SIFA ZA MJASIRIA MALI

Watu wengi wamekuwa wakilitumia hili jina MJASIRIAMALI bila wao kutambua kama wanalitumia sahihi au sio sahihi wengi wanaamini kuwa ni wajasiriamali lakini sio wajasiriamali ni wafanyabiashara japo wengi hujiita wajasiriamali.Mjasiriamali ni mtu gani?
Huyu ni mtu ambae anaweza kutumia jamii inayomzunguka katika kuanzisha fursa mbalimbali za kibiashara ambazo zitampatia kipato,mtu huyu huweza kuitumia rasilimali watu ili kujinufaisha,watu wengi wanaamini kufungua duka ni kuwa mjasiriamali hapana unaweza kufungua duka lakini bado ulichokifungua na jamii inayokuzunguka hakina faida na ni idadi ndogo tu ya watu ndio watakubaliana nacho lakini pia umefungua duka lakini unasubiria wateja waje tu,huu sio ujasiriamali bali ni ufanyabiashara.mjasiriamali biashara yake haina msimu maalumu lakini mfanyabiashara biashara yake inamsimu maalum.Zifuatazo ni sifa za mjasiria mali.

1. ANAPENDA KUJIFUNZA
Hapa ndipo ugonjwa wa watu wengi ulipo mtu anajiita mjasiriamali lakini muulize kasoma vitabu vingapi vya ujasiriamali au kahudhuria semina ngapi za ujasiriamali watanzania wengi tunapenda sana vitu vya urahisi hatupendi kujifunza kama kweli unataka kuwa mjasiriamali au ni mjasiriamali lazima uwe na sifa hii upende kujifunza kutoka kwa watu wengine na uhudhurie semina au mafunzo mengi ya ujasiriamali la sivyo utabaki kuwa mfanyabiashara.Maarifa siku za leo yamekuwa rahisi kuliko zamani.Unaweza kutumia simu yako kujifunza kwa kupitia kurasa mbalimbali za wataalam au watu mbalimbali waliojitoa kueleza ujuzi katika fani mbalimbali.
Jifunze vitu vinavyokuongezea ufahamu kuliko picha na video za ngono.Soma na sikiliza taarifa kuhusu shughuli zako.Kuna msemo usemao asiyetaka kujifunza atakuwa funza.
2. MBUNIFU
Mjasiriamali yoyote ni mbunifu,ninapozungumzia ubunifu ninamaana je unapata kitu tofauti kila siku ambacho jamii yako itapendezwa nacho au umeng'ang'ania aina moja siku zote? lazima kama mjasiriamali uwe mbunifu kila siku kuhakikisha unapata njia mpya ambazo zitakufanya upanue soko lako.au kazi yako ni kuona mwenzako kafungua boutique na wewe unaenda kufungua boutique.Kila siku jamii inahitaji kitu kipya,hivyo unatakiwa kubuni na kugusa hitaji la jamii.Unatakiwa kuwa mtu wa kugundua vitu vinavyopendwa na watu na ikiwezekana angalia fursa adimu mahali pako na wewe waletee karibu watu walio jirani.Weninge wanasema "transfer of technology".
3.MTU MWENYE KUTAMBUA SEHEMU YA KUPATA USHAURI
Hapa ndio watu wengi wanapata changamoto kwenye biashara,anayehitaji kuwa mjasiriamali au ni mjasiriamali lakini anapoenda kuomba ushauri ni kwa mtu ambae hata hajui ujasiriamali au kafanya kashindwa we unafikiri unaenda kumuomba mtu ushauri aliyeshindwa atakupa jibu gani? atakwambia huwezi matokeo yake na wewe unashindwa.Wengine wanafanya vyovyote pasipo kushauriwa na waliofanikiwa.Jitahidi sana kuwa na mshauri katika shughuli zako au  "role modal ".Unafanya kazi angalia waliofanikiwa katika fani yako kisha waombe ushauri wakusaidie using'ang'ane pekee yako.
4.MTU MWENYE MAHUSIANO NA WATU MBALIMBALI YA KIBIASHARA
Watu wengi hawaamini katika nguvu ya mtandao (power of network) kama kweli we ni mjasiriamali lazima uwe na mahusiano mazuri na watu wengi ya kibiashara lakini ukiangalia wajasiriamali wengi leo hii hawana mahusiano mazuri na watu wengine kibiashara hutaweza kukua kibiashara kama hutaweza jifunza kutoka kwa wangine jifunze kutoka kwa wengine rafiki na hutaweza jifunza kama hutakuwa na mahusiano mazuri na watu wengi kibiasha.Hili ni eneo zuri la kupanua mtandao wa watu.Jitahidi kuwa na mahusiano na wengine acha kujiona wewe ni bora kuliko wengine,angalia mahali palipo na fursa na wekeza.Watu fulani husema kuwa jinsi ulivyo ni fursa.
5.ANAYEPENDA USHINDANI
Siku zote kama mjasiriamali usipende kukwepa ushindani shindana ili bidhaa yako iwe bora,watu wengi hushindwa kufanikiwa katika biashara kwa sababu ya kuogopa ushindani,anashindwa kufanyabiashara fulani kwa sababu washindani wengi,unapokutana na washindani wengi ndio unafahamu mapungufu yako na  unaanza kujirekebisha ili bidhaa au huduma ziwe bora na imara.
6.ASIYIEOGOPA KUSHINDWA NA KUKATA TAMAA
Watu wengi hushindwa katika biashara kwa kuogopa kushindwa anataka kuanzisha kitu lakini cha kwanza anawaza nikifirisika je watu siwatanicheka? acha mawazo mgando rafiki kama kweli we ni mjasiriamali au unataka kuwa mjasiriamali kamwe usiogope kushindwa kwani ninasema mjasriamali ni mtu ambae yuko tayari kushindwa na kujaribu tena (risk taker) matajiri wote unaowaona duniani wamefeli mara nyingi na ndio wakaja kufanikiwa sasa kama unataka kuwa mjasiriamali usiogope kushindwa na wala usikate tamaa ukishindwa unaanza tena na tena na tena hiyo ndio sifa ya mjasiriamali.
7.MTU ANAYETUMIA MUDA WAKE WA ZIADA KUFANYA KITU CHA ZIADA
Siku zote mjasiriamali ni mtu ambaye anauwezo wa kufanya biashara zaidi ya moja yuko tayari kutumia muda wake wa ziada kufanya kitu ambacho japo kimuingizie hata elfu kumi kwa siku mtu ambaye anauwezo wa kutumia muda wake wa ziada kufanya kitu cha ziada huwa anafanikiwa sana maana huwa hapotezi muda.
Acha kuzubaa rafiki maisha yamebadilika unatumiaje muda wako wa ziada wakati vipo vitu ambavyo unaweza fanya na kujiongezea kipato,usisubiri kesho anza leo.tumia muda wako wa ziada kuingiza kipato cha ziada.Kama wewe ni mwajiriwa baada ya kutoka kwenye ajira yako unajishughulisha na nini ? au unakaa na kuzunguka bila utaratibu.Kumbuka hakuna tajiri wa muda wala maskini wa muda wote tuna muda sawa.Dakika,saa,siku,wiki,miezi na miaka inalingana.Tofauti ni jinsi unavyotumia muda na fursa badilika,uzee unakuita.
8.ANAYEITUMIA JAMII INAYOMZUNGUKA KUINGIZA KIPATO
Watu wengi hushindwa kulitambua hili na kujiita wajasiriamali lakini hawajui jinsi ya kuwatumia watu wanaokuzunguka katika kukuingizia kipato,rafiki unawatumiaje watu ambao mmekutana kwenye kikao cha harusi,kikao cha kitchen party au kikao cha familia au kwenye kahawa katika kuitambulisha biashara yako au unajua kazi kupiga umbea tu na kulalamika biashara yako haitoki,unategemea wateja unawapata wapi kama sio hao.Wengine kazini kuna idadi ya watu wengi kwa nini usiwauzie hata maandazi au muda wa maongezi.Unakaa kulalamika pasipo kuchukua hatua .Kumbuka umaskini wa kwanza ni kutoishughulisha akili yako.Anza kupeleka maji ya kunywa kazini kwenu au hata karanga za kukaanga basi hata mayai.Acha woga eti watakucheka badilika ndugu yangu.


   CHUKUA HATUA,MUDA WA KUWA MILIONEA NI LEO,KESHO INA WENYEWE


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUFANIKIWA KI -UCHUMI KWA NJIA YA MUNGU

UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI

SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO