Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 7, 2015

MAZINGIRA YETU

MAZINGIRA YETU Na. AYOUB JL.   MAZINGIRA NI NINI ?    Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai. Vitu vyenye uhai ni pamoja na mimea na wanyama na visivyo na uhai ni pamoja na uhai ni hewa, ardhi na maji. Mazingira yanahusisha pia vitu vyote vinavyosaidia kuendelea kuwepo kwa maisha ya mwanadamu na viumbe wengine. Hivyo basi maisha ya viumbe hai wa kizazi kilichopo na kijacho kinategemea uwepo wa mahusiano mazuri kati ya watu na mazingira. Shughuli za binadamu zimekua kwa kasi sana hususani kilimo,ufugaji,biashara,uchimbaji wa madini,utafutaji wa Nishati na Viwanda.Karibia kila shughuli inaathari chanya au hasi kwa mazingira na viumbe vilivyopo.Ni jambo la muhimu sana kwa kila mmoja kuwa makini katika shughuli ili kuyafanya rafiki kwa kila kiumbe.Mazingira rafiki ni Muhimu sana kwani hutuwezesha kuendelea kuvuna raslimali nyingi zilizofichwa. Hii ni sehemu ya Mazingira ya shule (Nembo ya kuelekea shuleni.) Nitaendelea wiki ijayo