KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
(B.) KARAMA ZA UFUNUO. (i) Neno la hekima.(1 Wakorintho 12:8) Awali ya yote yakupasa kujua nini haswa maana ya hekima.Ninapenda sana tafsiri ya hekima aliyoitoa mfalme Sulemani katika kitabu cha Mithali 1:2-3.Lakini pia mfalme huyu aliitafsiri wakati akimwomba Mungu “Hekima;ni moyo wa adili wa kuhukumu katika haki na ni uwezo wa kupambanua mema na mabaya…” (1 Wafalme 3:9) Hivyo tunaweza kusema kuwa Hekima - Ni moyo mwelevu unaotambua kila jambo kwa mtazamo wa kiungu na neno lake. Au hekima ni kunena au kusema jambo sahihi,kwa watu sahihi na wakati sahihi. Moyo huu wa adili wa kupambanua mema na mabaya katika haki ndio karama yenyewe ya ufunuo. Lakini hatusemi “ karama ya hekima” bali “ karama ya neno la hekima“. Mfano katika biblia; katika Luka 20:19-26,hapo utaona waandishi na wakuu wa makuhani wakijaribu kumkamata Bwana Yesu kwa hila zao,wakimtega kwa kumuuliza kwamba ni halali wao kumpa kodi Kaisari au la? Bwana Yesu akitumia karama ya “neno la hekima ” kuwajibu,na hat