VIZUIZI VINAVYOWAFANYA WATU WASIPENDE KUJIFUNZA NENO LA MUNGU
Na, Mch.JULY BOSHA FPCT KISESA
Katika semina za NENO la Mungu zilizoendelea FPCT Kisesa
Mtumishi wa Mungu Mch. JULAI BOSHA akiwa amejawa na nguvu za Roho Mtakatifu
aliwafundisha wanafunzi wa Kristo (Zamani Washirika) kuwa watu wengi hawapendi
mafundisho ya Neno la Mungu kutokana na sababu zifuataz :-
1. Makuhani/Wachungaji
kutofundisha kweli ya Mungu ipasavyo.Ezek 22:26 “Makuhani
wake wameihalifu sheria yangu, wametia unajisi vitu vyangu vitakatifu; hawakuweka
tofauti ya vitu vitakatifu na vitu vya kutumiwa sikuzote; wala
hawakuwafundisha watu kupambanua vitu vichafu na vitu vilivyo safi, nao
wamefumba macho yao, wasiziangalie sabato zangu, nami nimetiwa
unajisi kati yao”. Alieleza kuwa watumishi wengi hawana muda
wa utosha katika kuandaa mafundisho na matokeo yake hujikuta wandaa mafundisho
manyonge.
Baadhi hupenda kuwaachia wasaidizi wao kulisha
kundi huku wao wakisafiri kwenda matawi mengine kuliko kulisha matawi
yao.Wachungaji ndiyo wenye dira(maono ) ya watu walio chini yao lakini
hujisahau wiki au miezi kadhaa na kuondoka kila mialiko wanayopata.Aliwasihi
kufanya mabadiliko na kutumia muda mwingi kulisha mawati yao kuliko kusafiri kila
mara.Aidha aliwasihi viongozi kuwaangalia wachungaji katika mahitaji mengine
ili wao pia walishe kundi kwa kuwa hali ngumu ya maisha na kujikuta wanatumia
muda mwingi kusaka mahitaji binafsi ,familia na wategemezi.
2.
Kutokuwa makini kufuatilia mafundisho. Yer 32:33. Katika hili alisema
wanafunzi wengi wa Kristo hawako makini kufuatilia neno la Mungu na kujikuta
hawakui Kiroho siku hadi siku. Alisema mwanafunzi mzuri huwa makini kufuatilia
mafundisho.
3. Kutokuzingatia/kutokujali
au kupuuzia.
1
Kor 1 :18 “Kwa sababu neno la msalaba
kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu”.Wanafunzi wengi wana kawaida
kutofuatilia kwa kina mafundisho ya NENO LA MUNGU.Ama kwa makusudi au uzembe
tu.Mwanafunzi asiyefuatilia mafundisho hujiandaa kufanya vibaya.
4. Kukosa
utulivu wa akili katika ibada. Rum 10 :2 “Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa
ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.” Alisema kuwa wanafunzi wengi ambao muda
mwingi wanakuwa na mambo mengi(busy) katika ibada na kujikuta hawajifunzi
chochote mfano kuna watu ambao hukaa kupokezana watoto wachanga na kujikuta
wakipitwa na huduma .
Aliendelea
kufundisha sababu nyingine kama :-
5. Ugumu wa mioyo ( Math 13 : 4-5),mamb mengi yapo kwenye
mioyo na kujikuta wanakuwa wagumu kupokea mafundisho.
6. Shughuli za utafutaji huchukua nafasi ya kwanza kuliko
Mungu. Math 13 : 7
7. Mapokeo ya kidini/mazoea. Matendo 7 : 1,6: 1 .Watu
hawataki kupokea neno la Mungu kwa kisingizio cha ujuaji na kushikilia misimamo
ya imani zao.
8. Nguvu ya mpinga Kristo (roho ya mpinga kristo.).Shetani
yupo kazini na hayuko tayari kuona watu wanapokea mafundisho badala yake
atawaziba masikio wasisikie,macho wasione na kujikuta wanapotea “Sikilizeni neno hili, enyi watu wajinga msio na
ufahamu; mlio na macho ila hamwoni; mlio na masikio ila hamsikii. Yer 5
:21 , Lakini
ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;
ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. 2Wakorintho4
ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. 2Wakorintho4
Alisisitiza
watu wa Mungu wapende kujifunza kwa kuna hazina imefichika katika Neno la Mungu
( Ay 35 : 11,34 :32 na 1Yoh 2 :27 ,Zab
32 :8,25 :8 )
IMEANDIKWA NA AYOUB LEO
MUNGU AKUBARIKI SANA UNAPOFUATILIA MAFUNDISHO
HAYA.
Maoni