MUNGU ALIVYOWATENDEA WATU WA FPCT MWAHURI-KISESA KATIKA MKUTANO
Na.AYOUB JL Hakika tulimwona Mungu kipekee katika Mkutano wa Injili KAMILI YA KRISTO kwani watu walifunguliwa kutoka katika vifungo vya dhambi na nguvu za giza na kuachiliwa huru.Mtumishi wa Mungu kutoka Dar es Salaam Mchungaji BONIPHACE MBISE alihitimisha Mkutano kwa kuongoza maombi ya ujazo wa Nguvu za Roho Mtakatifu,kupinga kazi za shetani katika kila eneo (ardhi,anga,kusini,mashariki,magharibi na kaskazini). Aidha maombi ya kuombea Taifa letu la Tanzania yalikuwa ya kipekee kwa sababu hakuna eneo lililosaulika kuanzia MHE.RAIS,MAKAMU RAIS,WAZIRI MKUU,MAWAZIRI,SPIKA WA BUNGE,NAIBU,WABUNGE na viongozi wote.)Lakini pia aliombea raslimali za Taifa na watu wake. Watu waliompokea YESU wakipewa sala ya toba. Was...