Nini ukifanye wakati ukiwa mwanafunzi ?
Kuanzia mwezi huu wa saba 2016 tunakusudia kuwa na Club itakayojihusisha na masuala ya Kitaaluma pekee yake .Club hii itakuwa na utaratibu wa kukutana kwa ajili ya kubadilishana mada na wakati mwingine itakuwa na ratiba ya kuwatafuta walimu mahiri wa masomo ambao watawasilisha mada kutokana na uhitaji wa wanafunzi wenyewe. Mambo ya msingi katika Club hii itakuwa kujenga uwezo wa mwanafunzi kusoma kwa kujiamini,kufanya uchaguzi wa michepuo kutegemea dira ya maendeleo ya Kitaifa,kuunda urafiki wa kitaaluma unaoweza kumsaidia mwanafunzi kupata stadi mbalimbali zitakazomwezesha kuwa mbunifu,mdadisi na anayeweza kubadili changamoto kuwa fursa. MAHUSIANO NA WALIOTANGULIA KITAALUMA. Ni jambo baya sana kwa mwanafunzi kutojali waliofanikiwa.Ili aweze kufanikiwa anatakiwa kujifunza kwa waliofanikiwa .Ili aweze kujifunza lazima kuwepo mazingira maalum ya kubadilishana mawazo .Mwanafunzi wa kidato anatakiwa kuwa karibu na mwanafunzi wa kidato cha pili,mwanafunzi wa kidato cha pili an...