Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 17, 2018

UJENZI WA HOSTELI KITUMBA SEKONDARI

Picha
Harambee ya ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Kitumba inayopatikana katika kata ya Kisesa,Wilaya ya Magu,Mkoa wa Mwanza imefanyika vizuri kutokana na ushiriki wa wadau wa elimu ulivyokuwa kuanzia mwanzo hadi mwisho.Angalia matukio katika picha M geni rasmi akiongozana na wageni wengine kukagua vyumba vya madarasa vitakavyotumika kwa ajili ya kidato cha tano na sita. Mkuu wa shule ya Sekondari Kitumba Mwl,Jailos Msongole akitoa maelezo mafupi kwa mgeni rasmi na viongozi wa kata ya Kisesa. Mgeni rasmi akionesha kwa vitendo namna ya kuchimba msingi jengo la Hosteli linalokadiriwa kubeba wanafunzi 160. Mheshimiwa Diwani wa kata ya Kisesa ,Ndugu MARCO KABADI akishirikiana na mafundi katika ujenzi wa Msingi Mheshimiwa Diwani wa kata ya Kisesa ,Ndugu MARCO KABADI na Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi ambaye pia ni mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Igekemaja wakishirikiana na mafundi katika ujenzi wa Msingi Mgen...