Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba 3, 2017

AWAMU YA TATU YA MIKOPO ELIMU YA JUU 2017/2018

WANAFUNZI 7,901 WAPANGIWA MIKOPO KATIKA AWAMU YA TATU KWA 2017/2018 Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa orodha ya Awamu ya Tatu ya wanafunzi 7,901 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 29,578. Katika Awamu ya Kwanza, wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo na Awamu ya Pili wanafunzi 11,481. Orodha hiyo ya Awamu ya Tatu inapatikana hapa.   Aidha, orodha hii inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz) na itatumwa kwa vyuo husika. Kiasi cha shilingi 427.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na tayari Serikali imeshatoa shilingi 147.06 bilioni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/2018.

MIKOPO YA ELIMU YA JUU

Picha
Friday, November 3, 2017 Bodi ya mikopo Yawatoa Hofu Wanafunzi Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu nchini (HESLB) imewatoa hofu wanafunzi waliokosa mikopo kwakuwa ipo katika hatua za mwisho kutoa majina ya awamu ya tatu. Kauli hiyo imekuja ikiwa leo   ni siku ya mwisho iliyotolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ya kuitaka bodi hiyo kuhakikisha kila mwanafunzi mwenye sifa anapewa mkopo. Akizungumza leo Novemba 3,Meneja Mawasiliano wa bodi hiyo, Omega Ngole amesema agizo hilo linaendelea kutekelezwa na kwamba hadi kufikia kesho  kila mwanafunzi mwenye sifa atapata mkopo. Amesema kwa wale watakaokosa mkopo wanaweza kukata rufaa kupitia bodi hiyo ili kupitia upya taarifa zao. “Maelekezo hayo yote yanatekelezwa na tutakamilisha leo na tutatoa taarifa ya kuhusu utekelezaji wake wiki ijayo,” amesema Katika mwaka wa masomo wa 2017/18 Serikali imetenga bajeti ya Sh427 bilioni