NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE
 SEHEMU YA NNE B  Na: Patrick Sanga     Nafasi ya tano – Mwanamke kama Mjenzi   Katika sehemu ya 4a tulianza kwa kuangalia nafasi ya tano hata hivyo  kutokana na urefu wake nikaona vema kuigawanya nafasi hii ya tano katika  kipengelea a na b. Ili kusoma sehemu ya 4a bonyeza link ifuatayo  https://nsanacz.blogspot.com/2018/05/namna-mwanamke-anavyoweza-kutumia_47.html Katika sehemu ya 4b tutangalia ni kwa namna gani mwanamke atapata  hekima ya kumsaidia kujenga ndoa yake. Karibu sasa tuendelee…   Hebu tuanze kwa kuangalia mstari wa ajabu sana katika Muhubiri 7: 12 unasema ‘Kwa maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi, na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliyonayo’ .  Hekima ndio nguzo kuu ya ujenzi wa ndoa yako, naam ukiwa nayo ni  dhahiri kwamba italeta uponyaji kwenye ndoa yako pia. Mwanamke kama  mjenzi anahitaji kuwa na hekima ili kulinda ndoa yake akijua kwamba ki –  nafasi yeye ni Mlinzi wa mumewe. Kumbuka kwamba andiko letu la msingi  katika se...