Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 12, 2018

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

Maana ya Neno Karama za Roho Mtakatifu Karama za Roho Mtakatifu ni zawadi ambazo Roho Mtakatifu huwapa watu (wakristo wamwabuduo sana) kwa neema na ndiye huamua ampe nani, zawadi gani bila kujali anapenda au hapendi Karama ni utendaji kazi wa Roho mtakatifu ndani ya mwamini aliyeokoka. Karama haipatikani kwa kusomea darasani,kwa maana Yeye atoaye kila karama ni Roho mtakatifu.( 1 Wakorintho 12:8). Bali mwenye karama anaweza kwenda darasani kwa lengo la kuikuza karama yake kimaarifa ili atakapokua akiitumia aweze kuwa na wigo mkubwa wa matumizi ya karama hiyo. Jambo hili leo limekuwa ni shida kubwa linalosumbua kanisa la leo,maana wapo watu wanaohudumu kiroho huko makanisani kwa sababu walienda kusomea karama zao kisha baada ya mafunzo wengine wakajiita au kuitwa ni wachungaji,mashemasi,mitume,manabii pasipo Roho mtakatifu kuhusika kuwapa nyadhifa hizo. Mfano; Uchungaji hausomewi bali hutolewa na Roho mtakatifu,kisha baada ya kupewa huduma hiyo mtu aweza kwenda shule kupat...