DHANA YA UJASIRIA MALI
DHANA NA ASILI YA UJASIRIAMALI U jasiriamali kama somo limetokea kupendwa na watu wengi hasa katika jamii ya kisasa, lakini ni watu wachache wanaojua nini hasa maana ya ujasiriamali,mjasiriamali ni nani, chimbuko la ujasiriamali ni wapi, zipi ni sifa za mjasiriamali, nini mchango wa mjasiriamali katika maendeleo ya Taifa, je faida za kuwa mjasiriamali ni zipi. Ukijiuliza maswali haya utagundua kuwa kuna umuhimu wa kujifunza zaidi ju ya ujasiriamali. Ujasiriamali ni nyanja ambayo ikitiliwa mkazo inaweza kuleta mapinduzi katika ukuaji wa uchumi,teknolojia,siasa na utamaduni wa jamii husika. Katika muktadha wa Tanzania ujasiriamali kama zana ya msingi katika kukuza uchumi bado haujapewa kipaumbele kwani wadau na washika dau bado hawajaweka mtazamo chanya na nguvu katika kutoA elimu ya ujasiriamali kwa wananchi. Watanzania wengi wamekosa elimu hasa elimu ya mfumo rasmi(darasani) lakini elimu ya ujasiriamali inaweza tolewa popote bila hata kufuata mfumo rasmi na ikawaf...