NAFASI YAKO NI MUHIMU SANA KATIKA KUUJENGA MWILI WA KRISTO
Na: Patrick Sanga Biblia katika 1 Wakorinto 12:11-14,18 imeandikwa ‘ Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, AKIMGAWIA kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni VINGI . Bali Mungu AMEVITIA viungo kila kimoja katika mwili kama ALIVYOTAKA’ (1Wakorintho 12:1-31, Warumi 12:4-8) Kanisa ni mwili wa Kristo wenye viungo vingi, naam, kila kiungo kinao wajibu (unique) wa kufanya ili kuujenga mwili wa Kristo na kuusaidia kufikia malengo yake ipasavyo. Naam ili kutekeleza wajibu huo , kila kiungo kimepewa uwezo na kimewekewa namna (mipaka) yake ya utendaji kazi ambayo matokeo yake yanaathari kwa mwili mzima. Ku...