UJENZI WA HOSTELI KITUMBA SEKONDARI

Harambee ya ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Kitumba inayopatikana katika kata ya Kisesa,Wilaya ya Magu,Mkoa wa Mwanza imefanyika vizuri kutokana na ushiriki wa wadau wa elimu ulivyokuwa kuanzia mwanzo hadi mwisho.Angalia matukio katika picha
Mgeni rasmi akiongozana na wageni wengine kukagua vyumba vya madarasa vitakavyotumika kwa ajili ya kidato cha tano na sita.

Mkuu wa shule ya Sekondari Kitumba Mwl,Jailos Msongole akitoa maelezo mafupi kwa mgeni rasmi na viongozi wa kata ya Kisesa.

Mgeni rasmi akionesha kwa vitendo namna ya kuchimba msingi jengo la Hosteli linalokadiriwa kubeba wanafunzi 160.

Mheshimiwa Diwani wa kata ya Kisesa ,Ndugu MARCO KABADI akishirikiana na mafundi katika ujenzi wa Msingi

Mheshimiwa Diwani wa kata ya Kisesa ,Ndugu MARCO KABADI na Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi ambaye pia ni mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Igekemaja wakishirikiana na mafundi katika ujenzi wa Msingi



Mgeni rasmi katika harambee ya ujenzi wa HOSTELI ambaye alimwakilisha Mheshimiwa Desdery Kiswaga (MB) ,Mbunge wa jimbo la Magu (hayupo pichani),Mgeni rasmi ni katibu wa mbunge

Shughuli ya uchangiaji ikiendelea kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Wita Ndugu JAMES NKOYI (SUPER KILEMA),Katikati ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kitumba na kushoto ni Mwenyekiti wa Igekemaja

Afisa Elimu wa Kata ya Kisesa Mwl, JACKSON KADUTU akitoa mchango wake katika harambee hiyo

Mheshimiwa MARCO KABADI akitoa mchango katika harambee hiyo.Mheshimiwa huyu ndiye Mwenyekiti wa Maendeleo katika kata ya Kisesa .

Waheshimiwa madiwani kutoka kata mbalimbali za jimbo la Magu wakitoa mchango wao katika shughuli hiyo ya harambee ya ujenzi wa hosteli Kitumba sekondari.Aliyeshika Mic ni Mheshimiwa HILDA ,Diwani viti maalum.Kata ya KISESA.
ZOEZI LA HARAMBEE LILIFANIKIWA KWA KIWANGO KIZURI
Ili kuhakikisha ujenzi wa Hosteli unafanikiwa wadau mbalimbali walishiriki kikamilifu katika harambee hiyo,wadau hao ni pamoja na WALIMU KUTOKA KITUMBA SEKONDARI (wenyeji),Mondo S/Msingi,Igekemaja S/M, Kitumba S/m,Wita S/M,Kisesa S/M .lakini pia Wawakilishi kutoa kituo cha POLISI kisesa walikuwepo, Umoja wa wamiliki wa malori yanayosomba mchanga walikuwepo ,na marafiki mbalimbali nao pia walishiriki kikamilifu.
SHUGHULI YA UJENZI 
Ujenzi wa Msingi kwa ajili ya Hosteli unaendelea kwa hatua ya kwanza na kamati ya maendeleo ya kata inaendelea kuhakikisha kuwa ujenzi unafanikiwa.
TUTAENDELEA KUWALETEA TAARIFA ZAIDI

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUFANIKIWA KI -UCHUMI KWA NJIA YA MUNGU

UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI

SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO