KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU KATIKA KWELI YOTE
NA MWL, AYOUB LEO WIKI YA MAOMBI TAREHE 08,10,11,12,NA 12 JANUARI 2018,FPCT KISESA Roho Mtakatifu ni nani ? Ni Roho wa Mungu .Kwa nini anaitwa Roho wa Mungu ? Kwa sababu ni Mungu mwenye sifa za Ki-ungu.Sifa hizo ni :- v Anadumu milele Ebr 9 :14 v Yupo kila mahali v Ni mwenye nguvu zote v Ana ufahamu wote v Anafufua v Anaumba KAZI YA ROHO KATIKA KUONGOZA WATU KWENYE KWELI YOTE a) Kuwapasha wana wa Mungu juu ya mambo yajayo Yoh 16 :13. Wanadamu hawana uwezo wa kujua yanayotokea mbeleni pasipo kuwa na msaada wa nguvu juu yao.Roho Mtakatifu ndiye awezaye kuwafunulia na kuwajulisha juu yale yatakayokuwepo. b) Kuwajulisha /kuwahakikishia wana wa Mungu juu ya urithi wao kwa Mungu .Roho Mtakatifu ndiye anayeweza kuwapa uhakika wa kile wanachorithi au watakachopokea kutoka kwa Mungu.Gal 4:6-7,Rum 8 :14-17 c) Kuwaongoza wana wa Mungu katika kuishinda dhambi ...