Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 9, 2018

IFAHAMU ISRAEL

Top of Form 1.    NINI HATMA YA MGOGORO WA WAPALESTINA NA WAYAHUDI? 2.    NINI HATMA YA MGOGORO WA WAPALESTINA NA WAYAHUDI? 3.    NANI ANAPASWA KUWA MMILIKI HALALI WA NCHI HIYO? 4.    JUHUDI ZA USULUHISHI ZITAFANIKIWA? Mgogoro uliopo kati ya Wayahudi(Waisraeli) na Wapalestina umeigawanya dunia ambapo wapo wanaoamini kuwa Wayahudi ndio wanaopaswa kuwa wamiliki halali wa Nchi ya Israeli na wapo wanaoamini kwamba Wapalestina ndio wanaopaswa kuikalia Nchi hiyo kama Nchi yao . Kwa watu wengine Wayahudi wanaonekana ni watu wakatili wanaoikalia Nchi hiyo kimabavu huku wakiwanyanyasa Wapalestina. Wakati baadhi ya watu wanadai Wayahudi ndio wenye Nchi hiyo na Wapalestina wanaonekana ni Magaidi na watu wakorofi wanaowanyanayasa Wapalestina.Baadhi ya Wasomi na wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanaona kwamba Wapalestina wanatendewa visivyo. Baadhi ya Waislamu wao wanalichukulia suala la kunyanyaswa Wapalestina kuwa ni la mgogoro wa kidini na ...

ASILI YA ISRAEL

Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi. Akamuumba mtu akamweka katika nchi hiyo, akakubaliana naye kuwa ailinde, aitunze, tena aweze kuimiliki. Mtu huyo akakiuka Makubaliano yake na Mungu ambayo walikubaliana. Mtu huyo alifukuzwa na kuondolewa katika nchi ile aliyokuwa amewekwa ndani yake ili aweze kuitunza. Baada ya Mwaka elfu moja ya mtu huyo kufukuzwa kutoka katika nchi ile Mungu alimtafuta mtu miongoni mwa wanadamu atakaye mtumia kutimiza kusudi lake la moyoni mwake. Katika mpango huo akampata mtu ambaye aliitwa Abramu, ambaye baadaye alimbadlisha kutoka Abramu maana yake Kuhani wa Mungu akawa Abrahamu, baba wa Mataifa, Kuhani wa Mungu aliye hai. Ilikuwa imepita miaka elfu moja mpango wa kwanza uliposhindwa wa kumpata mtu huyo. Abrahamu alipewa masharti  ambayo akiyakubali ndipo akubaliwe kutumiwa na Mungu. Tunasoma katika kitabu cha Mwanzo  Sura ya Mwanzo 12: 1-3. BWANA akamwambia  Abrahamu, Toka wewe katika nchi yako  na jamaa zako, na nyumba...