KUKUA NA KUIMARIKA ROHONI


Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli” (Luka 1:80)
 Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima na neema ya Mungu ilikuwa juu yake (Luka 2:40)
kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiogoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu (1Petro 2:2)
Mtu anahitaji kukua rohoni na kuongezeka nguvu kwa sababu :-

  •  anazaliwa akiwa mchanga rohoni (immature). Mistari hii inatuonesha wazi kwamba mtu anatakiwa kukua sio tu mwili bali na roho yake pia,
  •  kuongeza hekima ndani ya mtu na neema juu yake.
  •   Ili awe na msingi wa mafanikio katika kila Nyanja.
Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama roho yako ifanikiwavyo (3 Yoh 1:2)
Kusudi la Mungu ni tufanikiwe katika maeneo yote ya maisha sio tu machache, sio unafanikiwa maswala ya kiuchumi halafu ndoa inakushinda, au unafanikiwa kielimu halafu sehemu ya kazi unashindwa. Ukweli ni kwamba, roho ya mtu inapofanikiwa katika eneo fulani, matokeo yake yanaonekana kwenye ulimwengu wa mwili kwenye eneo hilo.
Kinachotakiwa ni kwamba mtu awe na ufahamu na nguvu za kutawala mazingira yake. Na nguvu hizi zinatakiwa kuanzia Rohoni.

Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa, Ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka (Math 11:12
MAMBO YA KUZINGATIA ILI UIMARIKE KIROHO.
Tambua kwamba hakuna kukua bila kuimarika,na hakuna kuimarika bila lishe yenye virutubisho.Na lishe yenye virutubisho pasipo mazoezi(vitendo) utadumaa.
  • Yako mambo mengi yanayoweza kukufanya uimarike Rohoni :-Baadhi yake ni:-
a)       Kujifunza neno la Mungu ili uwe imara Kol 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.”Zab 119:11”Moyoni mwangu nimeliweka Neno lako,nisije ni kakutenda dhambi”
b)       Kuwa na tabia ya kumwomba Mungu.Math 7:7-8,Lk 18:1
c)       Kuenenda kama wajibu wetu ulivyo.Kol 1:10
d)       Kuishi kwa imani ya kumwamini Mungu.Ebr 11:1
e)       Kuwa na tabia ya kutendea kile unachojifunza au kuambiwa na Roho Mtakatifu au viongozi waliopewa nafasi na Mungu .(Kuwa mtendaji)Yak 2:14-26
 “Mtumishi yeyote wa MUNGU hawezi kufanya utumishi ulio mwema bila kukua na kuimarika Rohoni”.OMBA MUNGU ILI AKUPE NGUVU ZA KUKUWEZESHA KUKUA NA KUWA IMARA.
DALILI ZA KUKUA NA KUIMARIKA ROHONI
1.        Kuwa na macho ya rohoni yanayoona. Ef 1:18.
Macho ya Rohoni yatakufanya uweze kuona mambo tofauti na wengine wanavyoona.Mtu wa Mungu aliyekipofu hawezi kuona,na kama ataona ataona vibaya,na kama ataona vibaya atatenda kinyume.Bora upofu wa nyama kuliko upofu wa Roho.Aonaye maono ya Mungu amefumbuliwa macho Hes 24:4.Kama huoni mema ya Mungu unatakiwa kufumbuliwa macho uone 2fal 6:17.,Bwana huwafumbua macho waliopofuka………..Zab 146:8, Isa 35 :5,Mdo 26: 18
2.        Kuwa na uwezo wa kuchukua hatua na kuishi kama ulivyo wajibu wako. Yak 2: 14 -26, Kol 1:10,Flp 1:27-28.
Watu wengi ni wazuri wa kusikia lakini hawachukui hatua.Unapopokea neno la Mungu,linatakiwa kufanyiwa kazi kwanza.Mtu wa kwanza anayetakiwa kufanyia kazi Neno ni Yule aliyesikia au kupokea.Halafu jirani,rafiki au mwenzi.Matendo ndiyo huzaa tabia na mwenendo.Ninakushauri kama ulivyo wajibu wako kwa Bwana Kol 1 :10.
Swali Kwa nini watu wengi hawaenendi kama imani/wokovu/wajibu wao ulivyo? Ezek 12 :1-2,Math 13:13
3.        Kuwa hodari na Kusimama katika Bwana Ef 6:10 -11,Zab 31:241cor 16:13

Mtu aliyeimarika katika Roho ni hodari katika Nyanja mbalimbali.Akiwa katika majukumu ni hodari kwa kuwa anafanya kwa ufanisi.Hana mzaha katika kazi ya Mungu kama ni kuomba anaomba kweli,kama kuimba anaimba kweli,kama kutoa anatoa kweli.Kimsingi ni hodari katika mambo ya Mungu.
FAIDA ZA KUKUA NA KUIMARIKA ROHONI.Math 16:16-19
Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. 17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. 19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.

  1. ·         Kufanyika maskani ya Bwana,kwa kuwa Bwana atakuja kwako hakuna la kukushinda maana Bwana mwenyewe amekupa nguvu za kukanyaga nyoka na nge.
     2.    Kupewa Mamlaka ya Ki –Mungu.
Mungu akubariki sana ,na karibu katika mafundisho mengine.
Na,AYOUB JACOB LEO(Mzee wa kanisa FPCT KISESA)
Simu +255 (0) 755 035 722 au +255 (0) 785 645 177

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUFANIKIWA KI -UCHUMI KWA NJIA YA MUNGU

UCHAMBUZI WA KITABU CHA DANIELI

SOMO: NGUVU YA DAMU YA YESU KATIKA KUWEKA AGANO