HUDUMA YA KICHUNGAJI
Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima UTANGULIZI Katika sehemu nyingi za ulimwengu leo, kanisa la Mungu linakua kwa kasi, Matokeo yake kumekuwa na kundi kubwa la wakristo wanaohitaji huduma ya kichungaji na uongozi wa kiroho. Maandiko yanawaita watu hao kondoo ambao wanahitaji mchungaji wa kuwaongoza, kuwatunza, kuwahudumia, kuwalisha, na kusimamia usalama wao. Kristo alitumia mfano huu wa kondoo na mchungaji kuonyesha ni huduma gani watu wanaihitaji, Kwa bahati mbaya Pamoja na kuwa na wachungaji wengi na maaskofu wengi na waangalizi bado kondoo wengi hawajaweza kufikiwa kwa huduma ya kichungaji huduma hii inahitajika sana. Wewe mwenyewe umekuwa ni shahidi jinsi ambavyo umekutana na Kondoo wengi nje ya kanisa lako au waliokimbilia katika kanisa lako wakitokea sehemu nyingine na huenda labda kwa mchungaji au askofu maarufu sana au kanisa maarufu sana na ukashangaa kuona kuwa alishindwa kupata hudum...