DHANA YA UJASIRIA MALI

DHANA NA ASILI YA UJASIRIAMALI

Ujasiriamali kama somo limetokea kupendwa na watu wengi hasa katika jamii ya kisasa, lakini ni watu wachache wanaojua nini hasa maana ya ujasiriamali,mjasiriamali ni nani, chimbuko la ujasiriamali ni  wapi, zipi ni sifa za mjasiriamali, nini mchango wa mjasiriamali katika maendeleo ya Taifa, je faida za kuwa mjasiriamali  ni zipi. Ukijiuliza maswali haya utagundua kuwa kuna umuhimu wa kujifunza zaidi ju ya ujasiriamali. Ujasiriamali ni nyanja ambayo ikitiliwa mkazo inaweza kuleta mapinduzi katika ukuaji wa uchumi,teknolojia,siasa na utamaduni wa jamii husika.

Katika muktadha wa Tanzania ujasiriamali kama zana ya msingi katika kukuza uchumi bado haujapewa kipaumbele kwani wadau na washika dau bado hawajaweka mtazamo chanya na nguvu katika kutoA elimu ya ujasiriamali kwa wananchi. Watanzania wengi wamekosa elimu hasa elimu ya mfumo rasmi(darasani) lakini elimu ya ujasiriamali inaweza tolewa popote bila hata kufuata mfumo rasmi na ikawafikia watu wengi nao wakanufaika.
   
Nyanja hii ya ujasiriamali imefanyiwa utafiti na kuandikwa na kujadiliwa na wanazuoni na wasomi mbalimbali. Lengo ni kufanya ujasiriamali kuwa  mhimili unaojitegemea ambao unaweza kutengeneza fursa za kimaendeleo.

Wazo la ujasiriamali lilianzishwa mnamo miaka ya 1700 iliyopita,lakini bado maana iliyotolewa kipindi hicho ina nguvu japokuwa kuna maana nyingi zimekwisha tolewa na zinaendelea kutolewa. Hapo mwanzo UJASIRIAMALI ulijulikana kama ni "kitendo cha kuanzisha biashara"lakini wanauchumi wengi wanaamini ujasiriamali una maana zaidi ya hapo.

Baadhi ya wanauchumi wanaona kuwa mjasiriamali ni mtu ambaye yupo tayari kuthubutu au kuanzisha jambo jipya ambalo litampa faida au litakuwa na nafasi ya kumpa faida hapo daadaye. Lakini wengine wanadai kuwa mjasiriamali ni mbunifu ambaye ubunifu wake anaunadi na kuutumia ili apate faida. Wengine wanasema "mjasiriamali anabuni bidhaa mpya au njia mpya ya uzalishaji wa bidhaa ambayo soka linahitaji bidhaa hiyo au hiduma hiyo ambayo haijapata kusambazwa hapo kabla".


Mnamo karne ya 20 mwanauchumi Joseph compete (1883-1950) anamtazama mjasiriamali kama "mvumbuzi , mbunifu ,anayeleta mageuzi na mabadiriko".Compete anaendelea kusema "mjasiriamali anamsukumo wa ubunifu , mjasiriamali anabeba mchanganyiko mpya ambao unatoa nafasi au kusaidia viwanda vya zamani kubadirika na kuwa na mfumo mpya wa kuzalisha , kufanya biashara  na kutoa huduma.

mtaalamu wa biashara Peter Drunker anaendeleza wazo hili kwa kusema kuwa "mjasiriamali ni mtu ambaye kiukweli anatafiti kwa lengo la kuleta mabadiriko na anawajibika katika mabadiriko hayo,pia anatumia mabadirko kama changamoto katika kujiletea tija na ufanisi katika kazi zake

kwa ujumla tunaweza kusema kuwa ujasiriamali ni kitendo cha kuchukua hatua na kuanzisha kitu (biashara) kipya au kufanya jambo ambalo linafanywa na wengine lakini katika njia tofauti huku ubunifu na mipango thabiti inayoambatana na ujasiri pamoja na msukumo wa dhati wa kufanya kazi kwa didii ukiwa ndani ya mjasiriamili mwenyewe.

Wanauchumi wengi sasa wanakubali kwamba ujasiriamali ni kiungo muhimu katika kukuza na kuendeleza uchumi wa taifa,ujasiriamali ni njia mbadala ambayo ya kuongeza nafasi za ajira. Katika nchi zinazo endelea biashara ndogo zilizofanikiwa ni msingi ni msingi katika kuongeza ajira,kuongeza kipato na kupunguza umasikini, hivyo basi ni wajibu wa serikiali kusaidia wajasiriamali wakubwa kwa wadogo ili kuongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa na huduma kwani hatua hiyo itatoa mchango chanya katika mipango ya maendeleo ya nchi au Taifa husika.


MJASIRIAMALI NI NANI? (sifa za mjasiriamali)

  • Ni mtu ambaye anaanzisha na kumiliki kampuni
  • Ni mtu ambaye yupo tayalia kuthubutu
  • Ni mtu ambaye ni mbunifu
  • Ni mtu jasiri asiye ogopa kufeli au kushindwa
  • Ni mtu ambaye kilasiku anatafuta njia mpya za kuzalisha na kuleta upya na mabadiriko
  • Ni mtu mvumilivu
  • Ni kiongozi
  • Ni mshindani asiyekata tamaa
  • Ni mtu ambaye anapenda kuwajibika na kazi kwa bidii
  • Ni mtu anayetazama maisha ya mbele
  • N mtu ambaye anaweza kubadirisha na kutumia nafasi kama fulsa. 
  • Ni mtu ambaye anahitaji na anahamu ya mafanikio
  • Ni mtu ambaye anaweza kujitegemea.
Je wewe unasifa hizo hapo juu? lakini sio lazima uwe nazo zote zilizo orodheshwa hapo juu, hata sifa chache tu zina kufanya uwe mjasiriamali. kitu cha kuzingatia ni kwamba baadhi ya sifa mtu huzaliwa nazo na zingine mtu hujifunza tu, hivyo nawe unaweza jifunza na ukawa mjasiriamali mkubwa na mwenye mafanikio.

JE UPOTAYARI KUWA MJASIRIAMALI?

kama unata kuwa mjasiriamali basi jibu maswali yafuatayo, kama majibu yako yatakuwa ndio basi wewe ni mjasiriamali lakini kama majibu yako hayatakuwa ndio basi unaweza kujipanga upya na ukatafuta namana     nyingine ya kueweza kuwa mjasiriamali labda kwa kujifunza dhana za ujasiriamali.

maswali

1. je umejiandaa kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza marengo?

2. je upo tayali kukumbana na kutatua matatizo na changamoto?

3. je unayafahamu vizuri mazingira unayoishi na je upo tayali kuyatumia na kuanzisha jambo jipya/

4. je upotayari kusubili kwa muda mrefu matunda ya juhudi zako?

FAIDA ZA UJASIRIAMALI

  • kukuza na kuendeleza uchumi katika nchi
  • kupunguza umasikini miongoni mwa watu
  • ujasiriamali hutusaidia kutumia ipasavyo rasilimali tulizonazo
  • matumizi sahihi ya rasilimali watu
  • ujasiamali hutupa mwanga katika kufanya na kuanzisha shughuri mpya
  • ujira binasfsi na nafasi za ajira kwa watu wengi
  • hupunguza kiwango cha umasikini miongoni mwa watu
  • hupunguza tofauti katika maendeleo baina ya watu, mikoa, nchi n.k

VITU VINAVYOMJENGA MJASIRIAMALI

  • MTAJI
  • FURSA
  • UBUNIFU
  • MAWASILIANO
MTAJI
ni kitu chochote ambacho mjasiliamali anawezatumia katika kuzalishia au kufanyia jambo flani kwa lengo la kupata faida. mtaji umegawanyika katika miundo ifuatayo:- mtaji wa fedha,nguvu kazi,mtaji jamii,elimu na utaalamu katika jambo flani.

FURSA
Fulsa ni kama uti wa mgongo kwa mjasiliamali. mjasiliamali lazima awe na uwezo wa kutambua au kugundua fulsa, uwezo wa kuchambua na kuchanganua fulsa pia kuchukua hatua juu ya fulsa husika.

UBUNIFU
Kwa kawaida mjasiliamali anatakiwa kuwa mbunifu, ubunifu ndio unamtofautisha mtu mmoja na mwingine hata kama wote watafanya jambo linalo fanana. kilasiku unatakiwa kufikili ni jinsi gani utafanya jambo jipya ua jambo lililofanya na wengine lakini wewe ufanye katika njia tofauti.

MAWASILIANO
Mawasiliano huunganisha vitu pamoja ana huweka watu pamoja na husaidia kupata taarifu huhimu  katika biashara yako.Mawasiliana huunganisha mtaji, fulsa na ubunifu, mjasiliamali anatakiwa kuboresha mawasiliano ili afanikiwe katika ujasiliamali wake.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUFANIKIWA KI -UCHUMI KWA NJIA YA MUNGU

UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI

SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO