KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
SEHEMU YA PILI
Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu.Karibuni tuendelee kujifunza somo letu tuliloanza jana.
Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu.Karibuni tuendelee kujifunza somo letu tuliloanza jana.
A.KARAMA ZA KUSEMA.
(i)
Karama za lugha
~Karama
za lugha nazo zimegawanywa katika sehemu kuu mbili;
Lugha katika kulijenga kanisa, kuhutubu.
Udhihirisho
wa Roho wa namna hii hujulikana pia “lugha ya ibada” Hiki ni kipindi cha
kuwajenga waamini,kuwatia moyo,kuwatia nguvu kwa maneno yenye kueleweka vizuri
(1 Wakorintho 14:3). Sifa mojawapo ya karama hii ni kwamba,ili ifanye kazi
inategemea hadhara ya watu walioandaliwa kupokea ujumbe. Kuhutubu,kunamfanya
yeye aliye mjinga kupata nafasi ya kuelimika kwa neno la Mungu.
Lugha katika kunena(kunena kwa lugha mpya)
Uhidhihirisho
huu ni wa aina ya pili,ni udhihirisho wa Roho Mtakatifu katika kunena kwa
lugha.Kunena kwa lugha ni kutamka maneno katika Roho yasiyopangwa kutamkika,na
yasiyoeleweka masikioni mwa watu wa kawaida hata shetani haelewi kabisa !isipokuwa
roho ya mtu hunena mambo ya siri na Roho wa Mungu~ Matendo 2:4.
Kumbuka;kupo
kunena kwa lugha mpya baada ya Roho mtakatifu kushuka (Matendo 19:6,Matendo
2:4) Lakini pia kupo kunena kwa lugha kwa namna ya karama rasmi. Kile
ninachozungumzia hapa ni unenaji wa lugha katika karama.
Mtu
mwenye karama hii,muda wote aweza kunena kama apendavyo Roho mtakatifu. Haitaji
kuanza kutafuta uwepo kwamba aabudu kwa kipindi kirefu ndipo anene,bali anaweza
akaabudu kidogo tu kisha akanena,au akawa akinena katika maombi.
(ii) Kutafsiri lugha.
Karama
hii inategemea malighafi ya udhihirisho wa Roho mtakatifu wa kunena kwa lugha.
Maana ili utafsiri,unahitaji lugha iliyonenwa lakini haikueleweka,au haieleweki
katika hadhara husika,ndipo sasa hitaji la kufasiri hujitokeza. Karama hii
inawezeshwa na Roho mwenyewe,kwa sababu hakuna awezaye kufasiri lugha kwa
kutumia akili zake mwenyewe pasipo kuongozwa na Roho Mtakatifu. Wala hakuna
ujanja ujanja unaohitajika katika kufasiri lugha pale lugha mpya itolewayo,ni
kwa msaada wa Roho mtakatifu tu.
~Je karama hizi mbili yaani,karama ya kunena katika roho,na
kufasiri zinatumikaje?
JIBU;Yapo
mazingira mawili ambapo yakupasa kuyajua kwamba ni kipindi gani haswa cha
kufasiri lugha na kipindi gani haswa si cha kufasiri lugha pindi mmoja
anenapo(na huu ni ufunuo)
Hivyo
basi ili tuweze kuyajua haya yote hatuna budi kujua aina za unenaji wa
lugha,zipo mbili nazo ni;
(a)
Mtu akizungumza na MUNGU wake kwa njia ya lugha.
(b)
MUNGU akizungumza na watu wake kwa njia ya lugha.
Tazama,Mtu
akizungumza na MUNGU wake kwa njia ya lugha,haitaji mtafsiri maana mtu huyu
hunena mambo ya siri katika roho yake,wala hasemi na watu~ 1 Wakorintho 14:2.
Lakini,Mungu anaweza kuzungumza na watu wake kwa njia ya lugha akimtumia
mtumishi wake,hapa ndipo pana hitaji mwenye karama ya kutafsiri lugha aingie
kazini kwa msaada wa Roho mtakatifu ili kuwezesha ujumbe wa Mungu ueleweke kwa
watu wote ~ 1 Wakorintho 14:13
(iii)
Unabii.
1
Wakorintho 12:10
Hapo
zamani mtu mwenye karama hii alikuwa akijulikana kuwa ni “ mwonaji” Imeandikwa“
(Hapo zamani katika Israeli, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema
hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani
aliitwa Mwonaji.) “1 samweli 9:
Hivyo
basi,karama hii inampa mtu kuona mambo yajayo katika ulimwengu wa roho kwa
kadri Roho mtakatifu anavyojifunua kwake. Karama hii ni zawadi nzuri ya kupata
taharifa za matukio yajayo,ili uweze kuyashughulikia sasa. Hata kanisa,haliwezi
kwenda bila nabii,yeye aonaye mambo ya sirini. Ikumbukwe ya kwamba unabii
hautolewi kwa sababu ya mapenzi ya mtu fulani bali kwa sababu ya mapenzi ya
Roho mtakatifu;
“ Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna
unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana
unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena
yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2 Petro 1:20-21
Maoni