KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
(B.) KARAMA ZA UFUNUO.
(i)
Neno la hekima.(1 Wakorintho 12:8)
Awali
ya yote yakupasa kujua nini haswa maana ya hekima.Ninapenda sana tafsiri ya
hekima aliyoitoa mfalme Sulemani katika kitabu cha Mithali 1:2-3.Lakini pia
mfalme huyu aliitafsiri wakati akimwomba Mungu “Hekima;ni moyo wa adili wa
kuhukumu katika haki na ni uwezo wa kupambanua mema na mabaya…” (1 Wafalme 3:9)
Hivyo
tunaweza kusema kuwa
Hekima
- Ni moyo mwelevu unaotambua kila jambo kwa mtazamo wa kiungu na neno lake. Au
hekima ni kunena au kusema jambo sahihi,kwa watu sahihi na wakati sahihi.
Moyo
huu wa adili wa kupambanua mema na mabaya katika haki ndio karama yenyewe ya
ufunuo. Lakini hatusemi “ karama ya hekima” bali “ karama ya neno la hekima“.
Mfano katika biblia; katika Luka 20:19-26,hapo utaona waandishi na wakuu wa
makuhani wakijaribu kumkamata Bwana Yesu kwa hila zao,wakimtega kwa kumuuliza
kwamba ni halali wao kumpa kodi Kaisari au la?
Bwana
Yesu akitumia karama ya “neno la hekima ” kuwajibu,na hatimae wale wenye hila
walistaajabu na kunyamaa.Mifano mingine katika biblia;Soma Yoh. 8:3-11,Matendo
6:1-5,Matendo 15:25-29,Matendo 27:23-24. N.K
Utendaji kazi wa
karama hii ya neno la hekima;
~Huwezesha
kufanya maamuzi kwa usahihi na kwa haki.
Mtu
mwenye karama hii,anaweza akawaamua na kuwaongoza watu wake kihekima. Kanisa
linahitaji karama hii,ili pasiwepo na upendeleo wowote ule.
(ii)
Neno la maarifa. 1 Wakorintho 12:8
Neno
la maarifa ni mojawapo ya karama ya ufunuo wa Roho mtakatifu wa kujua mambo
mbali mbali katika uhalisia wake. Pia, ni sehemu ndogo ya maarifa ya Mungu
ndani ya mwenye karama hii. Tuangalie mifano michache kuhusu karama hii ndani
ya Bwana Yesu.
Yesu
alifahamu kweli iliyopo ndani ya Nathanaeli kabla hata hajakutana
naye,imeandikwa;“Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari
zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.Nathanaeli
akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita,
ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona.” Yoh.1:47-48.
Kupitia
andiko hilo,tunaona ya kwamba Yesu akiwa na neno la maarifa kuhusu Nathanaeli
wa kana ya Galilaya. Pia waweza kusoma Yoh.4:18-20,(Yesu akiwa na maarifa
kamili juu ya mwanamke msamaria kwa kujua yote aliyokuwa nayo kabla ya kukutana
naye.),
Soma
pia habari za Anania na Safira mkewe, Matendo 5:3,jinsi karama ya neno la
maarifa ilivyofanya kazi ndani ya Petro,kiasi cha kujua siri yote aliyoifanya
Anania na Safira mkewe katika mauzo ya kiwanja.
Kumbuka;neno
la maarifa ni tofauti kabisa na maarifa ya mwanadamu ya asili. Hii ni karama yaani
ni utendaji kazi wa Roho Mtakatifu katika maarifa yake. Hivyo maarifa haya ni
tofauti na maarifa ya kusomea,tena ni tofauti na maarifa ya asili bali ni Roho
mwenyewe.
Utendaji kazi wa karama
hii;
(a)
Kufichua dhambi. ~Matendo 5:1-3
~Kupitia
karama ya neno la maarifa,dhambi hufichuliwa. Maovu pia hufichuliwa kwa sababu
mwenye karama hii amepewa kuona kimaarifa.
(b)
Kuwa na wigo mpana wa kutatua tatizo.
Karama
hii,inampa wigo mkubwa muhusika wa kutatua tatizo kwa maana anakuwa na maarifa
ya ki-Mungu juu ya tatizo. Kuna kipindi fulani ambacho unahitaji neno la
maarifa ili uweze kushughulikia tatizo la kiroho kiundani haswa.
(c)
Karama hii inakuwezesha kushauri,kuomba,au kuombea
wengine kwamapana.
~Tazama,
mtu akijawa na karama ya neno la maarifa huweza kujua jinsi impasavyo ya kutoa
ushauri mzuri kwa mtu mwenye kuhitaji kushauriwa,kwa maana wakati mshauriwa
anaeleza hapo mwenye karama anaweza kujua jambo sahihi la kumshauri na lipi
asimshauri kwa maana atakuwa akiona na kuyapima maneno yote ya mshauriwa hata
kama hajamaliza kumsimulia. Karama hii ya neno la maarifa itamuwezesha mtumishi
ajue namna gani ya kumuombea pia.
(iii)Kupambanua Roho.
~Hii
ni mojawapo ya karama ya ufunuo yenye umuhimu sana katika kanisa la leo.
Kupamanua roho ni kipawa cha kuzipima roho ,maana nyakati hizi za mwisho zipo
roho zidanganyazo(1 Timotheo 4:1). Pia kupambanua roho,ni kipawa cha kuhakiki
roho,kuzinyambua nyambua roho. Uwezo huu ni wa umuhimu sana,maana kwa njia ya
karama hii ndiposa mtu aweza kutofautisha roho za mashetani na Roho wa Bwana.
Ufanyaji
kazi wa karama hii ni kama ifuatavyo;
(a)Kuzipima roho za watu mbali
mbali.
Roho
za watu mbali mbali zenye kunena habari za Yesu,lazima zipimwe kwa kupitia
karama hii. Maana si wote wananena sahihi,bali wengine wengi wamejawa na tamaa
zao na wala si watu wa Mungu kwa kazi wazifanyazo. Mfano tuangalie hapa;
“Ikawa
tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa
uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata
Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye
juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo
akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo,
mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.” Matendo 16:16-18
Kijakazi
huyu alikuwa na pepo wa uaguzi,ambapo pepo huyu ni roho ya shetani. Ingawa kile
alichokisema kilikuwa sawa maana aliwasemea akina Paulo kwamba ni watumishi wa
Mungu aliye hai,wenye kuhubiri njia ya wokovu lakini roho hiyo iliyoyasema
ilikuwa ni roho ya pepo,ndio maana Paulo aliweza kumkemea na kumtoa. Paulo
aliweza kupambanua roho ndani ya yule kijakazi.
Sasa
waweza fikiria kwamba kama Paulo asingelikuwa na karama hii,wewe unafikirije?
Je ni kweli angeweza kumkemea? Ukweli ni kwamba angemuacha yule kijakazi
aendelee kusema maneno yale,tena angekubali kabisa kwamba waandamane wote
katika kuhiubiri injili. Na laiti kama angeambatana naye pasipo kuijua roho
itendayo kazi ndani ya yule kijakazi,basi ni dhahiri huduma ya Paulo
ingemsumbua baadae.
Na
hili ndilo linaloendelea hata leo katika makanisa yetu. Maana wapo watu ni
wapunga pepo hali wakijifanya ni watumishi wa kweli. Na kwa sababu ya kuikosa
karama hii,tumejikuta tukiwakumbatia watu hao na kuwapa nafasi mbali mbali za
kiutumishi~ sasa mwishoe hatujui ipi miujiza ya kweli,na ipi ni ya uongo kwa
sababu ya kushindwa kupambanua roho.
(b)Kuzipima roho za watumishi wa
Mungu.
~Wapo
watumishi wa Mungu wa ukweli ambao hufanya kazi ya Mungu kihusahihi kabisa.
Lakini baadhi yao wanaweza wakatumiwa na roho za kishetani pasipo wao kujijua
ya kwamba wanatumika kipindi hicho,inawezekana katika kipindi hicho cha
kutumika na roho mbaya wao wakawa wamejisahau,labda waliruhusu
hasira,uchungu,magomvi,hofu.N.K,
Hivyo
hayo yote yakawa ni mlango wa shetani,kisha roho ya pepo ikaingia ndani yao.
Hapo sasa roho itakayotenda kazi kipindi hicho siyo Roho mtakatifu bali ni roho
mtakafujo roho ya shetani hali mtumishi huyo ni wa Mungu. Tumeona mara nyingi
maneno mabaya yakiwatoka watumishi wa Mungu,mpaka tunashangaa kwamba ni kweli
mchungaji huyu huyu tunayemfahamu?!! Au mwingine,?!!
Mfano
tuangalie hapa;
“
Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda
Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na
waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.Petro akamchukua, akaanza
kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.Akageuka, akamwambia Petro,
Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu,
bali ya wanadamu.” Mathayo 16:21-23
Petro
alikuwa si shetani,bali ni mtumishi wa Mungu kweli kweli. Lakini katika andiko
hili tunaona Yesu akamwambia “Nenda nyuma yangu,shetani;u kikwazo kwangu…” Yesu
aliweza kutambua ya kwamba roho iliyokuwa ikitenda kazi saa ile haikuwa roho ya
Petro bali ilikuwa ni roho ya shetani.
Si
Roho yule wa Bwana kwa kipindi kile bali ni roho ya shetani ndio ilikuwa
ikinena ndani ya Petro,Yesu akaipambanua kisha akatambua. Ikumbukwe kwamba Yesu
alipoanza kuwaonya juu ya mateso yake,huyu Petro aliingiwa na hofu,kumbuka
;hofu ni mlango wa shetani,hivyo Petro aliweza kufungua mlango na roho mbaya
ikamuingia ndiposa akaanza kumkemea Yesu kwa kuyakataa yale ambayo Yesu alikuwa
akiwaambia.
Katika eneo hilo,si rahisi kujua roho ya shetani na Roho wa Mungu ikiwa
kama huna karama hii ya kupambanua roho. Karama hii ikikosekana,wengi hunaswa
katika roho za miujiza ya shetani wakidhani ni ya Mungu….
MUNGU AKUBARIKI SANA MWANA WA MUNGU
Mshirikishe na rafiki yako jambo
hili
Amina !
Maoni