WOKOVU NI KUWA NA USHIRIKA
SEHEMU YA KWANZA KWELI KUU: Maisha yetu ya wokovu hayana maana kabisa kama hatutakuwa na ushirika na Baba, Mwana, Roho Mtakatifu, na sisi kwa sisi kama kanisa la Kristo ambalo ni mwili wa Kristo. Mstari wa Msingi (Kukumbuka): 1 Wakorintho 1:9 Mungu ni mwamainifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe , Yesu Kristo Bwana wetu. Ndugu mpendwa, leo nitaanza mfululizo wa somo hili ambalo litakuwezesha wewe kueneza mizizi yako ya imani katika Yesu Kristo Bwana wetu ambaye ni Mungu Mwana, na katika Mungu Roho Mtakatifu na katika Mungu Baba kwa kujua nini maana ya kuwa na ushirika, namna ya kuwa na ushirikana jinsi ya kuendelea kuwa na ushirika Mungu (Baba, Mwana na Roho Matakatifu). Karibu sana. UTANGULIZI: Katika utangulizi wetu, tutaangalia zaidi maana ya maneno makuu matatu ambayo yatajitokeza katika somo letu hili na miongoni mwa maneno hayo mawili yamejitokeza katika kichwa cha somo letu. Hivyo ni lazima tuyaangalie ili tuwe na