VIZUIZI VINAVYOWAFANYA WATU WASIPENDE KUJIFUNZA NENO LA MUNGU
Na, Mch.JULY BOSHA FPCT KISESA Katika semina za NENO la Mungu zilizoendelea FPCT Kisesa Mtumishi wa Mungu Mch. JULAI BOSHA akiwa amejawa na nguvu za Roho Mtakatifu aliwafundisha wanafunzi wa Kristo (Zamani Washirika) kuwa watu wengi hawapendi mafundisho ya Neno la Mungu kutokana na sababu zifuataz :- 1. Makuhani/Wachungaji kutofundisha kweli ya Mungu ipasavyo .Ezek 22:26 “ Makuhani wake wameihalifu sheria yangu, wametia unajisi vitu vyangu vitakatifu; hawakuweka tofauti ya vitu vitakatifu na vitu vya kutumiwa sikuzote; wala hawakuwafundisha watu kupambanua vitu vichafu na vitu vilivyo safi, nao wamefumba macho yao , wasiziangalie sabato zangu, nami nimetiwa unajisi kati yao”. Alieleza kuwa watumishi wengi hawana muda wa utosha katika kuandaa mafundisho na matokeo yake hujikuta wandaa mafundisho manyonge. Baadhi hupenda kuwaachia wasaidizi wao kulisha kundi huku wao wakisafiri kwenda matawi mengine kuliko kuli...