kwa kuondoa dhabihu zake na kunajisi Sabato, hekalu na watu wa Mungu.  Pia alidharau miungu na baba zake na kuleta miungu ya kigeni ya Wayunani (Jupiter olympius)
        Mst. 40-43 – Mfalme wa mwisho Kusini alivamia tena utawala wa Antiokia Epifane , lakini alishindwa tena.  Mfalme wa Kaskazini aliteka mali nyingi ya Wamisri.
        Mst. 44-45 – Habari za maadui kutoka Mashariki na Kaskazini ni majeshi Waajemi na Waapathi zikamsumbua.  Akaingia na kuwateka Wayahudi.  Lakini aliugua ugonjwa usioponyeka na kufa.
N.B:  Antiokia Wpifane alikuwa kivuli cha mpinga Kristo atakayekuja.
FALME  MBILI:
KUSINI (Ptolemy)                                                            KASKAZINI (Seleukia)
Ptolemy I Soster –323 –285                            Seleukia Nicator – 312-280
Ptolemy II Philadelphus –285-246   Antiokia I Sater – 280-261
Ptolemy III Euergetes – 246 – 221  Antiokia II (Theos) – 261 –246
Ptolemy IV Philopator – 221 –204   Selukia II Callinicus –246-226
Ptolemy V – Epifane – 204 – 181    Selukia III Ceranus –226-223
Ptolemy VI Philometa –181-145                      Antiokia III 223-187
                                                                                        Selukia IV –187-175
                                                                                        Antiokia IV Epifane –175-164
D.            WAKATI WA TAABU  – Dan. 11:36-12:13
                Lengo la 6:  Taja ushahidi ambao unayaweka matukio yaliyomo katika Danieli 12 kutoka katika Juma la Sabini.
                Dan 11:36 – 45 inazungumzia juu ya kutokea kwa mpinga Kristo atakaye vamia taifa la Israel na kujitangaza kwamba yeye ni Mungu anayetakiwa kuabudiwa.Atafanya kazi kwa miaka mitatu na nusu baadaye kuangamizwa.   
Ushahidi katika sura 12 unaonyesha kuwa wakati wa taabu utatokea katika kipindi nusu ya pili ya juma la Sabini.  Kipindi hicho kitakuwa cha miaka 3 na nusu.  Kipindi hicho kitaanza wakati mpinga Kristo amevunja mkataba wa amani na Wayahudi.
                                Matukio ya wiki ya sabini ni kama ifuatavyo:-
1.        Kitaanzishwa na ujio wa mpinga Kristo atakayeongoza mataifa kumi.
2.        Ataweka mkataba wa amani na Wayahudi  wa miaka saba. Baada ya miaka 3 na nusu mkataba utavunjwa.
3.        Atawageukia Wayahudi na kuwatesa kwa lengo la kuwaangamiza, lakini malaika Mikaeli atawasaidia na watakatifu kuokolewa.
4.        Kabla ya Mungu kuanzisha ufalme wake ataondosha utawala wa mpinga Kristo.
5.        Watakatifu waovu watafufuliwa kuingia katika aibu na watakatifu katika baraka ya milele.
MUHTASARI WA MATUKIO MUHIMU:
605 KK – Mateka wa kwanza kupelekwa Babeli akiwemo Danieli na rafiki zake
597 KK – Mateka wengine wapelekwa Babeli akiwemo Ezekieli
587 KK – Yerusalemu uliangamizwa na watu kupelekwa utumwani Babeli.
587 KK – Koreshi anakuwa mfalme wa Uajemi.
550 KK – Uajemi yaishinda Umedi
539 K K – Uajemi yaishinda Babeli
538 KK – Kundi la kwanza la Wayahudi wakiongozwa na Zerubabeli warudi Yerusalemu.  Kazi ya ujuzi wa Hekalu yaanza
516 KK – Hekalu laisha kujengwa. 
458 KK – Wakiongozwa na Ezra Wayahudi kundi la pili warudi Yerusalemu.
445 KK – Nehemia aenda Yerusalemu kama Gavana
333 KK – Alexander Mkuu aishinda Uajemi
323 KK – Dola ya Ugriki inagawanyika katika sehemu nne.
                    301-198 – Palestina ilitawaliwa na Misri (Ptolemy)
                    198 –143 – Palestina ilitawaliwa na Syria (Seleukia)
171 KK – Antiokia Epifane anakuwa mfalme wa Syria
168 KK – Antiokia Epifane alinajisi Hekalu la Wayahudi
165 KK – Wayahudi waliongozwa na Makabayo wanalikomboa Hekalu.
145 KK – Palestina yapata uhuru.
 63    -     Dola ya Rumi wateka Palestina
6                 - Kuzaliwa kwa Yesu
                 31 BK – Kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo
                 70 BK  - Kuangamizwa kwa Yerusalemu na Warumi.
MASWALI:
  1. Umuhimu wa maono ya sura ya 10 ulikuwa una lengo lifuatalo:
(a)     ______________________
(b)     ______________________
(c)      ______________________
  1. Katika sura ya 10:13-21 kuna vitu gani vya kiroho vinavyofunuliwa?
  2. Taja mambo ambayo wafalme hawa waliwafanyia Wayahudi:
(a)     Koreshi ____________________________
(b)     Antashasta _________________________
(c)      Ahasuero __________________________
  1. Antiokia Epifane anakumbukwa kwa matendo gani aliyowatendea Wayahudi?
  2. Taja matukio matano yatakayotokea katika juma la Sabini.
_______________________________________________________________________________________________________________
       SEHEMU YA 2 – KUANZA KWA MATUKIO YA SIKU ZA MWISHO:
                 
SOMO LA 5:  KITABU CHA UFUNUO:
                Lengo la 1:  Taja mambo matano yanayoelezea chanzo cha Ufunuo katika sura ya 1:-
                Mambo matano yaliyodhihirishwa katika sura ya 1 ni:-
1.        Ufunuo wa Yesu Kristo 1:1
2.        Ujumbe huu uliwasilishwa kwa Yohana kupitia Yesu Kristo, malaika na maono – 1:1,10-18
3.        Ujumbe huo uliletwa kwa Yohana – 1:1,4,9,2
4.        Alipewa ujumbe huu akiwa mfungwa katika kisiwa cha Patmo
5.        Walengwa wa ujumbe yalikuwa makanisa saba katika Jumba la Asia.
Kitabu hiki kiliandikwa wakati wa utawala wa Domitian aliyetaka watu wamwabudu kama Mungu.  Amri hii ilileta matatizo na mateso kwa wakristo.  Hivyo kitabu hiki kiliandika katika mazingira haya.
M A K U S U D I:
Lengo la 2:  Eleza kusudi la kuandikwa kwa kitabu hiki>
Kusudi la kuandikwa kitabu hiki liko katika sehemu tatu:-
1.        Nyaraka zilizoandikwa zilikuwa za kukemea makanisa yaliyoridhia dhambi bila kuikemea.
2.        Kutokana na mateso ya Domitian aliyetaka kuabudiwa – kitabu hiki kiliandika kuwatia moyo kuvumilia mateso na kuwa waaminifu hadi kufa.
3.        Kiliandikwa kwa ajili ya Kanisa la Kizazi chake ili kuwaonyesha waamini juu ya mapambano waliyo nayo dhidi ya majeshi ya shetani.  Jinsi kuja kwa pili kwa Yesu Kristo kutakavyokomesha utawala mwovu wa mpinga Kristo.
M H U S I K A:
Lengo la 3 :  Eleza mhusika mkuu linazungumzwaje:
                Mtiririko wa kitabu cha Ufunuo ni kuelezea kuja mara ya pili kwa Yesu Kristo (Ufu.1:7).  Mhusika Mkuu katika kitabu cha Ufunuo ni Yesu Kristo mwenyewe.  Yale aliyokwishafanya, anayofanya sasa na yale atakayofanya baadaye.
MWANDISHI NA TAREHE:
Lengo la 4: Orodhesha ushahidi wa Uandishi na Tarehe ya Kitabu cha Ufunuo:
                Kitabu hiki kiliandikwa na Yohana Mtume wakati wa utawala wa Kaisari Domitian mnamo mwaka kati ya 91-96 BK.  Ushahidi tunaopata ni matumishi ya maneno “Logos” “Nikao” na “Ekkenteo” (kushinda na kuchoma).  Pia ushuhuda wa Viongozi wa mwanzo wa kanisa kama Justin Martyr unathibitisha kuwa mtume Yohana aliandika, ushahidi wa ndani ya kitabu unahusiana na kuwa kifungoni kisiwani Patmo huko Asia ya Kati.
SEHEMU KUU ZA KITABU:
Lengo la 5:  Eleza sehemu kuu za Kitabu.
Katika Ufu. 1:19 Yesu mwenyewe anaelezea:-
A.       Utangulizi – 1:1-8
B.       Yale uliyaona 1:9-20
C.       Nayo yaliyopo 2-3
D.       Yatakayokuwepo baadaye – 4:1-22:6
(a)      Kanisa katika Utukufu – 4:1-5:14
(b)      Dhiki Kuu – 6:1- 19:21
(c)      Miaka elfu  -20:1-6
(d)      Gogu  na Magogu – 20:7-10
(e)      Kiti cheupe 2:11-15
(f)       Mambo yote mapya – 21:1-22:6
E.       Hitimisho  - 22:7-21
Maelezo ya Zaidi:
Ni maelezo ya kina kuhusiana na jambo lililokwisha elezwa tayari.
Sura ya 7         - Wayahudi 144 na waliovikwa mavazi meupe.
Sura ya10  - Malaika mwenye nguvu mwenye Gombo au kitabu
Sura 11:1-14 – Mashahidi wawili
Sura ya 12   -  Mwanamke, mtoto na Joka
Sura ya 13    - Wanyama wawili
Sura ya  14   -  144,000 (Israeli), mwisho wa Injili kuhubiriwa, Tangazo la Kuangushwa kwa Babeli, mavuno ya mwisho na shinikizo.
Sura ya 17    -  Wanyama wawili na kahaba mkuu
Sura ya 18  -    Babeli
MASWALI:
  1. Chanzo cha Ufunuo ni kipi?
  2. Taja makusudi matatu ya kitabu cha Ufunuo
  3. Nani mhusika Mkuu wa kitabu hiki?
  4. Taja sehemu kuu za kitabu hiki.
SOMO LA 6: KANUNI ZITAKAZOKUSAIDIA KUELEWA UJUMBE WA UFUNUO:
A.             MAONI MANNE NA MAANA ZAKE:
                Lengo la 1:  Tambua njia nne tofauti zinazotumiwa na watu mbalimbali kutafsiri Kitabu cha Ufunuo:
                1. Preterest:           Unabii huu ulitimizwa wakati wa Kanisa la kwanza lilipopitia katika
mateso yaliyoendeshwa na Warumi.  Wengine wanaamini kuwa unabii ulitimizwa mwaka 70 BK wakati Yerusalemu ulipoangamizwa.
2. Historicit:           Nabii hizi zinahusiana na watu na matukio mbalimbali yaliyotokea huko nyuma – km. Napoleon na kuinuka kwa Uislam.
3. Idealist:              Matukio yanaelezea mifano ya kiroho kuhusiana na mapambano kati ya Mungu na shetani.
4. Futurist :            Nabii hizi zinahusiana na matukio halisi yatakayotokea siku zijazo ili kukamilisha mpango wa Mungu.
B.             MAMBO  MUHIMU:
                Lengo la 2: Eleza kanuni za kutafsiri ujumbe wa kitabu cha Ufunuo:
                Kitabu cha Ufunuo ni cha aina ya Apokrifa, hivyo:-
(a)     Kinatumia ishara na mifano kutoa ukweli
(b)     Malaika wanaoelezea matukio
(c)      Kinaonyesha ushindi wa Mungu juu ya shetani.
KANUNI ZA KUTAFSIRI NA MAANA ZAKE:
Kanuni Na. 2- Acha Maandiko yatafsiri yenyewe – Eze. 12:1-16
Kanuni Na. 2 – Tumia mwonekano wa unabii – mf. Lk. 4:16-21; Isa. 61:1,2
Kanuni Na 3 – Tambua kutumia mara mbili kwa andiko la unabii
Kanuni Na. 4 – Elewa matumizi ya ishara na mifano.
Aina za mifano      Mfano                                     Maana:
                Namba                                    moja                                        Mungu
                                                                Mbili                                         Kuhakikishwa
                                                                Tatu                                         Utatu
                                                                Nne                                         Dunia
                                                                Sita                                          Mwanadamu, uovu
                                                                Saba                                        Utimilifu wa Mungu
                                                                Kumi                                        Kukamilika kwa siasa
                                                                Kumi na mbili                           Mwisho wa kukamilisha
Wanyama                               Mwanakondoo                         Yesu
                                                Farasi                                      Uwezo wa Kijeshi
                                                Wanyama                                Mpinga Kristo na nabii wa uongo
                                                Vyura                                       Mapepo wachafu
                                                Silaha                                      Yesu
Rangi                                      Nyeupe                    Utakatifu
                                                Nyekundu                                Damu vitani
                                                Nyeusi                                     Baa la Tauni
                                                Zambarau                               Anasa za Kifalme
                                                Kijani                                        Burudisho
                                                Kijivujivu                   Mauti.
MASWALI:                            
1.Taja maoni manne na maana zake kuhusiana na Uufunuo.
2. Orodhesha kanuni nne za kutafsiri kitabu cha Ufunuo.
                SOMO LA 7:  YALE YOHANA ALIYAONA:
A.             CHANZO NA KUSUDI LA UFUNUO:
                Lengo la 1:  Eleza chanzo cha Kitabu cha Ufunuo na ujumbe wake.
Chanzo cha ujumbe wa kitabu ni Mungu akiwa na lengo la kuifunua kweli kwa watumishi wa Mungu.  Hivyo kitaeleweka kwa watu wake kwa sababu wanayo hekima kutoka kwa Mungu.
B.             EN TACHEI:
                Lengo la 2:  Eleza maana ya neno “upesi”  - Ufu. 1:1
Yesu  alimtuma malaika wake kumwonyesha Yohana mambo ambayo hayana budi kuja upesi – neno upesi linatokana na neno la Kigriki “En Tachei” likiwa na maana “mara moja “   upesi, ghafla, wakati wowote.
C             MAANA YA  “MALAIKA”:
                Lengo la 3:  Eleza njia mbali mbali za Kibiblia kuhusiana na neno “Malaika” na
                                       Ujumbe alioonyeshwa Yohana (Ufu.1:2)
Ufu. 1:1 unaonyesha kuwa neno “malaika” lina maana ya mpeleka habari (tarishi). Hii inaonyesha kuwa Yesu Kristo alifunuliwa kwa Yohana na malaika.  Katika Biblia kuna malaika wa aina mbili:
Wajumbe wa  kimwili na wa Ki-Mungu.  Huyu malaika alitoa ujumbe kwa kutumia ishara na mifano.  Mambo mawili yaliyofunuliwa ni Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo.
D.            HERI SABA ZILIZOMO KATIKA  UFUNUO  (1:3-5)
                Hizi ni baraka za Mungu kwa watu watakaotenda mambo Fulani.
                Lengo la 4 : Orodhesha Heri hizo.
                1.     Ufu. 1:3 - “Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu na kuyashika yaliyoandikwa..”
                2.     Ufu. 14:13 -Heri wafu wafao katika Bwana, tangu sasa wapate kupumzika.
3.     Ufu. 16:15 - Heri akeshaye na kuyatunza mavazi yake asiende uchi..”
4.        Ufu. 19:9 -   Heri walioalikwa karamu ya Arusi ya Mwanakondoo
5.        Ufu.20: 6 -  Heri na Mtakatifu ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa Kwanza
6.        Ufu. 22:7 - Heri yeye ashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.
7.        Ufu. 22:14 – Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa Uzima.
E.             ROHO SABA ZA MUNGU – Ufu. 1:4
                Lengo la 5: Onyesha Roho saba ni nini?
Roho saba za Mungu maana yake ni ukamilifu wa huduma ya Roho Mtakatifu kwa Kanisa la Mungu.
F.             AINA TATU ZA KUJITAMBULISHA KWA YESU – 1:5,6
                Lengo la 6: Eleza jinsi Yesu anavyojitambulisha.
(a)     Yesu ni Shahidi mwaminifu
(b)     Mzaliwa kwa Kwanza wa walio hai
(c)      Mkuu wa Wafalme wa dunia.
G.            ALFA  NA  OMEGA –1:8
                Lengo la 7:  Eleza sababu inayomfanya Yesu aitwe Alfa na Omega.
                Yesu anaitwa Alfa na Omega kwa sababu herufi za Kiyunani zinaelezea kuwa katika yeye Mungu Baba aliumba vitu vyote na katika yeye Baba ataleta mwisho wa kila kitu.
H.            NENO  TAZAMA – 1:7
Lengo la 8: Eleza maana tofauti za neno Tazama, katika kifungu hiki lina maana ya:
(a)     Kuona kwa macho ya kimwili
(b)     Kuelewa au kufahamu
(c)      Kushangaa na kujiuliza.
I.              SIKU  YA  BWANA  - 1:10
                Lengo la 9 : Eleza maana ya siku ya Bwana.         
Katika mstari huu una maana siku ya kwanza ya juma, Jumapili. Yohana alikuwa katika roho siku hiyo.
J.             SAUTI,  AMRI  NA MAONO – 1:10-16
                Lengo la 10:   Elezea Yesu aliyeonwa na Yohana.
                Yohana alimwona Yesu katika Utukufu wake.
a.        Vazi lililofika miguuni                - Ukuu wa Yesu kama nabii, kuhani na mfalme.     
b.         Kichwa na nywele zake          - Utakatifu,, hekima na Umilele wa Yesu
c.        Macho kama mwali wa moto- Anajua yote
d.        Miguu kama  shaba iliyosuguliwa             - Hukumu ya Yesu kwa watu
e.        Sauti ya majimaji                      - Mamlaka na nguvu za Yesu
f.         Mkono wake wa kuume           - Kujali, msaada na kudhibiti kwa Yesu
g.        Upanga utokao kinywani         - Neno lenye mamlaka ya Yesu
h.        Uso kama jua katika nguvu zake – Utukufu , Ukuu na Utakatifu wake.
K.             MAUTI NA KUZIMU  -  1:17,18
                Lengo la 11  : Eleza neno “Paradiso”, jadili mahali ilipo.
               
Kufuatana na Maandiko, Paradiso ni mahali pa kuwafariji watakatifu waliokufa.  Wakati wa Agano la Kale paliitwa kifuani pa Ibrahimu huko kuzimu.  Yesu alipokufa na kufufuka Paradiso ilihamishwa mbinguni.  Hivyo kuzimu ni mahali wanapokwenda waovu wanaokufa.    

NYOTA  NA  VINARA VYA TAA  - Ufu. 1:19,20

Lengo la 12:  Elezea maana ya nyota na Vinara.
                Nyota saba ni malaika saba ikiwa na maana ya wachungaji wa Makanisa. Vinara saba ni makanisa saba (Mst.20) ambayo yamewekwa kuwa nuru ya kumfunua Yesu Kristo kwa watu.  Yesu yupo katikati ya vinara kuonyesha uwepo wa Mungu upo ndani ya kanisa na wachungaji wapo mikononi mwake.
MASWALI:
  1. Neno “ Malaika” lina maana gani katika Ufunuo.
  2. Orodhesha heri zilizomo katika Ufunuo
  3. Siku ya Bwana inayotajwa Ufu.1:10 ni ipi?
  4. Nini maana ya Alfa na Omega – Ufu.1:8
SOMO  LA  8:  NYARAKA KWA EFESO, SMIRNA NA PERGAMO:
Lengo la 1: Orodhesha mambo yaliyomo katika barua zilizoandikwa kwa.
                              Makanisa Saba:
a.        Salamu kwa Kiongozi wa kila Kanisa.
b.        Tabia na hali za Yesu Kristo.
c.        Yale Yesu anayajua kwa kila Kanisa
d.        Yale anayoyafurahia katika kila Kanisa isipokuwa Laodekia
e.        Yale Yesu aliyakosoa na kukemea katika kila Kanisa isipokuwa Smirna na Filedefia.
f.         Ahadi kwa kila Kanisa
g.        Ushauri kwa kila Kanisa kusikia ujumbe
h.        Ahadi kwa washindi
N.B:  Jumbe kwa Makanisa saba inaelezea hali ya Kiroho iliyokuwemo ndani
            Ya Makanisa hayo.  Hali hiyo inalingana na Makanisa ya vizazi vyote.
(i)                   BARUA KWA KANISA LA EFESO:
Lengo la 2:  Eleza Historia na hali ya Kanisa la Efeso.
        Efeso ulikuwa mji na bandari wenye ibada za sanamu uliozungukwa na mashamba mazuri.
(a)     Kanisa lilianzishwa na Paulo katika safari ya tatu ya Utume. Watu wengi waliokolewa na kuchoma uchawi wao (Mdo.19:1-41).  Paulo alifanya kazi Efeso kwa muda wa miaka 3 (Mdo. 20:31)
(b)     Baadaye Kanisa hili alilisimamia Timotheo ili kukemea mafundisho potofu yaliyoletwa na baadhi ya waamini (1Tim. 1:3)
(c)      Kanisa lilisifiwa na Yesu kuwa mambo matano mazuri:-
BIDII,UVUMILIVU,KUTOVUMILIA UOVU, KUWAJARIBU WATIITAO MITUME, KUCHUKIA MAFUNDISHO YA WANIKOLAO.
(d)     Lilikemea kwa kupoteza upendo wa kwanza; hivyo lilikuwa katika hatari ya kutengwa.
Fundisho:    Uhusiano wetu na Yesu uwe wa kwanza kuliko vitu vyote, mfano
 Mke, watoto, kazi, nk.
(ii)                 BARUA KWA KANISA LA SMIRNA –2:8-11
Lengo la 3:  Eleza hali na mistari ya Kanisa la Smirna.
(a)     Mju wa Smirna ulichukua jina kutokana na manukato yaitwayo Myrrh . Ulikuwa mji tajiri katika Asia ya Kati
(b)     Ulikuwa na Wayahudi wenye nguvu na wapinzani wa Injili.
(c)      Kanisa lilikuwa na watu maskini na wenye kupitia mateso.  Wayahudi walikuwa wanawatukana Wakristo.
(d)     Yesu anaonya kuwa baadhi yao watatupwa gerezani wawe waaminifu mpaka kufa.
Fundisho:  Yesu Kristo anajua majaribu tunayopitia, anataka tuwe
                     waaminifu  na atatupa taji ya uzima.
(iii)                BARUA KWA KANISA LA PERGAMO – 2:12-17
Lengo la 4: Eleza hali na Historia ya Kanisa.
(a)     Mji wa Pergamo ulikuwa makao makuu ya kisiasa na dini katika Asia ya Kati.  Ndipo palikuwa pa kwanza kuanzisha kumwabudu Kaisari (kiti cha enzi cha shetani).
(b)     Yesu anajitambulisha kwa kuwa na upanga mkali maana yake anakosoa mafundisho potofu.
(c)      Kanisa linasifiwa kwa uaminifu na kushikilia Imani.
(d)     Yesu analikosoa kwa kuwavumilia watu wenye Imani potofu.
(Mafundisho ya Ballam – ibada ya sanamu na uzinzi- mafundisho ya Wanikolao).
                                Fundisho:  Lazima waamini wasipinge imani potofu na mafundisho potofu.
(iv)                BARUA KWA KANISA LA THIATIRA –2:18-29
Lengo la 5:  Eleza hali na Historia ya Kanisa:
(a)     Kanisa lilikuwa katika mji wa viwanda vya nguo vya zambarau. Lydia alitokea hapa.
(b)     Yesu alilisifu Kanisa kwa mambo manne – (UPENDO, IMANI, HUDUMA, SUBIRA)
(c)      Yesu analikosoa Kanisa kwa kumridhia Mwanamke nabii wa uongo mwenye tabia za Yezebeli.
Fundisho:  Yesu anachukua Kanisa likifumbia macho walimu wa uongo
                     Yesu anaahidi kuwashughulikia wote wafundishao uongo.
(v)                 BARUA KWA KANISA LA SARDI  - 3:1-6
Lengo la 6:  Elezea Historia na hali ya Kanisa:
(a)     Mji wa Sardi ulikuwa juu ya mlima katika njia kuu ya biashara.  Ulikuwa na ngome imara ya kijeshi na tajiri, uliojengwa na Kaisari Tiberia.
(b)     Yesu anajitambulisha kuwa anazo hizo Roho saba, kuonyesha kuwa anafahamu matendo ndani ya Kanisa. Watumishi wanawajibika kwake.
(c)      Kanisa linakemewa kwa kuonekana kwa jina  liko hai , lakini ukweli limekufa.
(d)     Baadhi ya waamini walikuwa safi.
Fundisho:  Kanisa linatakiwa kuwa hai Kiroho.
(vi)                BARUA KWA KANISA LA FILEDEFIA – 3:7-13
 Lengo la 7: Eleza Historia na hali ya Kanisa
(a)     Kanisa lilikuwa katika mji uliojengwa na mfalme Pergamo. Ulichukua jina la mjenzi Akalus Phidadefia.
(b)     Mji ulikuwa unakabiliwa na matetemeko na makao ya ibada ya kipagani. Uliitwa Athens ndogo.
(c)      Yesu analisifia Kanisa kwa mambo matatu.
·         Linazo nguvu kidogo
·         Limetunza Neno lake
·         Halikujulikana jina la Yesu.
(d)     Yesu analiahidi mambo manne:
·         Atawafanya kuwa nguzo katika Hekalu la Mungu
·         Ataandika jina jipya la Mungu juu yao
·         Ataandika juu yao jina la mji wa Mungu
·         Ataandika juu yao jina lake jipya.
(vii)              BARUA KWA KANISA LA LAODEKIA – 3:14-22
Lengo la 8: Eleza historia na  hali ya Kanisa.
(a)     Kanisa lilikuwa katika mji tajiri kwa viwanda, nguo na maziwa, madawa na mabenki.
(b)     Mji huu uliopewa jina la malkia Laodekia ulikuwa na bomba la maji vuguvugu.
(c)      Kanisa halina sifa njema Yesu analikemea kwa tabia ya uvuguvugu iliyo  nayo na kulishauri kutubu.
Fundisho:  Yesu hapendi mtu vuguvugu anataka mtu aamue kumfuata  
                      yeye au  hapana.
               
                HALI TATU ZA KIROHO:
1.        Hali ya moto  -  Mwamini mwaminifu aliyejitoa kikamilifu kwa Bwana. Ameokolewa na anamfuata Yesu Kristo.
2.        Hali ya uvuguvugu –Ni mtu aliyeokolewa lakini hajafikia kiwango cha Kristo na Injili yake.Anashika baadhi ya mambo ya Mungu.
                3.     Hali ya Ubaridi - Mtu anaishi kama ulimwengu hana hamu ya mambo ya   kiroho na Mungu.
MASWALI:
  1. Orodhesha sifa zilizotolewa na Yesu kwa kila Kanisa.
  2. Orodhesha udhaifu unaotolewa kwa kila Kanisa.
SEHEMU YA 3: MAENDELEO YA MATUKIO KATIKA SIKU YA MWISHO:
SOMO LA 9: KANISA  NA  DHIKI KUU:
A.             MAANA YA USEMI “BAADA YA HAYO” – 4:1.
                Lengo la 1: Eleza maana ya usemi huu:
Usemi huu unatokana na neno la Kigriki “Meta tauta” likiwa na maana ya yale yatakayotokea baada ya kipindi cha Kanisa.
B.             MLANGO UKAFUNGUKA MBINGUNI – 4:2
Lengo la 2: Eleza juu ya maoni ya kuwa tendo la Yohana kuchukuliwa toka duniani  kupitia mlango uliofunguliwa kwenda mbinguni kunahusiana na unyakuo wa Kanisa.
1.        Yesu alisikia sauti ya Yesu Kristo, Yohana anaambiwa “panda hata huku” mara moja.  Mambo yanabadilika mbinguni.
2.        Kunyakuliwa kwa Yohana 4:1-2 kunaonekana kuwakilisha kunyakuliwa Kanisa kabla ya dhiki Kuu.  Hii inadhihirisha ya kuwa Kanisa litaondolewa kabla ya dhiki kuu.
3.        Pia neno Kanisa halitumiki baada ya sura ya 3 hadi 22.
C.            UPEKEE  WA  DHIKI  KUU:
                Lengo la 3: Eleza kwa nini dhiki kuu ni jambo la pekee katika historia ya Binadamu duniani.
Dhiki kuu ni tukio la pekee katika historia katika dunia , kwa sababu ni dhiki pekee ambayo inaitwa siku kubwa ya hasira ya Mungu.
D.            UNYAKUO  WA  KANISA –(1Thess. 4:11-13)
Lengo la 4: Eleza mambo yatakayotokea wakati wa kunyakuliwa Kanisa.
Tunaamini Kanisa litanyakuliwa kabla ya dhiki kuu , kwa sababu hatusomi neno lolote “Kanisa” kutoka Ufu. 4:1-22.  Hivyo Kanisa halitapitia katika dhiki kuu (1Thes. 5:9).  Mambo mawili yatatokea wakati Yesu anakuja kwa mwaliko mkuu kutoka mbinguni- Baragumu Italia:
(a)     Kwanza, wafu waliolala katika Kristo watafufuliwa.
(b)     Pili, walio hai watabadilishwa na kunyakuliwa pamoja na wafu waliofufuliwa kumlaki Bwana hewani.
N.B: Yesu ataleta roho za waliokuwa katika Bwana pamoja naye ili kuungana na Miili iliyofufuliwa.
E.             MANENO YANAYOTUMIWA KATIKA KUJA KWA YESU:
                Lengo la 5: Eleza maana ya maneno ya Kigriki  yanayotumiwa, maneno ni:
(a)     HARPADZO   - Kunyakua kwa nguvu           
(b)     EPIPHANELA - Mg’ao
(c)      PAROUSIA     - Kuja mwenyewe.
F.             MAJADILIANO YA MWASWALI MATATU KUHUSIANA NA SIKU ZA MWISHO (Mt. 24:3)
(a)     Mathayo haelezi jinsi Yesu alivyojibu maswali, bali Luka anaelezea majibu.  Siku za mwisho zitaambatana na usaliti, wakristo wa uongo, chuki na mateso kwa waamini.  Pamoja na kurudi nyuma kwa watu, Injili itahubiriwa duniani pote.
(b)     Yesu alielezea matukio ambayo yangetokea mara moja na yale yangetokea baada ya muda mrefu katika taifa la Wayahudi hasa kuangamizwa kwa hekalu na mji wa Yerusalemu.  Alieleza.
(c)      Anaelezea na dalili zitakazoonyesha kuja kwake.
Mt. 24:2-14 – Yesu anaelezea mambo yatakayotokea kabla ya Kanisa kunyakuliwa:-
1.        Manabii na wakristo wa uongo watakaowadanganya watu wengi.
2.        Kuongezeka kwa vita, njaa na matetemeko yatakuwa mwanzo wa utungu.
3.        Mateso yataongezeka zaidi kwa waamini na wengi wao wataacha imani.
4.        Vurugu, uhalifu na kuasi sheria za Mungu kutaongezeka.
5.        Injili ya Kristo itahubiriwa duniani pote.
Mt. 24:42-44  - Hakuna ajuaye saa ya Yesu kuja kunyakua Kanisa. Siku itakuja ghafla kwa waamini na wasioamini.
Mt. 24:15-28  - Yesu anaelezea matukio yatakayotokea wakati wa kipindi cha dhiki ambayo waliookoka wakati huo watayaona       kabla ya Yesu kurudi mara ya pili.
1.        Chukizo la uharibifu lililonenwa na nabii Danieli
2.        Kutokea kwa manabii na wakristo wa uongo watakaowadanganya hata wateule.
3.        Taabu na dhiki kubwa
4.        Jua na Mwezi kutiwa giza na nyota kuanguka.
5.        Yesu atarudi mara ya pili.
Mt. 25:1-13 – Mfano wa Wanawali Kumi:
      Huu mfano unaonyesha unyakuo utawajia ghafla waamini waaminifu na wasio waaminifu.  Yesu anatuasa kuwa hatangojea kanisa lote lijiandae.  Hivyo kila mwamini anatakiwa kujiandaa kwa kuishi maisha matakatifu na kuwa na Uwepo wa Roho Mtakatifu.
Mt. 25:14-30  - Mfano  wa  Talanta:
     Hapa Yesu anatueleza kanuni muhimu zitakazoamua nafasi ya mwamini katika ufalme wa mbinguni.  Nafasi na thawabu zitategemea jinsi ulivyojitoa kwa Bwana na Ufalme wake.
Mt. 25:31-46 – Hukumu ya Kondoo na Mbuzi:
                     Kondoo -ni watu waliookoka na wako hai wakati wa dhiki kuu.
                     Mbuzi – ni watu waovu waliosalia wakati wa dhiki kuu.
                Hukumu inahusiana na :-
1.        Kutenganishwa kwa watu waliookolewa na watu waovu.
2.        Na matendo ya upendo na huruma kwa wale walioteseka kwa ajili ya Yesu.
3.        Waovu watatupwa katika ziwa la moto na wenye haki watakuwa raia katika ufalme wa Mungu.
ANAYEZUIA NA MPINGA KRISTO:
Lengo la 6: Mtambue anayezuia uovu na mpinga Kristo:
(a)     Walimu wa uongo wamekuwa wanawaambia Wathesalonike kuwa siku ya Bwana imekwisha pita.  Hivyo waliamini kuwa wameachwa.
(b)     Mambo mawili ambayo lazima yatokee kabla ya dhiki kuu:
(i)                   Uasi mkuu utatokea
(ii)                  Mpinga Kristo atatokea.
(c)      Roho Mtakatifu akitenda kazi kupitia Kanisa ndiye anazuia uasi na Mpinga Kristo.
(d)     Mwovu atakuja katika mamlaka kwa njia ya udanganyifu na kufanya miujiza.  Hivyo watu wengi watampokea kwa sababu ya kukataa kweli.
(e)     Jinsi tunavyoendelea mwisho wa nyakati uasi na uovu unaongezeka.  Utafikia kilele wakati wa mpinga Kristo.

MASWALI:-

1. Kunyakuliwa kwa Yohana kwenda mbinguni kunawakilisha nini?
2. Taja mambo mawili yatakayotokea wakati wa kunyakuliwa kwa Kanisa.
3. Katika waraka wa Wathesalonike Paulo anasema yupo azuiaye kutokea kwa mpinga
    Kristo. Huyo ni nani?
4. Ni mambo gani Yesu anaelezea katika sura zifuatazo:-
(a)     Mt. 24:4-14
(b)     Mt. 24:42-44
(c)      Mt. 24:15-28
SOMO LA 10(a):  MWANZO WA JUMA LA SABINI:
A.             MWENYE KITI CHA ENZI MBINGUNI – 4:3
                Lengo la 1 : Mtambue mwenye kiti cha Enzi mbinguni.
Mwenye  Kiti cha Enzi mbinguni ni Mungu mwenyezi. Anayeishi katika utukufu akiwa amezungukwa na viumbe vinavyomwabuudu.  Upinde wa mvua ulikizunguka Kiti unaonyesha Ahadi za Mungu.
B.             MAELEZO KUHUSIANA NA WAZEE ISHIRINI NA NNE  - Ufu. 4:4
                Lengo la 2: Elezea na kuwatambua wazee Ishirini na Nne (Ufu. 4:4)
Wazee wamevaa mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani mwao wanaonyesha ni watu waliokombolewa kwa sababu:-
(a)     Mavazi meupe ni kwa ajili ya watu waliokombolewa.
(b)     Taji za dhahabu wanapewa waliokombolewa baada ya kumshinda shetani-3:3
(c)      Kufuatana na Ufu.21:12-14 – ukuta wa Yerusalemu una milango 12 yenye majina ya makabila 12 ya Israeli na misingi 12 yenye majina ya mitume 12.
(d)     Hakuna katika Biblia ambapo malaika hutajwa kama wazee.
(e)     Kutokana na Ebr. 11:39,40 na Ufu. 21:12-14 inaonekana wazee hao huwakilisha watakatifu wa Agano la Kale na A/Jipya.
C.            VITAMBUE VIUMBE HAI WANNE – 4:6-11
                Lengo la 3: Eleza viumbe.
Viumbe hai wane vipo kwa ajili ya kusifu Mungu mwenyezi.  Inawezekana viumbe hivi vinawakilisha viumbe wote.  Viumbe vyote vitaleta utukufu na heshima mbinguni wakati vitakapokombolewa kutoka katika laana.
D.            KITABU KILICHOTIWA MHURI  - Ufu. 5:1.
                Lengo la 4: Eleza maana ya kitabu hiki.
Kitabu hiki kina umuhimu sana kwa sbabu kina ufunuo wa Mungu kuhusiana na mambo yatakayokabili dunia na mwanadamu katika siku zijazo.  Kinaelezea jinsi watu watakavyohukumiwa, ushindi wa Mungu juu ya Mungu na watu wake juu ya uovu.  Kila muhuri unapovunjwa jambo hutokea.
E.             YESU KRISTO MWANAKODOO ANAYESIFIWA – 5:6-14
                Lengo la 5: Eleza maana ya Mwanakondoo aliyechinjwa.
(a)     Kristo anaonekana kuwa ni Mwanakodnoo aliyechinjwa.  Hii inaonyesha kujitoa kwake pale msalabani (Kalvari) kwa ajili ya dhambi za watu.  Ni kitambulisho cha kustahili, nguvu, mamlaka na ushindi wa Yesu juu ya msalaba.
(b)     Pembe saba zinaonyesha nguvu na uwezo wa mtawala.
F.             KUFUNGULIWA KWA MIHURI SITA – 6:1-17.
                Lengo la 6: Taja vitu vinavyotokea baada ya kufungua mihuri sita.
Watu wengi wasioamini kuwa Kanisa litapitia katika dhiki kuu wanaamini kuwa kufunguliwa kwa mihuri ni mwanzo wa dhiki kuu.
(a)Mhuri wa Kwanza- Mpanda farasi mweupe mwenye uta kinywani ni Mpinga Kristo.
                (b)    Mhuri wa Pili   - Farasi mwekundu anawakilisha vita na vifo vya kutisha.
(c)      Mhuri wa Tatu - Farasi mweusi unaonyesha njaa na ukame wa kutisha.     
(d)     Mhuri wa Nne  - Farasi wa kijivu akiwakilisha vita, njaa,tauni na hayawani
(e)     Mhuri wa Tano - Watakatifu waliouawa wakiwa mbele ya Kiti cha Enzi.
(f)       Mhuri wa Sita  - Tetemeko kubwa linalotikisa ulimwengu mzima.
MASWALI:                           
1. Je, Wazee Ishirina na nne ni akina nani?
2. Taja matukio yanayotokea kila muhuri unapofunguliwa. (Ufu. 6:1-17)
SOMO LA 10 (b): MATUKIO KATIKATI YA DHIKI KUU NA KUENDELEA:
                Lengo la 1: Eleza matukio – dhiki kuu hadi mbingu mpya.
(a)     Kufungua mihuri saba na Baragumu saba miaka 3 na nusu ya kwanza.
(b)     Vitasa saba katikka miaka 3 na nusu ya mwisho
(c)      Ufufuo wa Watakatifu
(d)     Utawala wa miaka 1,000
(e)     Hukumu ya mbele ya Kiti Cheupe.
(f)       Mbingu mpya na nchi mpya.
B.             MALAIKA WANNE NA MALAIKA ANAYETIA MUHURI – 7:1-3
                Lengo la 2: Eleza sababu za kutiwa muhuri wa 144,000.
Malaika wane wanazuia upepo , na kuidhuru nchi.  Malaika mwingine anatokea kwa ajili ya kuwatia muhuri watumishi wa Mungu.  Lengo la kutiwa muhuri 144,000 ni kuwapa ulinzi wakati wa hukumu inapotolewa majeshi ya pepo waovu yasiwadhuru.
C.            WATU 144,000  - 7:4.
                Lengo la 3: Eleza ni akina nani 144,000 kutoka makabila kumi na mbili.
                Hawa ni Wayahudi watakaomwamini Kristo wakati dhiki kuu kutoka kabila 12 za Israeli.  Muhuri vipajini pao ni kuonyesha kuwa ni mali ya Mungu na watalindwa na Mungu kutokana nahukumu yake.
D.            144,000 –WATAMBULIWA – 7:5-8.
                                Lengo la 4: Eleza sababu zinazofanya makabila mengine yameondolewa:
Majina ya Danieli na Efraimu hayamo katika orodha ya makabila ya Israeli.  Hii inawezekana kwa sababu makabila haya yaliongoza taifa katika ibada za sanamu na uasi.
E.             MKUTANO MKUBWA WA WALIOVAA MAVAZI MEUPE  - 7:9-17.
                Lengo la 5:  Eleza umuhimu wa watu hawa waliovaa nguo nyeupe (Ufu.7)
Hawa ni watu walioamini wakati wa dhiki kuu. Wametoka katika kabila duniani.  Watanyakuliwa mwishoni mwa dhiki kuu na kuhudhuria karamu ya Mwanakondoo.  Ukweli huu unaonyesha watu wataokolewa wakati wa dhiki kuu.
Wazee 24
Mkutano Mkubwa
Wameketi Vitini
Wamesimama mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu
Wana Taji
Hawana Taji
Wana vinubi na vyelezo
Wameshika matawi ya mitende.
F.             MALAIKA ALIYE NA  CHETEZO CHA DHAHABU – 8:3,4
                Lengo la 6 : Eleza ni nani malaika mwenye chetezo.
Muhuri wa Saba unafunguliwa kunakuwa na ukimya.  Hapa haijulikani maana y    ake.  Malaika aliye na chetezo ni Yesu Kristo kwa sababu katika A/Kale , makuhani peke yao walifunikiza uvumba kuwaombea watu.  Katika A/Jipya Yesu Kristo ndiye kuhani mkuu, mpatanishi kati ya Mungu na watu.
G.            TARUMBETA  SITA  - 8:6-9:21
Lengo la 7: Eleza ni matukio gani yatakayotokea wakati wa kupigwa tarumbeta  Sita.
Tarumbeta  ya 1 – Theluthi 1ya mimea ya nchi itateketea
Tarumbeta ya 2   Theluthi1 ya bahari kuwa damu na viumbe na meli  Kuangamizwa
Tarumbeta ya 3 – Theluthi 1 ya mito na chemchemi zitatafurika na watu wengi kufa.
Tarumbeta ya 4 – Theluthi 1 ya jua ikapigwa, na 1 ya Mwezi na 1 ya nyota ili Theluthi itiwe giza.
Tarumbea ya 5 – Majeshi ya pepo waovu kutesa watu wasio na mhuri wa Mungu kwa miezi   mitano.
Tarumbeta ya 6 – Mateka 4 walifunguliwa na kuwa theluthi 1 ya watu.
Tarumbeta ya 7 -  Sauti kutoka mbinguni kuwa ufalme ni wa Mungu.
N.B:  Licha ya mateso yote haya watu wanakataa kutubu.
MASWALI:
  1. Taja matukio yanayotokea wakati wa baragumu saba.
  2. Je, 144,000 waliotajwa hapa ni akina nani?
  3. Kuna tofauti gani kati ya wazee 24 na mkutano mkubwa?
SOMO LA 11:  MAENDELEO YA UNABII.
A.             MALAIKA MWENYE NGUVU – 10:1-7
                Lengo la 1  : Eleza ushahidi unaoweza kukusaidia kujua huyu malaika ni nani.
Ushahidi unatuonyesha kuwa huyu malaika mwenye nguvu ni Yesu ni huu ufuatao:-
(a)     Mwonekano wake ni  sawa na Yesu wa Ufunuo -  1:13-15
(b)     Kiapo chake anachoapa.Hakuna katika Biblia malaika aliyeapa.
(c)      Sauti yake kama simba aungurumapo.Biblia ( Yoel. 3:16) inasema Bwana anaunguruma kama simba( Hosea 11:10,11;Amosi 3:8) Usemi wa malaika “hapatakuwa na wakati baada ya haya” (Ufu.10:6-7).  Una maana kuwa yale yaliyokusudiwa hukumu juu ya uovu lazima utekelezwe.
B.             YOHANA ATUMWA KUTOA UNABII  - Ufu.10:8-11
Lengo la 2: Eleza maana ya Yohana kula kitabu kidogo.
Kitabu hicho alichokula Yohana kilikuwa na ujumbe uliokuwa unaeleza kukamilisha kusudi la Mungu kwa watu duniani.  Kilielezea mambo yatakayotokea.  Kujua ujumbe kulikuwa kutamu kama asali, bali baadaye kulisababisha uchungu ndani ya moyo wa Yohana.  Hivyo Mungu anamwagiza akahubiri ujumbe huo ili watakaomwamini wapate uzima wa milele na wasioamini wapate kuhukumiwa.
C.            MAELEZO ZAIDI KABLA YA BARAGUMU YA SABA – Ufu.11:1-14
                Lengo la 3:  Eleza maana ya kupimwa kwa hekalu na mahusiano yake ni miezi 42.
1.        Kulipima Hekalu – 11:1,2:
Kupimwa kwa hekalu na madhabahu na kuhesabiwa kwa wanaoabudu kunamaanisha kuwa E_Wayahudi watajenga hekalu lao.  Kutokana na Agano lao na mpinga Kristo watakuwa na uhuru wa kuabudu.  Katikati ya dhiki kuu mpinga Kristo atavunja agano na kulinajisi hekalu.  Kipindi cha miezi 42 ambacho ni miaka 3 na nusu mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa mataifa, mpinga Kristo atawatesa na kuwaua Wayahudi waaminifu.  Mwisho wa miaka 3 na nusu utakamilisha mwisho wa kipindi cha mataifa.
2.        Mashahidi wawili  - 11:3-14
Lengo la 4:  Eleza kusudi la Mashahidi wawili, uwezo wao, matokeo ya ushuhuda wao na ni akina nani.
        Mashahidi wawili watatokea ambao watahubiri Injili kwa uwezo mkubwa huku wakileta hukumu na mapigo kwa wale wanaowapinga.  Watahubiri Injili  kwa muda wa siku 1260.  Baada ya kumaliza ushuhuda watauawa na mpinga Kristo ambaye atakuwa amepona jeraha lake.  Miili yao italazwa mitaani na kushuhudiwa na watu kwa njia ya Televisheni.  Baada ya siku tatu, nusu watafunguliwa na kupaa, matokeo yake kutakuwa na tetemeko kubwa la ardhi litakaloua watu 7000.
        Mashahidi wanadhaniwa na wanatheolojia kuwa ni Henoko na Eliya kwa sababu hawakuonja mauti walitwaliwa mbinguni.
Fundisho:  Mtumishi wa Mungu ataondolewa ikiwa amemaliza kazi.
D.            KUPIGWA KWA BARAGUMU YA SABA -  11:15-19
                Lengo la 5: Eleza mkazo wa baragumu lasaba.
Mkazo wa baragumu ya saba ni tangazo la kuwa falme za ulimwengu zimekuwa ufalme wa Yesu Kristo.  Pia inaonyesha kuwa hukumu inakaribia kumalizika,  “kufunguliwa kwa Hekalu la Mungu mbinguni na sanduku la agano kuonekana hekaluni mwake”, ina maa lengo la agano ambalo ni ahadi ya ufalme linakaribia kutimizwa.  Mungu anatunza ahadi ya neno lake. Matetemeko ni dalili ya kuja kwa mwisho.
E.             MWANAMKE  NA  JOKA.
                MWANAMKE ALIYEVIKWA JUA – 12:1-6,13-16.
Lengo la 6:Eleza na kumtambua huyu mwanamke aliyevikwa jua na elezea na
                      Kukimbia kwake:
Ishara 1:                 Mwanamke huyu ni taifa la Israeli lenye makabila kumi na mbili ambamo Masihi kwake.
Ishara 2:                 Joka lenye vichwa saba na taji maana yake ni shetani katika nguvu zake. Nyoka mbinguni ni malaika waasi aliofukuzwa  nao kutoka mbinguni.  Mtoto aliyenyakuliwa ni Yesu Kristo aliyezaliwa na kufufuliwa na kupaa kwenda mbinguni.  Naye atatawala mataifa.Mwanamke alikimbia maana yake katikati ya dhiki kuu Israeli wanakimbia kutoka Utawala wa mateso ya mpinga Kristo .  Israeli atakimbilia Perza huko katika nchi Ya Yordan, na kuhifadhiwa kwa muda wa miaka 3 na nusu.  Hawa Waisraeli ni Uzao utakaosumbuliwa (Ufu. 12:13-17)
MASWALI:
  1. Ni ushahidi gani unaotuonyesha kuwa huyu malaika ni Yesu Kristo?
(a)     ________________________
(b)     ________________________
(c)      ________________________
  1. Nini matokeo ya ujumbe wa mashahidi wawili (11:3-14)
  2. Baragumu ya saba inaashiria nini?
  3. Taja ishara zilizomo katika Ufu. 12:12.

SEHEMU YA 4: MWISHO WA SIKU ZA MWISHO

                SOMO LA 12: JOKA NA VIBARAKA VYAKE.
                1.JOKA 12:3-4.
                Lengo la 1: Mtambue joka na shughuli zake.
Huyu anajulikana kama shetani, joka la zamani la Ibilisi.  Majina yana maana gani?:-
(a)     Joka la zamani – mdanganyifu – Mwa. 3:1-13
(b)     Ibilisi        - Mjaribu, mwenye hila, mpingaji – Mt. 4:1; Efe. 6:11;
(c)      Shetani                   - mshitaki – 1Pet 5:8; Zek 3:1
                2. VITA MBINGUNI  - Ufu. 12:7-12;  17:7-18
                Lengo la 2: Eleza  vita hivyo mbinguni.
Wakati wa dhiki kuu hakutakuwa na mapambano ya kiroho duniani tu , bali hata mbinguni kutakuwa na vita mbinguni.  Shetani na malaika zake watapigana na Mungu na malaika.  Shetani atatupwa chini na kutoruhusiwa mbinguni. Akiwa na hasira na akijua ana muda mchache  anafanya vita na  Waisraeli waaminifu walioko Israeli wanashindwa na kutetewa na Mungu.  Hivyo anawaudhi  mabaki wa uzao ambao Wayahudi waliotawanyika duniani waliomwamini Yesu Kristo.
A.             MNYAMA ALIYETOKA BAHARINI – 13:1-10
                Lengo la 3:  Elezea asili yake, chanzo cha nguvu za mnyama.
Huyu mnyama ni mtumishi wa shetani, ni mwanadamu aliyetoka katika watu wa dunia.  Baadhi ya wanatheolojia wanasema ni falme saba ambazo zimesumbua taifa la Israeli yaani-Misri, Syria, Babeli, Uajemi, Ugriki na Rumi.  Pembe kumi ni viongozi kumi watakaotawala pamoja na mpinga Kristo kwa muda mfupi.
Atatawala kwa nguvu na mamlaka kwa muda wa miezi 42. atakapofufuka au kupona jeraha lake atataka watu wote wamwabudu.  Atawatesa na kuwaua watakatifu wengi.  Kutokana na uwezo aliopewa shetani atawaunganisha watu kupigana na Mungu.
B.             NABII WA UONGO  - 13:11 -18
                Lengo la 4 :  Elezea kuhusiana na mnyama wa pili.
Huyu mnyama anaonekana kama mwana-kondoo, lakini anasema kama joka.  Hii ina maana atajidai mpole, mwenye upendo na kujali , lakini tabia yake ni ya kishetani.  Huyu ataanzisha kanisa la uongo ambalo litamwabudu mpinga Kristo.  Atafanya miujiza minngi na kuwafanya watu  wamwabudu mpinga Kristo. Watauwawa wale watakaopinga amri hiyo na kuwa waaminifu kwa Yesu Kristo.
C.            NAMBA, JINA NA ALAMA YAKE – 13:16-18
                Lengo la 5:  Jadili alama ya mnyama na umuhimu wake.
                Ili kuwadhibiti wamwabudu mpinga Kristo atatumia silaha ya kiuchumi.  Wote wanaotaka kununua na kuuza wawe na namba au jina la mpinga Kristo pajini pa uso au mkononi.  Hivyo namba hiyo itawafanya watu wamkubali au wampinge mpinga Kristo – wasomi wengi wanahangaika kutafuta jina la mpinga Kristo lakini wanapingana.
D.            KAHABA MKUU  - 17:1-6
                Lengo la 6: Elezea kweli mbili kuhusu kahaba na mambo yake katika siku ya mwisho.
Huyu kahaba anawakilisha dini zote za uongo.  Katika Biblia kahaba ni mtu anayemwasi Mungu na kuabudu miungu mingine.  Hivyo kahaba huyu ataikana Imani na Injili ya Yesu Kristo. Hili ni kanisa la uongo litakalomsaidia Kristo kupata madaraka.  Litashiriki katika kuwatesa watakatifu.  Dini na siasa itatumika kutawala mataifa.  Baadaye mwishoni mpinga kristo atalichukia hili kanisa la uongo.  Hivyo ataiangamiza  tasisi hii.
E.             UNABII WA SIKU ZA MWISHO  - Dan. 9:24
                Mambo sita yatakayokamilishwa katika majuma sabini ni:-
1.        Kumaliza makosa
2.        Kukomesha dhambi
3.        Kusamehe uovu
4.        Kuleta haki ya milele
5.        Kutia muhuri maono na unabii
6.        Kupaka mafuta mahali patakatifu kabisa.
1. MWANAKONDOO NA 144,000 – 14:1-5
                Lengo la 7:  Zitambue kweli kuhusiana na utambulisho na tabia za 144,000:        
Hali ya 144,000 ni wasafi kiroho, wamekombolewa kutoka duniani wameandikwa vipajini mwao jina la Baba na wanamfuata Bwana.Hawa ni watakatifu ambao hawakujinajisi na uchafu wa dhambi na ibada ya mpinga Kristo wala hawajawahi kusema uongo.Hawa ndio watakao uimba wimbo wa Mwanakondoo.Watakuwa wamechaguliwa miongoni mwa watakatifu walionyakuliwa kwenda mbinguni kabla ya dhiki kuu. 
                2. TANGAZO LA MALAIKA WATATU – 14:6-13
Lengo la 8:  Jadili kwa kifupi yaliyomo katika matangazo ya malaika watatu.
(a)     Malaika wa kwanza anawataka watu wote duniani wamche Mungu kwa sababu saa ya hukumu imefika.
(b)     Malaika wa pili, anatangaza kuanguka kwa Babeli – yaani mifumo ya siasa, dini na uchumi ya dunia imefika kikomo.
(c)      Malaika wa tatu, anawaonya watu wanaokubali kupokea chapa watateswa katika ziwa la moto milele.
(d)     Wale watakaokufa katika Bwana watakuwa heri , kwani watapumzika taabu zao (mateso na kwenda kwa Bwana).
3. MAVUNO YA DUNIA  - 14:14-20
                Lengo la 9: Eleza mahusiano ya mavuno na shinikizo la divai.               
Mavuno haya yanahusiana na hukumu.  Mavuno ya zabibu ni dunia na shinikizo la divai linahusiana na ghadhabu ya hukumu ya Mungu, itakayowafikia wakazi wa dunia.  Ni umwagikaji wa damu wa kutisha.
MASWALI:
  1. Nini maana ya majina haya:
(a)     Joka la zamani ________________________
(b)     Ibilisi ________________________________
(c)      Shetani ______________________________
  1. Mpina Kristo atakapotoka atafanya nini?
  2. Nabii wa uongo atamsaidiaje mpinga Kristo?
  3. Kahaba mkuu ni nani?
  4. Namba ya mnyama 666 itatumikaje?
  5. Nini tabia za 144,000 walio pamoja na mwanakondoo? (Uf. 14:1-5)
SOMO LA 13:  MATUKIO YA MWISHO WA DHIKI KUU:
A.             MAANDALIZI YA VITASA SABA.
1.        ISHARA KUU YA TATU –Ufu. 15:1-8
Lengo la 1:  Itambue ishara kuu ya tatu. Eleza umuhimu wake.
        Ishara kuu inayotolewa hapa ni ya malaika wenye vitasa saba ambayo ni mapigo ya mwisho.  Ishara mbili zingine ni: Mwanamke aliyevikwa jua (Ufu.12:1) na Joka kubwa jekundu lenye pembe kumi na vichwa saba (Ufu. 12:3).  Ishara kuu ya tatu ni ya muhimu kwa sababu inahitimisha hasira na hukumu ya Mungu.
2.        KUMWAGWA KWA VITASA VYA GHADHABU YA MUNGU – 16:1-21
Lengo la 2: Eleza vitasa saba vinawakilisha nini na athari juu ya wanadhamu:
Kitasa 1:          Madonda mabaya na ya kuumiza yawapata wanadamu walio na Alama ya mpinga Kristo.
Kitasa 2:          Viumbe hai vyote baharini vinakufa.
Kitasa 3:          Mito na chimchemi za maji zageuka damu
Kitasa 4:          Jua likawaunguza wanadamu
Kitasa 5:          Giza kubwa juu ya utawala wa mpinga Kristo
Kitasa 6:          Vita vya Harmagedonia.
Kitasa 7:          Ngurumo na tetemeko Babeli na miji ya mataifa yaangushwa. Visiwa na milima ikatoweka, mvua ya mawe kubwa ilinyesha.
Matokeo ya mapigo haya watu waliendelea na mioyo migumu na kumtukana Mungu.

KAHABA MKUU – 17:1-18

                Kahaba mkuu ni mji ule mkuu ulio na mamlaka juu ya wafalme wote.  Hii itakuwa ni Kanisa la uongo ambalo litakuwa na nguvu ya ushawishi kwa viongozi mbalimbali duniani, katika miaka 3 na nusu ya mwanzo ya dhiki kuu itamsaidia mpinga Kristo ili kupata madaraka.  Lakini mpinga Kristo atakapopata nguvu na kufufuka au kupona jeraha lake atafanya  hila ya kumwangamiza.  Wakati wa kipindi cha miaka 3 na nusu ya mwisho mpinga Kristo atataka kuabudiwa na wote.  Hili kanisa la uongo litashiriki katika kuwaua watakatifu watakaopingana  naye.
B.            PEMBE KUMI  - 17:10-15
                Lengo la 3:  Elezea juu ya pembe kumi:
Mstari wa 10 unazungumzia wafalme saba, watano wameanguka na mmoja bado.  Watu wanaamini kuwa ni falme za Misri, Ashuru, Babeli, Uajemi na Umedi, Ugriki iliyokuwa bado kuanguka ni Rumi.  Wa saba  unakuja ni jumuiya ya mataifa kumi.  Mpinga Kristo atakuwa ni mfalme wa nane.  Pembe kumi ni mataifa kumi yenye nguvu za kisiasa na watamsaidia mpinga Kristo na kupingana na Yesu Kristo.
C.            KUANGUKA KWA BABELI NA MIFUMO YA KISIASA NA KIUCHUMI:
                HUKUMU  YA  BABELI  - 18:1-24
1.        Mji wa kisiasa na kiuchumu wa Babeli unatafsiriwa na wasomo kuwa unawezekana ni mji halisi ambao ni makao makuu ya mpinga Kristo.  Pia unafikiriwa kuwa ni mfumo wa kisiasa na kiuchumi wa mwanadamu.
2.        Maangamizi ya Babeli yanaonyesha kuanguka mifumo ya kisiasa na kiuchumi iliyotokea katika historia yote ya mwanadamu kama tulivyosoma katika Dan. 2 na 7, lazima mifumo ya falme za dunia hii kubatilishwa na kuondolewa ili ufalme wa Kristo uje.
3.        Mungu ndiye suluhisho la matatizo yote ya kijamii na kiuchumi ambayo yamesababishwa na dhambi ya mwanadamu.
4.        Mifumo ya kidunia na mpinga Kristo wataangamizwa.
D.            KUJA MARA YA PILI KWA YESU:
1.        SHUKRANI KWA AJILI YA HUKUMU JUU YA BABELI.-Ufu. 19:1-5
Lengo la 4:  Wataje wale wanaotoa sifa kwa Mungu mbinguni na kiini cha sifa zao.
(a)     Wale wanaotoa sifa na shukrani ni umati wa watu wengi, wazee ishirini na nne na viumbe hai wane – Mungu anawatia moyo.
(b)     Kiini cha sifa kwa wale wanaomsifu Mungu mbinguni ni>
(i)                   Kuangusha uasi wa shetani na hukumu ya haki ya Mungu
(ii)                  Tabia na asili ya Mungu chanzo cha ukombozi.
(iii)                 Kuanzishwa kwa ufalme wa Mungu katika historia ya mwanadamu.
2.        HARUSI YA MWANA-KONDOO – 19:6-10
Lengoo la 5: Elezea karamu ya harusi ya Mwanakondoo na vazi la Bibi Harusi
        Karamu ya Harusi ya Mwanakondoo inatangazwa katika Maandiko, ila haielezwi kwa undani.
·         Ni wakati wa kuunganika kwa Yesu Kristo na watu wake
·         Itafanyika katika wakati ambao Mungu amefanya
·         Wale tu walioalikwa watahudhuria Harusi hiyo, wale waliookolewa.
·         Mavazi ya Bibi Harusi ni matendo mema ya watakatifu.  Kukaa na kumtii Yesu Kristo.
3.        KUFUNULIWA KWA MASIHI  - 19:11-21
Lengo la 6: Elezea wajibu wa Masihi aliyepanda farasi mweupe.
        Yesu Kristo ni wakala wa ghadhabu ya Mungu na tumaini la waamini.  Yesu anamwaga hukumu juu ya waovu, lakini wakati huo ni chanzo cha faraja na utukufu kwa watu wake wanaoshuhudia utawala wa haki.  Yesu anakuja mara ya pili pamoja na watakatifu wake.  Anakuja akiwa mfalme wa wafalme na Bwana wa Mabwana, Anakuja akiwa jemadari kuanzisha kweli na haki, kuhukumu mataifa na kufanya vita dhidi ya uovu.
·         Kuwatawala kwa fimbo ya chuma – maana yake kuwaangamiza mataifa.
·         Anakanyaga shinikizo la mvinyo – maana yake hukumu ya kutisha.

KARAMU  YA MUNGU  - 19:17-18

Lengo la 7:  Elezea karamu ya Mungu.
                Hii ina mahusiano na vita ya Har-Magedonia, Mungu atawaangamiza watu waovu wengi wakati wa vita hivyo kiasi kwamba watahitajiwa ndege wala nyama wengi ili kusafisha uwanja wa vita.  Hii ni kwa sababu itakuwa vigumu kuzika watu.

HUKUMU YA MPINGA KRISTO NA NABII WA UONGO – 19:19-21

Lengo la 8: Elezea hukumu ya wanyama wawili waovu.
1.        Mpinga Kristo atakusanya majeshi yake ili apigane na Bwana Yesu na majeshi yake.
2.        Majeshi ya mpinga Kristo yatashindwa vibaya, mpinga Kristo na Nabii wa uongo watatekwa na kutupwa ziwa la moto.
3.        Majeshi au watu waliopigana wakiongozwa na mpinga Kristo waliuawa.
MASWALI:
  1. Taja matukio yanayotokea wakati wa vitasa saba
  2. Kuanguka kwa Babeli kuna maanisha nini?
  3. Nani watakuwepo katika karamu ya Harusi ya Mwana kondoo?
  4. Nini hatma ya mwisho ya mpinga Kristo na nabii wa uongo?
SOMO LA 14:  UFALME WA KRISTO WA MIAKA ELFU NA ULIMWENGU UJAO:
A.             MIAKA ELFU:
1.        KUFUNGWA KWA SHETANI – 20:1-3
Lengo la 1:  Orodhesha mojawapo ya hali ya kiroho itakayokuwepo wakati
                           Wa miaka elfu. Kwa nini kutakuwa na mafanikio?
Mojawapo ya hali ya kiroho ambayo itakuwepo wakati wa utawala wa miaka elfu ni ya kutokuwepo kwa udanganyifu hapa duniani.  Hii ni kutokana na kufungwa kwa shetani huko kuzimu kwa kipindi chote cha miaka elfu.
2.        UFUFUO WA  KWANZA – 20:4-6
Lengo la 2:  Taja watakaohusika katika ufufuo wa kwanza.
        Kwanza kuna watakatifu watakaofufuliwa kabla ya dhiki kuu.  Pili ni kundi la waamini watakaofufuliwa baada ya dhiki kuu ili kutawala pamoja na Kristo.  Hawa ndio walioteswa na kuuawa wakati wa dhiki kuu.   Watashiriki katika kutawala pamoja na Kristo.
3.        MAONI MBALI MBALI KUHUSIANA NA MILLENIA:
Lengo la 3: Eleza maana ya Millenia na kueleza maoni mbali mbali.
        Neno Millenia linatokana na lugha ya Kilatini likiwa na maana ya miaka 1,000. Sasa kuna maoni mbali mbali kuhusiana na millennia , nayo ni:-
(a)      Post Millenialism - Yesu atakuja wakati ulimwengu umejiandaa Kumpokea
(b)    Amillenialism       -  Hakutakuwa ufalme wa miaka elfu wakati wa kurudi kwa  Yesu mara ya pili.
(c)  Premillenialism - Ulimwengu utakabiliwa na utawala wa Masihi- Yesu wa kipindi cha miaka elfu wakati Yesu atakaporudi  mara ya pili (Ufu.20) unasema kurudi kwa Yesu  mara ya pili kutafuatiwa na kufungwa kwa shetani  kuzimu na ufufuo wa wenye haki ambao watatawala pamoja na Kristo kwa muda wa miaka elfu.
4.             HALI KATIKA UTAWALA WA MIAKA ELFU:
                                Lengo la 4: Eleza hali na maisha yatakayokuwepo wakati wa millennia.
                                Mambo haya yatakuwepo katika kipindi hiki:-
(a)      Amani duniani pote hapatakuwepo na vita wala jujifunza vita (Zab. 46:9; Isa. 2:4; 9:6-7; Mika 4:3-4)
(b)      Maendeleo makubwa ya kiuchumi – (Isa. 65:21-24; Amo.9:13-15; Mika 4:4-5)
(c)      Haki itatawala (Isa. 11:13-15; Yer. 23:5)
(d)      Watu wote watamjua Bwana (Isa.11:9; Habak.2:14; Zek.8:21-23)
(e)      Wanyama waondolewa ukali, watakula majani (Isa. 11:6-9; 65:25)
(f)       Nchi itarudishwa hali yake ya kwanza na kuzaa sana (Isa. 35:1,2; Amo. 9:13-15; Eze.36:8-12)
(g)      Maisha marefu (Isa.65:20-22)
(h)      Mabadiliko ya dunia ya kupokea mwanga wa jua na Mwezi (Isa.30:26)
Lengo la 5:  Taja wakazi wa ufalme wa miaka elfu.
Kutakuwa na aina mbili ya watu: Kwanza watakatifu waliokuja na Yesu ambao watatawala pamoja na Kristo.  Pili, ni watu wenye miili hii ya kawaida ambao walikuwa waaminifu wakati wa dhiki kuu na wale watakaozaliwa wakati wa miaka elfu . (Mt. 25).
B.             BAADA YA MIAKA ELFU.
1.        UASI WA MWISHO WA SHETANI -  Ufu. 20:7-10
Lengo la 6:  Eleza sababu za shetani kufunguliwa na matokeo yake.
        Shetani atafunguliwa kutoka gerezani baada ya miaka elfu ili awajaribu watu waliozaliwa wakati wa millennia.  Hii itawkuwa nafasi yao ya kuchagua kumtii mungu au shetani.  Watu wengi watamfuata shetani na kuizingira kambi ya watakatifu.  Kabla ya kuishambulia kambi,  moto utashuka kutoka mbinguni na kuwangamiza. Shetani atatupwa katika ziwa la moto.

HUKUMU YA MWISHO MBELE YA KITI CHEUPE-  20:11-15

Lengo la 7:  Eleza kweli kuhusiana na hukumu ya mwisho.
Katika wakati huu watu wote waovu watafufuliwa na kusimama mbele ya kiti cheupe ili kuhukumiwa.
(a)     Mtu asiyeandikwa jina katika kitabu cha Uzima atahukumiwa.
(b)     Wote waliomkataa Yesu na wokovu wake watatupa katika ziwa la moto wa milele
(c)      Mauti na kuzimu zilitupwa katika ziwa la moto.
Jehanam ni moto mkali usiozimika kamwe, tanuru la moto ambako watu watasaga meno na kuomboleza.  Pia hii ndio mauti ya pili (Mt. 22:13; 25:30; 13:42,50; Mk. 9:43)
C.            MPANGO MPYA  - Ufu. 21-22
1.        MBINGU MPYA NA NCHI MPYA – Ufu. 21.
Lengo la 8: Eleza maana hasa ya mbingu mpya na nchi mpya.
        Kulingana na somo hili ina maana ya kuwa mbingu na nchi ya sasa zitaondolewa.  Baada ya kuja mbingu mpya na nchi mpya (Isa. 51:6; 2Pet.3:7,10-12).  Nchi ya sasa inaondolewa kwa sababu imechakazwa na kunajisiwa na dhambi.  Nchi mpya haina bahari.
2.        YERUSALEMU MPYA – 21:2-22:5
Lengo la 9: Eleza jinsi mji ulivyo:
(a)     Mji huu unaitwa ni Bibi Harusi kwa sababu Mungu atakaa pamoja na watu wake.
(b)     Mji una milango 12 ambayo inawakilisha taifa la Israeli.  Pia una misingi 12 ambayo inawakilisha kanisa.  Hii ni kuonyesha umoja wa watakatifu wa A/Kale na A/Jipya.
(c)      Mji ni mraba wenye mapana, marefu na wimo sawa wa maili 1,500.  Ukionyesha kuwa utakuwa na makao ya kutosha ya watakatifu wote wa vizazi vyote.  Pia mji unajawa na utukufu na utakatifu wa Mungu.
(d)     Mji hauna hekalu kwa sababu Mungu na Mwanakondoo ndio hekalu lake.
(e)     Hakuna usiku katika mji huo
(f)       Barabara zake ni za dhahabu.
(g)     Kulingana na Wanatheolojia, mji huu utakaliwa na watakatifu wote kabla ya dhiki kuu.- yaani walionyakuliwa kabla ya dhiki kuu na wale watakaofufuliwa baada ya dhiki kuu.
(h)     Nchi mpya itakaliwa na watu wote ambao waliishi katika ufalme wa miaka elfu na walimkataa ibilisi na ushawishi wote. Inasemekana watakuwa mataifa wanaongozwa na wafalme.  Wafalme hao wataenda Yerusalemu kumtukuza Mungu kwa yale anayofanya katika nchi mpya (Ufu. 21:24-26)
(i)       Wakazi wa mji wa Yerusalemu ni washindi waliovumilia taabu na adha mbali mbali
(j)       Hawa hawataingia katika nchi hiyo:
§  Waoga ambao wanaogopa kumkiri na kumfuata Yesu Kristo Aliye hai (Mk. 8:35; 1Thess. 2:4)
§  Wasioamini – hawa ni pamoja na wakristo ambao wameanguka dhambini.
§  Waamini wote wanaosema wanamfuata Yesu, lakini wanaishi katika dhambi (1Kor. 6:9,10; Efe. 5:5-7; Gal. 5:19-21)
§  Hawa wote watatupwa katika ziwa la moto
(k)      Watakatifu watamwona uso  wake – hili ndilo lengo la historia ya ukombozi.  Watamwona Yesu Mwanakondoo kwani wataishi naye. (Mt. 5:8; 1Yh. 3:2)
(l)       Mti wa Uzima ambao ni halisi unaonyesha mfano wa Roho Mtakatifu na Uzima, baraka na nguvu za kiroho zitokazo kwa Mungu. (Isa. 44:3; Yn. 7:37-39)
D.            HITIMISHO  - 22:6-21
                Lengo la 10:  Eleza mambo muhimu yaliyomo katika Hitimisho;
1.        Anathibitisha kuwa unabii  huu ni wa kweli kwa sababu umetolewa na Bwana wa roho za Manabii ambaye aliwaongoza Manabii kunena
2.        Yesu anasema anakuja upesi na amebarikiwa yule atakayezingatia Unabii huu.
3.        Kila mtu  atapokea kulingana alivyotenda hapa duniani.
4.        Baraka ni kwa wale wanaoshika amri zake ambao watapewa haki ya kuuendea mti wa uzima na kuingia mji wa Yerusalemu mpya.
5.        Watu waovu wanaosema uongo na wauaji watatupwa katika ziwa la moto wa milele
6.        Roho Mtakatifu na Bibi Harusi (Kanisa) wanafanya kazi ya kuwaalika watu kupokea Neno la wokovu.
7.        Kuna hukumu juu ya watu ambao wanachagua sehemu Fulani na kuziacha zingine katika unabii huu.  Hivyo hivyo kwa wale wanaongezea mawazo yao juu ya Neno.
8.        Yohana anaitikia kuwa uje Bwana hii inamaanisha:
(a)     Wakristo wa kweli wanaomba na wanahamu ya kurudi kwa Bwana kwani ndipo ukombozi wetu utakamilika.
(b)     Siku ya kurudi Yesu imekaribia ambapo atarudi katika utukufu wake.
Je, mpendwa uko tayari kunyakuliwa?
MASWALI:
  1. Taja matukio mbali mbali yatakayotokea kabla ya Yesu Kristo kutawala?
  2. Eleza maana ya millennia kuhusiana na maoni ya:
(a)     Post millennialism _______________________
(b)     Amillennialism __________________________
(c)      Premillennialism ________________________
  1. Mambo gani yatakuwepo wakati wa utawala wa Kristo wa miaka elfu moja?
  2. Jehanam ni nini?
  3. Eleza kwa kifupi kuhusiana na mbingu mpya na nchi mpya.
CHANZO : DiraElimu
KUHUSU MWANDISHI
Rev Innocent Mkombozi Samuel Kamote alimezaliwa kijiji cha Kicheba  wilaya ya Muheza, Mkoa wa Tanga.
Ni Mchungaji na Mwalimu pia ni Mwandishji wa Vitabu na makala mbalimbali

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUFANIKIWA KI -UCHUMI KWA NJIA YA MUNGU

SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO