NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE
Na,PATRICK SANGA      Mithali 14: 1 ‘Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe’ .   Mchungaji mmoja rafiki yangu aliniambia asilimia hamsini mpaka sabini ya  changamoto au matatizo anayoshughulika nayo mara kwa mara katika kanisa  lake ni ya wanandoa. Kwa lugha nyepesi asilimia 50 – 70 ni matatizo  yatokanayo au yanayohusiana na ndoa. Binafsi pia kwa upande wangu  kupitia nafasi yangu katika mwili wa Kristo, email za wasomaji  ninazopata na pia baadhi ya semina za ndoa ambazo nimefanya kuhusu eneo  hili nimegundua kwa hakika ndoa nyingi za wana wa Mungu zina shida na  wao hawajajua kwamba vita hii inatoka kwa Shetani, maana anajua ndoa  zikitengamaa ni faida kwa ufalme wa Mungu na ni uharibifu kwenye ufalme  wake wa giza. Naam anapigana usiku na mchana ili kuhakikisha ndoa  hazitengamai kwa kuleta fujo za kila aina.   Kila siku katika ndoa kuna changamoto zinazaliwa mpaka imefika mahala  baadhi ya wanandoa wanawaza kwa nini...