UJASIRIAMALI
HII NDIO MAANA HALISI YA KUENDESHA BIASHARA KISOMI UJASIRIAMALI Kwanza kabla hatujaenda mbali tambua yafuatayo: Sio lazima mwenye biashara awe msomi ili biashara iendeshwe kisomi Sio kila msomi anaweza endesha biashara kisomi. Kuendesha biashara kisomi sio tuu kufanikisha biashara ipate faida. Kuendesha biashara kisomi ni zaidi ya elimu ya darasani ya biashara Endelea kusoma ufahamu vizuri nini cha kufanya ili biashara iendeshwe kisomi. Ipo hivi, kuendesha biashara kisomi ni pale unapoamini na kutenda mambo yahusuyo biashara yako kwa imani na mtazamo kuwa biashara yako ipo sio tuu kwa sababu ya kupata faida ili wewe ujinufaishe bali huko kupata faida ni sehemu tuu ya malipo yako ya kukufanya uihudumie biashara yako ifikie kile ambacho kweli haswa ndio lengo lake. Hivyo kwa mtazamo wa kisomi ni kuwa pamoja na kwamba wewe unajiita bosi, kiukweli wewe ni mtumishi tuu wa hiyo biashara. Itazame biashara yako kama kiumbe ambacho kimekwisha zaliwa, ...