SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO
SOMO:
NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO
Na
Ayoub Jacob Leo,FPCT KISESA 13.11.2016 hadi 27.11.2016
Nini
maana ya Agano?
Maana: Ni mapatano au makubaliano yanayowekwa baina
ya pande mbili au zaidi ili kutekeleza jambo/mkakati uliopo.Katika Maandiko
kuna maagano mengi yaliyowekwa na Mungu na watu au watumishi wake.
Mfano Agano la Mungu
na Adam Edeni,Mungu na Nuhu,Mungu na Ibrahim,Mungu na Musa,Agano la kanisa la
leo kwa damu ya Yesu( Math 26:28)
MSINGI
WA AGANO LA DAMU YA YESU
Yer 31:31-33,Ebr 8:8
- · Agano hilo linatambulishwa kuwa jipya
- · Halitafanana na agano lolote lile
- · Agano litatia sheria ndani ya mioyo yao.
- · Ndani ya mioyo yao zitaandikwa
- · Agano litawafanya watu wa Mungu kuwa milki yake.
Damu
ya Yesu ina nguvu kupita agano lolote :- ( Math 26:28a)
- · Damu ya Yesu kwa ajili ya ondoleo la dhambi Math 26 :28,1Yoh 1:7-8
“Na kila Kuhani husimama kila siku akifanya
ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi ambazo (Yesu Kristo), alipokwisha
kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele aliketi
mkono wa kuume wa Mungu;tangu hapo akingojea hata adui wawekwe kuwa chini ya
miguu yake. Maana kwa toleo moja AMEWAKAMILISHA HATA MILELE
hao wanaotakaswa. Na Roho Mtakatifu naye atushuhudia; kwa maana, baada ya
kusema, Hili ni agano (Jipya) nitakaloagana nao baada ya siku zile,
anena Bwana, nitatia sheria zangu mioyoni mwao, na katika nia zao
nitaandika; ndipo anenapo, dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka
tena kabisa. Basi ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa
ajili ya dhambi” (Waebrania 10:11 –18)
Mtu anapotubu dhambi zake na kumwamini
Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake; Damu ya Yesu Kristo inafuta
dhambi hizo moyoni mwake, pamoja na kufuta dhambi zilizoandikwa katika vitabu
vya mbinguni kwa ajili ya kumshitaki.
“Na katika Torati Karibu vitu vyote
husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. Basi ilikuwa sharti
nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya
mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo. Kwa
sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono ndio mfano
wa patakatifu halisi; bali aliingia Mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa
Mungu kwa ajili yetu; wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani Mkuu
aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake;kama ni hivyo,
ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini
sasa MARA MOJA TU, katika utimilifu wa nyakati amefunuliwa, AZITANGUE
DHAMBI KWA DHABIHU YA NAFSI YAKE” (Waebrania 9:22-26)
·
2. Damu
ya Yesu katika kufanya upatanisho, ( Ef 2:12-17),2Cor
5:17-20
“Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye
hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa
sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu ni mmoja, na mpatanishi
kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo
Yesu” ambaye alijitoa mwenyewe
kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira
yake” (1Timotheo
2:3-6)
UPATANISHO KATI YA MTU NA MTU
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo
utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao, mkiangalia sana
mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu
lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengine wakatiwa unajisi( kumb 29:18,Mdo 8:22-23)
kwa hilo” (Waebrania
12:14,15).
·
KUACHILIA DAMU YA YESU JUU YA MAFARAKANO
Lakini sasa, katika Kristo
Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa
karibu kwa DAMU YAKE KRISTO. Kwa maana yeye ndiye amani yetu,
aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati KILICHOTUTENGA. Naye akiisha kuuondoa ule UADUI KWA MWILI WAKE; ndiyo sheria ya amri zilizo katika
maagizo; ili afanye hao wawili kuwa MTU MPYA MMOJA ndani ya
nafsi yake; akafanya AMANI. AKAWAPATANISHA WOTE WAWILI NA Mungu katika
mwili mmoja, kwa njia ya MSALABA, AKIISHA KUUFISHA ULE UADUI KWA HUO
MSALABA” (Waefeso
2:12-17).,Is 57:19,52:7,Kol 2:13-14,2Cor 5:17
a)
Damu ya Yesu hubomoa ngome/viambaza.
b)
Damu ya Yesu huondoa uadui/chuki
c)
Damu ya Yesu huleta umoja
d)
Damu ya Yesu huleta umoja
Kumbuka hakuna Amani pasipo mapatano(agano)
20Kwa hiyo
sisi ni mabalozi wa Kristo, kana kwamba Mungu anawasihi kwa kupitia vinywa
vyetu, nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu. 21Kwa
maana Mungu alimfanya Yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi
tupate kufanywa haki ya Mungu katika Yeye ( 2 Cor 5:17
3.
Damu
ya Yesu katika kufanya urejesho ( 2cor 5:18, Col 1:20
Nini maana ya
urejesho ?,
Ni tendo la kurudisha
kitu/hali iyopotea/kuharibika katika hali yake ya awali au asili.Law 26:23,Rum
12:2
HALI/VITU
VINAVYOWEZA KUPOTEA
a) Ufahamu/akili
( uwezo wa fikira)-Isa 59:14,Dan 4:34-38
b) Vitu
/mali .2fal 6: 1-7
c) Afya/uzima-Kila
mara magonjwa au mateso 2fal 4: 38,Uf 21:4
d) Umri/miaka
ya kuishi- Yoeli 2:25
e) Mahusiano
mfano Ndoa,Urafiki, Ibada 2ny 29:24
JINSI
YA KUFANYA UREJESHO
i.
Jikabidhi katika mikono ya Mungu 1Pet
5:6-10
ii.
Kiri mamlaka ya damu ya Yesu.Achilia
damu ya Yesu kwa mamlaka na ujasiri kwa kuwa umekubaliwa. Kwa sababu neno la msalaba kwao
wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya MUNGU. '' 1 Kor
1:18.
Zek 9:11,Isa 61:1
iii.
Nyunyiza damu ya Yesu-Kut 24:28,Chovya
mali ndani ya damu ya Yesu Uf 19:13
· 4.
Damu
ya Yesu katika Kuleta ushindi kwa mwana wa Mungu.
10Hatimaye, mzidi kuwa hodari
katika Bwana na katika uweza wa nguvu Zake. 11Vaeni silaha zote za Mungu mpate
kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12Kwa maana kushindana kwetu si
juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na
mamlaka, juu ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa
roho. 13Kwa hiyo twaeni silaha zote za
Mungu,mpate kuweza kushindana siku ya uovu,na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.(
Efeso 6:10-13)
Ndugu yangu kumbuka
kwamba kila wakati shetani yupo katika vita.Hapendi kuona watu wanafanikiwa kwa
jambo lolote liwe dogo au kubwa.Mfano ukipiga hatua yoyote nzuri yeye anaandaa
mpango wa kukurudisha nyuma.
Aidha unatakiwa kujua
kuwa hatupigani na watu bali falme (
tawala).Hii ina maana kwamba kila mahali shetani ana tawala zake,baadhi ya
maeneo kuna utawala wa mila( mahali pengine watemi,watwala n.k ).Hawa walio wengi wana maagano fulani
katika ulimwengu wa roho,tena wengine wana vyeo vya kutumika wakuu wa ardhi,maji,anga,biashara,mifugo
na uzao.
Mwana wa Mungu
anatakiwa kuvaa silaha za kuweza kushinda.Baadhi ya silaha ni damu ya
Yesu.Ufunuo 12:7-8,11……nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo.Mwana wa Mungu
damu ya Yesu ina nguvu za kukuletea ushindi.
MAMBO YA KUZINGATIA
ILI UPATE USHINDI KWA DAMU YA YESU
a) Mshukuru Mungu kwa kukukomboa
kutoka katika vifungo vya dhambi.1Yoh1:7-8,Ebr 10:11-18,9:20-29.
Kila vita inayokuja
imepimwa unatakiwa kumshukuru Mungu maana kila jaribu lina mlango wa
kutokea.Ukiona kuna vita kumbuka kwamba
vita ni ya Bwana.Hivyo mshukuru Mungu ili ajitokeza na kukuletea ushindi.
Kumbuka katika
shukrani kuna nguvu,hivyo ukikabiliwa na changamoto mshukuru Mungu mwambie vita
iliyopo ndiyo nafasi yako.Hakika Mungu akiinuliwa yeye hudhihirika.
b)
Jivike
silaha ya damu ya Yesu Uf 12:11, Nyunyiza damu ya
Yesu,jichovye ndani ya damu ya mwanakondoo.
c)
Achilia
damu ya Yesu juu ya vita kwa kuisemesha vita uliyonayo.
Kumbuka ndani mwako
kuna nguvu,nguvu hizo zikiachiliwa shetani hana lake maana umekubalika.Usijidharau
tamka ushindi,tangaza vita,simamisha dhoruba,n.k
MIFANO YA WATU WALIOSEMESHA VITA/CHANGAMOTO AU
UPINZANI
i.
Bwana Yesu alisemesha dhoruba na upepo
( Mark 4:35-41,Lk 8:22-23,Yesu aliulaani
mtini ( Mark 11:12-22),Yesu alimsemesha Lazaro aliyekufa ( Yoh 11 :1- )
ii.
Daudi alimsemesha Goliathi (1Sam
17:45)
iii.
Ezekieli alizungumza na mifupa mikavu
( Eze 37 :1- ).
§
Jiulize upepo na dhoruba yako
utausemesha nini ? Muda wa kutuliza upepo umefika,usizame ukemee kwani Bwana wa
Vita yupo.Tumia damu yake hakika utauona mkono wa Bwana.
§
Goliath wako ni nani ? Mwendee kwa
damu ya Yesu uone atavyokuwa mikononi mwako ?
§ Mifupo
mikavu yako nini ? Iamuru ijikusanye,itabirie na kurejesha uzima.
MWISHO
Hakuna
uchawi wala mapepo vinavyosimama mbele ya damu ya Yesu.Damu ya Yesu ni kiboko
juu ya vita.Wana wa Israel walitumia damu ya mwanakondoo kama pigo la
mwisho.Hakika Mungu aliwapigania.Wewe ni zaidi ya Musa,Daudi na Ezekieli.
Damu
ya Yesu ni msingi wa agano jipya ( Lk 22:20 ).Tumia damu ya Yesu hakika
Utashinda.
Mungu
Akubariki sana.
Niandikie
Baruapepe
:ayoubleo@yahoo.com au +255785 645 177 au +255755 035 722
Blog
: www.nsanacz.blogspot.com
Maoni