Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 13, 2018

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

SEHEMU YA PILI Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu.Karibuni tuendelee kujifunza somo letu tuliloanza jana. A. KARAMA ZA KUSEMA. (i) Karama za lugha ~Karama za lugha nazo zimegawanywa katika sehemu kuu mbili; Lugha katika kulijenga kanisa, kuhutubu. Udhihirisho wa Roho wa namna hii hujulikana pia “lugha ya ibada” Hiki ni kipindi cha kuwajenga waamini,kuwatia moyo,kuwatia nguvu kwa maneno yenye kueleweka vizuri (1 Wakorintho 14:3). Sifa mojawapo ya karama hii ni kwamba,ili ifanye kazi inategemea hadhara ya watu walioandaliwa kupokea ujumbe. Kuhutubu,kunamfanya yeye aliye mjinga kupata nafasi ya kuelimika kwa neno la Mungu. Lugha katika kunena(kunena kwa lugha mpya) Uhidhihirisho huu ni wa aina ya pili,ni udhihirisho wa Roho Mtakatifu katika kunena kwa lugha.Kunena kwa lugha ni kutamka maneno katika Roho yasiyopangwa kutamkika,na yasiyoeleweka masikioni mwa watu wa kawaida hata shetani haelewi kabisa !isipokuwa roho ya mtu hunena mambo ya siri na Roho wa Mungu~ Matendo 2:4. ...