NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUTUMIA NAFASI ZAKE KUBADILISHA MAISHA YA NDOA YAKE (Sehemu ya 4a)
Na: Patrick Sanga Nafasi ya tano – Mwanamke kama Mjenzi Katika sehemu ya tatu tuliangalia nafasi ya nne ambayo ni Mwanamke kama Mlinzi. Ili kuisoma endapo hukusoma bonyeza link hii https://nsanacz.blogspot.com/2018/05/namna-mwanamke-anavyoweza-kutumia_6.html. Fuatana nami sasa tuendelee na mfululizo wa somo hili. Biblia katika kitabu cha Mithali 14:1 inasema ‘ Kila mwanamke aliye na hekima huijenga nyumba yake: Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe’. Tafsiri ya neno nyumba ni familia, naam na familia inajumuisha baba, mama na watoto endapo mmejaliwa. Hata hivyo katika hali ya kawaida watoto watalelewa katika msingi mzuri endapo ndoa husika imetengamaa. Ifahamike kwamba hili andiko si la wanandoa peke yao, bali hata wanawake wasio wanandoa wenye familia kama wajane, walezi nk linawahusu. Kwa kuwa hapa tunazungumzia habari za wanandoa nitalifafanua zaidi kutoka kwenye kona hiyo. Pia neno nyumba limetumika ili kutupatia urahisi wa kuelewa namna nyumba