MIKOPO YA ELIMU YA JUU
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Friday, November 3, 2017
Bodi ya mikopo Yawatoa Hofu Wanafunzi
Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya juu nchini (HESLB) imewatoa hofu wanafunzi
waliokosa mikopo kwakuwa ipo katika hatua za mwisho kutoa majina ya
awamu ya tatu.
Kauli
hiyo imekuja ikiwa leo ni siku ya mwisho iliyotolewa na Naibu Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ya kuitaka bodi hiyo
kuhakikisha kila mwanafunzi mwenye sifa anapewa mkopo.
Akizungumza
leo Novemba 3,Meneja Mawasiliano wa bodi hiyo, Omega Ngole amesema
agizo hilo linaendelea kutekelezwa na kwamba hadi kufikia kesho kila
mwanafunzi mwenye sifa atapata mkopo.
Amesema kwa wale watakaokosa mkopo wanaweza kukata rufaa kupitia bodi hiyo ili kupitia upya taarifa zao.
“Maelekezo hayo yote yanatekelezwa na tutakamilisha leo na tutatoa taarifa ya kuhusu utekelezaji wake wiki ijayo,” amesema
Katika
mwaka wa masomo wa 2017/18 Serikali imetenga bajeti ya Sh427 bilioni
kwaajili ya mikopo ambapo wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza
watanufaika na fungu hilo.
Hadi
sasa Jumla ya wanafunzi 21,677 maombi yao yamekubaliwa ikiwa ni awamu
mbili zilizotolewa na bodi hiyo ambapo awamu ya kwanza ilitoa majina
10,196 na ya pili 11,481.
Meneja
huyo amesema kwa wale waliodahiliwa kwenye vyuo walivyothibitisha
kupitia Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) tayari fedha zimeanza kutumwa kwenye
vyuo husika.
“Mwanafunzi
akipangiwa mkopo halafu asipoliridhika, akaona uhitaji wake ni mkubwa
kuliko kiwango alichokipata kuna nafasi ya kukata rufaa ambayo itaanza
wiki ijayo,”amesema.
M
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni