ASILI YA ISRAEL
Hapo
mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi. Akamuumba mtu akamweka katika nchi hiyo,
akakubaliana naye kuwa ailinde, aitunze, tena aweze kuimiliki. Mtu huyo
akakiuka Makubaliano yake na Mungu ambayo walikubaliana.
Mtu
huyo alifukuzwa na kuondolewa katika nchi ile aliyokuwa amewekwa ndani yake ili
aweze kuitunza.
Baada
ya Mwaka elfu moja ya mtu huyo kufukuzwa kutoka katika nchi ile Mungu
alimtafuta mtu miongoni mwa wanadamu atakaye mtumia kutimiza kusudi lake la
moyoni mwake.
Katika
mpango huo akampata mtu ambaye aliitwa Abramu, ambaye baadaye alimbadlisha
kutoka Abramu maana yake Kuhani wa Mungu akawa Abrahamu, baba wa Mataifa,
Kuhani wa Mungu aliye hai. Ilikuwa imepita miaka elfu moja mpango wa kwanza
uliposhindwa wa kumpata mtu huyo.
Abrahamu
alipewa masharti ambayo akiyakubali ndipo akubaliwe kutumiwa na Mungu.
Tunasoma katika kitabu cha Mwanzo Sura ya Mwanzo 12: 1-3.
BWANA
akamwambia Abrahamu, Toka wewe katika nchi yako na jamaa zako, na
nyumba ya baba yako uende mpaka nchi nitakayo kuonesha, nami nitakufanya wewe
kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako nawe uwe Baraka, Nami
nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani, na katika wewe jamaa zote
za dunia watabarikiwa.
Mungu
alimwaahidi huyo mtu mambo makuu yafuatayo, akikubali kufanya kama
anavyomwagiza Kwanza: Atampa nchi, Pili: Atamfanya kuwa Taifa kubwa, Tatu:
Atamfanya kuwa Baraka , Nne: Jamaa zote za dunia watabarikiwa kupitia yeye,
Tano: Atawabariki wambarikio na kumlaani Yule Atakaye mlaani.
Mtu
huyo alikubali masharti hayo yote ambayo Mungu alimpa Mwanzo 17:6-7.
Nitakufanya
uwe na Uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa taifa, na wafalme watatoka
kwako. Agano langu nitalifanya kuwa imara kati ya mimi na wewe, na Uzao wako
baada yako na vizazi vyao kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na
kwa Uzao wako baada yako.
Nami
nitakupa wewe na Uzao wako baada ya yako nchi hii unayo ikaa ugeni, nchi yote
ya kaanani, kuwa milki ya milele, nami nitakuwa Mungu wao.
Mungu
alimpa Abrahamu nchi ya Kaanani kuwa Milki yake, yeye na Uzao wake. Kaanani
lilikuwa ni jina la nchi ambayo leo hii inaitwa Israel, kwa sasa.
Mjukuu
wa Abrahamu ambaye jina lake lina maana ya mtu mdanganyaji, mtu aliye tumia
mabavu kupata anacho kitaka, mtu ambaye ni mavumbi. Kwa kuwa Mungu
alitaka kubadilisha jina la Yakobo, kumpa jina jipya, mpango wake Mungu
ukamleta Yakobo kukutana na Malaika ambaye walishikana mieleka usiku kucha.
Mwanzo 32:24-28
Yakobo
akakaa peke yake, na mtu mmoja akashindana naye mweleka hadi alfajiri. Naye
alipoona ya kuwa hamshindi akamgusa panapo paja lake, akateguka uvungu wa paja
lake. Yakobo alipokuwa akishindana naye akasema Niache, niende maana
kumepambazuka. Akasema sikuachi usipo nibariki. Akamuhuliza jina lako
nani? Akasema Yakobo. Akamwambia jina lako hutaitwa tena Yakobo ila
Israeli maana umeshindana na Mungu, na watu nawe ukawashinda.
Kuanzia
hapo Yakobo akaitwa Israeli, Jina Israeli linahusu mtu aliyeitwa hapo mwanzo
Yakobo mwana wa Isaka, mjukuu wa Abrahamu.
Nchi
ya Israeli ilipata jina kutoka kwa mtu huyo ambaye ni Yakobo.
Asili
ya Taifa la Israel
Tuangalie
mwanzo wa taifa hili la Israeli. Yakobo alizaa watoto kumi na wawili ambao
wanaunda kabila kumi na mbili za Israeli, mtoto mmoja wa Yakobo aitwae Yusufu,
alikuwa mtoto wa pekee katikati ya ndugu zake, walimuita muota ndoto. Kwa
kuwa hizo ndoto zake alipozisimulia kwa kaka zake zikawafanya wamchukie. Siku
moja aliota ndoto kuwa ndugu zake wangeishi maisha ya kumsujudia.
Kwa
hiyo ndugu zake walipokuwa malishoni Yusufu akawaletea chakula, wao wakaamua
kumuuza kwa wafanya biashara ambao nao wakamuuza kwa mtu mmoja potifa aliye
kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Misri.
Huyo
Yusufu aliishi kama mtumwa wa mtu huyo, alipewa kuangalia mali zote za
Yule bwana. Mashamba ya mtu huyo pamoja na mifugo yake ikaongezeka
maradufu kwa sababu yake. Lakini mwanamke wa Yule bwana alimtamani Yusufu
akataka kulala naye na kufanya uzinzi lakini Yusufu akakataa maana alikuwa mtu
mwaminifu kwa Mungu. Mwishowe Yule mwanamke akamsingizia kwa mumewe kuwa mtumwa
wako alitaka kunibaka nikakataa.
Huyo
bwana Mmisri akamtupa Yusufu jela akafungwa kifungo kisichojulikana muda gani
angeliweza kufunguliwa.
Humo
gerezani Yusufu aliendelea kuishi Maisha ya Uadilifu na Uaminifu kwa Mungu
wake. Siku moja mfalme Farao wa Misri akaota ndoto iliyoshindikana kutafsiriwa.
Akaitwa Yusufu, aliyekuwa mfungwa akatoa tafsiri yake ambayo ilikuwa ni ya
muhimu sana.
Mfalme
Farao akaamuru Yusufu afanywe Waziri Mkuu wa Misri ambaye alisaidia nchi hiyo
kukusanya chakula na kukiweka akiba kwa miaka ya njaa itakayo kuja baadaye.
Misri
ilikuwa na miaka saba ya Mavuno makubwa sana. Yusufu akasimamia Ukusanyaji wa
hicho chakula na kukihifadhi katika maghala kwa nchi nzima.
Wakati
Misri inashibe ya chakula huko nchi ya Kaanani kulikuwa na njaa kali , Misri
ilikuwa na miaka saba ya Mavuno makubwa sana. Yusufu akasimamia Ukusanyaji wa
hicho chakula na kukihifadhi katika maghala kwa nchi nzima.
Wakati
Misri inashibe ya chakula huko nchi ya Kaanani kulikuwa na njaa kali hata Mzee
Yakobo akawatuma kuja Misri kununua chakula. Mwanzo 42:1-3
Basi
Yakobo akaona ya kuwa kuna nafaka katika Misri, Yakobo akawaambia wanawe kwa
nini mnatazama? Akasema, angalia nimesikia ya kuwa nafaka iko Misri,
Shukeni mkatununulie chakula tupate kuishi wala tusife.
Basi
ndugu kumi wa Yusufu, wakashuka Misri ili wanunue nafaka. Walipofika Misri
walikutana na Yusufu ambaye alikuwa mtu mkubwa lakini hawakumtambua kama ndugu
yao.
Yusufu
aliamuru wauziwe chakula walichotaka. Njaa ilikuwa nzito huko Kaanani, mwisho
wao walirudi Misri kununua nafaka kwa mara nyingi, mwishowe Yusufu
alijitambulisha kwao kuwa mimi ni Yusufu mliye niuza huku Misri Mwanzo 45:3-4
Yusufu
akawaambia ndugu zake mimi ndimi Yusufu, baba angali hai? Wala ndugu zake
hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele zake. Yusufu akawaambia
ndugu zake karibuni kwangu, basi wakakaribia. Akasema mimi ni Yusufu, ndugu
yenu ambaye mliniuza Misri. Yusufu aliwasamehe hakujilipiza.
Baadae
Mzee Yakobo Israeli alihamia Misri na watu wa nyumba yake wapatao sabini.
Yakobo akaungana na Mwanawe Yusufu wakakaa Misri.
Baada
ya miaka 430 hao watu 70 walioingia nchini Misri waliongezeka hadi kufikia
jumla ya watu 25,000,000 wakawa tishio katika nchi ya Misri. Tunasoma Kutoka
1:7
Na
wana wa Israeli walikuwa na Uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa
wengi, nao wakaendelea kuongezeka nguvu na ile nchi ilikuwa imejawa na wao.
Kwa
sababu hiyo Wamisri walipoona ya Yusufu amekufa ambaye alikuwa ndugu yao, tena
kiongozi katika serikali. Wamisri waliwachukia Waisraeli na kuwa tesa sana.
Lakini walivyo watesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi sana.
Mwisho
wa mateso yao Mungu alimtuma mtu mmoja aitwaye Musa, ambaye aliwaongoza
Waisraeli kwenda nchi yao ambayo ndiyo Israeli ya sasa.
Safari
yao iliwachukua muda wa miaka 40 kuhifikia nchi yao ya ahadi. Katika miaka hiyo
40 Mungu akafanya agano pamoja nao ambalo liliwatofautisha na mataifa
mengineyo. Mungu akawapa amri kumi, Mungu akawapa alama yao juu ya miili
yao tohara. Mungu akawapa siku ya kupumzika Sabato.
Kwa
hiyo hakuna nchi au taifa ambalo linaweza kuwa juu ya Israeli, maana
Israeli ni nchi takatifu kwa Mungu. Mfalme wake Daudi aliuteua mji wa
Yerusalemu kuwa makao makuu ya nchi ya Israeli miaka 3,000 iliyopita. Nao
utaendelea kuwa mji wake Mkuu hata Kristo atakapo kuja kutawala tena.
KWA
NINI ISRAEL.
Kuzungumzia taifa la Isreali, Kumbumbuku La Torati 7:7-9 yatuambia, “BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwasababu mlikuwa wengi kuliko
mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote; bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu,
akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kusika amri zake, hata vizazi elfu.”
Kuzungumzia taifa la Isreali, Kumbumbuku La Torati 7:7-9 yatuambia, “BWANA hakuwapenda ninyi, wala hakuwachagua ninyi, kwasababu mlikuwa wengi kuliko
mataifa yote, maana mlikuwa wachache kuliko watu wote; bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu,
akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kusika amri zake, hata vizazi elfu.”
Mungu
alilichagua taifa la Israeli kuwa watu ambao kupitia kwao Yesu Kristo
atazaliwa- mwokozi kutuokoa katika dhambi na kifo (Yohana 3:16). Mungu kwanza
aliahidi Masihi baada ya Adamu na Hawa kuanguka katika dhambi ( Mwanzo mlango
wa 3). Mungu baadaye alithibitisha kuwa Masihi atakuja kutoka kwa uzao wa
Abrahamu, Isaka, na Yakobo (Mwanzo 12:1-3). Yesu Kristo ndiye sababu kuu ya
Mungu kuichagua Israeli kuwa watu wake malaamu. Mungu hakustahili kuwa na watu
wateule, lakini aliamua kufanya namna hiyo. Yesu alistahili kuja kutoka kwa
taifa la watu fulani na Mungu akachagua Israeli
Ingawa,
sababu ya Mungu kulichagua taifa la Israeli halikuwa peke lengo la kumtoa
Masihi. Nia ya Mungu kwa Israeli ilikuwa kwamba wataenda na kuwafunza wengine
kumhusu. Israeli ilikuwa liwe taifa la makuhani, manabii na wamisionari kwa
ulimwengu. Nia ya Mungu ilikuwa, Israeli iwe na watu wa kipekee, taifa ambalo
lingeelekeza wengine kwa Mungu na ahadi zake, kutolewa kwa mkombozi, Masihi na
mwokozi. Kwa sehemu nyingi Israeli ilikosea katika jukumu hili. Hata hivyo
lengo lake kabisa kwa Israeli- lile la kuleta Masihi katika ulimwengu-
lilitimizwa kikamilifu katika Kristo Yesu.
BARIKIWA
MAKALA HII CHANZO CHAKE NI
UFALME WA MUNGU KWANZA.ORG
Maoni