KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU KATIKA KWELI YOTE

NA MWL, AYOUB LEO
WIKI YA MAOMBI TAREHE 08,10,11,12,NA 12 JANUARI 2018,FPCT KISESA
Roho Mtakatifu ni nani ?
Ni Roho wa Mungu .Kwa nini anaitwa Roho wa  Mungu ?
Kwa sababu ni Mungu mwenye sifa za Ki-ungu.Sifa hizo ni :-
v  Anadumu milele Ebr 9 :14
v  Yupo kila mahali
v  Ni mwenye nguvu zote
v  Ana ufahamu wote
v  Anafufua
v  Anaumba
KAZI YA ROHO KATIKA KUONGOZA WATU  KWENYE KWELI YOTE
a)    Kuwapasha wana wa Mungu juu ya mambo yajayo Yoh 16 :13.Wanadamu hawana uwezo wa kujua yanayotokea mbeleni pasipo kuwa na msaada wa nguvu juu yao.Roho Mtakatifu ndiye awezaye kuwafunulia na kuwajulisha juu yale yatakayokuwepo.
b)    Kuwajulisha /kuwahakikishia wana wa Mungu juu ya urithi wao kwa Mungu.Roho Mtakatifu ndiye anayeweza kuwapa uhakika wa kile wanachorithi au watakachopokea kutoka kwa Mungu.Gal 4:6-7,Rum 8 :14-17
c)    Kuwaongoza wana wa Mungu katika kuishinda dhambi Rum 8 : 26,Yoh 16:8
ü  Kwa sababu yeye huifunua dhambi na kuiweka bayana.1cor 14:24-25,Ebr 4:12-13,Mdo 5:1-11
ü  Kwa sababu yeye anahukumu dhambi na kuhakikisha ukweli juu ya dhambi Mdo 5 :1-11
ü  Kwa sababu yeye anatoa nguvu za kuishinda dhambi Gal 5:16.Roho Mtakatifu ndiye mwenye uwezo wa kumpatia mwana wa Mungu nguvu za kushinda dhambi kwa kuwa yeye anapokaribishwa na kuwa ndani yako anakufanya uishi kama Roho wa Mungu anavyotaka na hivyo utaishi kwa kufuata yale Roho anayotaka ufanye.
d)    Kuwaongoza wana wa Mungu kuwa na nguvu za kuyastahimili na kushinda majaribu.Lk  4 : 1-13,Math 4:1-11,Mark 1:12 -13.Yesu akiwa amejaa Roho Mtakatifu aliongozwa kwenda kwenye majaribu ya shetani na mwisho alimaliza akiwa mshindi katika jaribu.
Wana wa Mungu wanahitaji nguvu za Mungu ili waweze kuwa thabiti kuyashinda majaribu.Majaribu ni mitihani,kama majaribu ni mitihani Roho Mtakatifu akiwa juu yako atakuambia na kukupa nguvu za kushinda jaribu linalokukabili.Kumbuka hakuna njia ya mkato ya kuepuka jaribu, jaribu linaposimama ni lazima lifike mwisho ndipo tunaweza kuvuka na kupiga hatua nyingine.
e)    Kuwaongoza wana wa Mungu katika kufundisha na kujifunza NENO la Mungu ipasavyo.Yoh 14 :26.Roho Mtakatifu ndiye Mwalimu Mkuu katika mambo yanamhusu Mungu kwa sababu analithibitisha neno na kulifanya kuwa hai kwa wakati uliopita,uliopo na unaokuja.
Lakini pia fikiria Neno la Mungu linafundishwa kwa watu wenye mila tofauti,elimu tofauti,historia tofauti na jinsi tofauti lakini kila mmoja hupokea na kujengwa kwa kadri Roho wa MUNGU alivyokusudia.
f)     Kuwaongoza wana wa Mungu kusema au kunena ipasavyo (kuwa na mwitiko sahihi pale wanapopaswa kuitikia hoja) 2Pet 1:21.Kuna nyakati wana wa Mungu wanakutana na hoja au maswali juu ya wokovu au maisha yao ya utakatifu.Anayeweza kuwapa majibu sahihi ya kuwajibu wale wanaouliza juu ya wokovu tunaweza kuwajibu majibu sahihi kama tukiwa ndani ya Roho Mtakatifu.Hivyo ni muhimu sana kuwa na nguvu hii kwa kuwa maswali ni mengi.
Mkumbuke Petro alivyomjibu simon mchawi alipotaka kununua nguvu ya Mungu ya kuwaponya watu kwa fedha.Kumbuka wewe kama mwana wa Mungu unahitaji mafuta ya Mungu ili uwahubiri au kuwashudia watu maneno ya Mungu.Isaya 61: 1 “ Roho ya Mungu I juu yangu;kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema ,amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo,kuwatangazia mateka uhuru wao,na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao ..
KWA NINI TUNAHITAJI KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU ?
1.    Ili atufundishe NENO la Mungu ipasavyo.Yoh 14:26.Roho Mtakatifu anafundisha elimu yote inayohusu maisha yetu kwa kuwa anajua ufahamu wetu na upungufu (udhaifu wetu ).Roho Mtakatifu ana uwezo mkubwa wa kujua maarifa yanayohitajika kwa wakati sahihi na mahali sahihi.Kila anapoachilia Neno anajua linahitajika kwako ni la kwako.Math 10:19 -20,2Tim 3:16 -17.
2.    Ili tuzae matunda yanayompendeza Mungu.Gal 5:22-25,Ef 5:9.Roho Mtakatifu akiwa ndani yetu anasababisha tuwe na upendo,utu wema,uaminifu,upole,kiasi,uvumilivu.Hatuwezi kuzaa matunda ya Roho Mtakatifu kama hatuna Roho Mtakatifu ndani yetu.Hauwezi kuwasamehe watu kama huna msamaha ndani yako,lazima uwe na msamaha ndipo utasamehe,lazima uwe na upendo ndipo unaweza kuwapenda wengine.Huwezi kutoa kile usichokuwa nacho.Wakumbuke watumishi wa Mungu walivyosema pindi walipoombwa msaada na mhitaji.Walisemi kile tulicho nacho ndicho tukupacho,simama uende ?.Wangapi unashindwa kuwatendea wema ? tafuta nguvu za Mungu ili uzae ,matunda yanayompendeza Mungu.
3.    Ili tuvune uzima wa milele .Gal 6 :8,Rum 8:13.Kama mwana wa Mungu anatamani kuwa na maisha yanayodumu lazima awe na Roho Mtakatifu kwa kuwa ataishi milele.Ataishi milele yeye mwenyewe au kupitia kazi zake alizofanya.Maana yake ataacha alama isiyofutika kwa wema aliofanya.Mkumbuke Dorcas .Kupitia kazi zake aliishi tena,yaani kazi alizowafanyia wajane zilimfanya kuishi tena.
4.    Ili tuwe watoto (wana wa Mungu ) na kumwabudu Mungu ipasavyo.Rum 8:9,Yoh 3 : 5 -7,4 :23 -24. Roho Mtakatifu ndiye anayetufanya tuitwe wana wa Mungu,anatengeneza ushirika uliothabiti na kutuingiza katika ufalme wa Mungu.Tukiwa katika ufalme (nguvu zake ) tunamwabudu kwa Roho na kweli.Tukifanywa wana wa Mungu ndipo tunapoweza kumpenda Mungu kwa dhati,tutapenda ibada toka moyoni,moyo utasikia hatia pale tunachelewa au kuikosa ibada..
Ukiona hausikii kujuta pale inapotokea hujapata muda wa kuwa mbele za Mungu,unapaswa kujiuliza.
v  Unawezaje kuona kawaida kukaa muda au siku pasipo kwenda katika  ibada ?.Wewe si mwana wa Mungu ndiyo maana unaona kawaida kumaliza majuma mengi kiasi hicho bila kuwa mbele za Mungu.
v  Wewe unawezaje kuishi pasipo nguvu za Mungu?.Unakumbuka wanafunzi wa Yesu walivyoambiwa wakae mpaka wapokee nguvu ?
5.    Ili tufanyiwe kibali machoni pa Mungu na wana wanadamu. 2Tim 2:15,1Tim 4:6,tito 2:7-8
Mwana wa Mungu anapobatizwa kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu anafanywa upya .Maana yake yakale yanapita na kuwa mpya .Rum 8 :11,Eze 39:29,36:26.
v  Tumkumbuke Esta kabla ya kwenda kwa mfalme alitafuta kibali kwanza. Esta 2:17, 5:2, 7:3, 8:5).
v  Yesu alipewa kibali na Mungu mwenyewe –Math 3 :17
v  Paulo alikubalika kwanza      1Thes 2:4
v  Timotheo anaambiwa na Paulo atafute kukubalika -2Tim 2:15
v  Wana Israel walipewa kibali mbele ya mamisri na wakapewa vyombo vya dhahabu na vya fedha walivyotaka –Kut 11 :3
v  Mungu alimpa Yusuf Kibali mbele ya mkuu wa  gereza ,ndipo akawa Mkuu –mwanzo 39: 21.
v  Mungu alimpa Daniel Kibali na huruma mbele ya mkuu wa matowashi .Akapewa ruhusa ya kutokula vyakula vyenye unajisi –Dan 1 :9
v  Ruthu alipewa kibali mbele ya Boazi ,mwishowe aliolewa japokuwa hakuwa mwisraeli.
v  Daudi alipata kibali mbele ya Sauli.
“Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema, tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu (Ikulu); maana AMEONA KIBALI MACHONI PANGU”
(1Samweli 16:22).
v  Nehemia alipata kibali mbele ya Mfalme; akapewa ruhusa ya kutoka kwenda kuujenga mji wa Yerusalemu na akapewa na vifaa vya kuujengea.
(Nehemia 2:5-8).
Kibali cha kila mwana wa Mungu kinapatikana toka kwa Mungu,kibali kinatengenezwa .Anayetengeneza kibali chako ni ROHO MTAKATIFU maana anakutambulisha kwa Mungu na kukufanya ufahamike kwa Mungu na mwisho kila utakalofanya litakubalika.Mungu akubariki sana.
MWALIMU AYOUB JACOB LEO ANAPATIKANA KANISA LA FPCT KISESA-MWANZA.

SIMU NAMBA  0755 035 722 AU 0785 64 51 77 ,Barua pepe :ayoubleo@yahoo.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUFANIKIWA KI -UCHUMI KWA NJIA YA MUNGU

UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI

SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO