NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE (Part 2)
Na: Patrick Sanga Maada: Nafasi ya Msaidizi, Mshauri na Mleta kibali Ili kusoma sehemu ya kwanza bonyeza link hii https://nsanacz.blogspot.com/2018/05/namna-mwanamke-anavyoweza-kutumia.html Mpenzi msomaji, Mungu akubariki kwa kufuatilia mfululizo wa somo hili. Ni imani na maombi yangu kwamba masomo haya yatafanyika msaada kwenye maisha yako na ndoa yako kwa ujumla. Katika sehemu hii ya pili nitaandika kuhusu nafasi tatu ambazo ni nafasi ya Mwanamke kama Msaidizi, Mshauri na Mleta kibali. Mwanamke kama Msaidizi Mwanzo 2:18 ‘ BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye’ . Ukisoma mstari huu katika toleo la GNB Biblia inasema ‘ Then the LORD God said, “It is not good for the man to live alone. I will make a suitable companion to help him. ” Biblia inatueleza kwamba Adam ndiye aliyetangulia kwanza kudhihirishwa kabla ya Mwanamke. Kabla ya Hawa kuletwa, Mungu alimpa Adam majukumu mengi ambayo alip...