KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU



Maana ya Neno Karama za Roho Mtakatifu
Karama za Roho Mtakatifu ni zawadi ambazo Roho Mtakatifu huwapa watu (wakristo
wamwabuduo sana) kwa neema na ndiye huamua ampe nani, zawadi gani bila kujali anapenda au hapendi Karama ni utendaji kazi wa Roho mtakatifu ndani ya mwamini aliyeokoka.
Karama haipatikani kwa kusomea darasani,kwa maana Yeye atoaye kila karama ni Roho mtakatifu.( 1 Wakorintho 12:8). Bali mwenye karama anaweza kwenda darasani kwa lengo la kuikuza karama yake kimaarifa ili atakapokua akiitumia aweze kuwa na wigo mkubwa wa matumizi ya karama hiyo.
Jambo hili leo limekuwa ni shida kubwa linalosumbua kanisa la leo,maana wapo watu wanaohudumu kiroho huko makanisani kwa sababu walienda kusomea karama zao kisha baada ya mafunzo wengine wakajiita au kuitwa ni wachungaji,mashemasi,mitume,manabii pasipo Roho mtakatifu kuhusika kuwapa nyadhifa hizo. Mfano; Uchungaji hausomewi bali hutolewa na Roho mtakatifu,kisha baada ya kupewa huduma hiyo mtu aweza kwenda shule kupata mwanga zaidi juu ya uchungaji hali kadhalika na karama nyingine zozote zile.
Hatuwezi kuwa wachungaji,mitume,walimu kwa vyeti tu kwa sababu kinachohudumu kanisani sio cheti bali kile kinachohudumu ni roho ikiongozwa na Roho mtakatifu. Kama ndio hivyo,basi ni dhahiri kabisa Roho mtakatifu ndie agawaye karama tofauti tofauti kama apendavyo Yeye.
AINA ZA KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU.
Karama hizi ni miongoni mwa karama ambazo biblia imeziorodhesha katika 1 Wakorintho 12:8-10. Ili kuelewa vizuri na kupata mpangilio mzuri,basi nimekupangia karama hizi katika makundi makuu matatu
A.Karama za kusema.
(i) Lugha.
(ii) Kutafsiri lugha.
(iii)Unabii.
B .Karama za Ufunuo.
(i) Neno la hekima.
(ii)Neno la maarifa.
(iii)Kupambanua Roho
C. Karama za uwezo.
(i) Karama ya imani.
(ii)Karama za uponyaji.
(iii)Matendo ya miujiza.
Roho mtakatifu ametoa ufunuo mbali mbali kwa kufaidiana kama apendavyo Yeye 1 Wakorintho 12:8.
Itaendelea........

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUFANIKIWA KI -UCHUMI KWA NJIA YA MUNGU

UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI

SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO