SOMO : UTATAKA KUTUBU LAKINI TOBA YAKO ITAKATALIWA.
MCH. BOAZ ANASI FPCT
UJIJI KIGOMA
Kuna mambo
yanaonekana kana kwamba Mungu ana ugomvi na wewe.
Mambo haya
yanakwamisha au kukufanya ushindwe kumwona Mungu katika maisha yako.
Isa 1:19,Yak 4
:7a,Kut 19 : 3-8
3Musa akapanda kwa Mungu, na BWANA akamwita toka mlima
ule, akisema, Utawaambia nyumba ya Yakobo, na kuwaarifu wana wa Israeli, maneno
haya; 4#Kum
32:11; Isa 63:9; Ufu 12:14Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi
nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. 5#Kum 4:20; 7:6; 10:14; 14:2; 26:18; 32:8;
1 Fal 8:53; Zab 50:12; 135:4; Tit 2:14; 1 Kor 10:26Sasa basi ikiwa mtaitii
sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu
kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, 6#Ufu 1:6; 5:10; 20:6; 1 Pet 2:5,9; Law
20:24; Kum 7:6; Isa 62:12; 1 The 5:27nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa
takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli. 7Musa akaenda akawaita wazee
wa watu, akawafunulia maneno hayo yote, BWANA aliyokuwa amemwagiza. 8#Kut 24:3,7; Kum 26:17Watu wote wakaitika pamoja
wakisema, Hayo yote aliyoyasema BWANA tutayatenda. Naye Musa akamwambia BWANA
maneno ya hao watu.
JAMBO
LA KWANZA : KUTOKUTII SAUTI YA MUNGU
Kumbuka jinsi Mungu
alivyowatendea Israeli kwa mapigo kumi.Mungu aliwaahidi kuwa kama watamtii
atawatukuza juu ya mataifa yote.
Watu walikubali na kusema
kwamba watayatenda yote (watatii).Mungu hapa anaweka mkataba kati yake na
wanawa
Isa 1:19 Kama mkikubali na
kutii mtakula mema ya nchi; Kumbe kama mkiitii sauti ya Mungu mtakula mema ya Nchi.Kanisa
la leo limejikuta halitii sauti ya MUNGU (NENO).Jambo hili linaleta shida kwa
watu wengi.Wanakataa kutii maigizo ya Mungu katika maisha yao.
Kama tukifanya mambo yote
pasipo utii ni kujilisha upepo.Sifa pasipo utii ni kujilisha upepo.Yako mambo
tunayafanya katika ibada lakini watu wanapungukiwa na neno moja la utii.Kila
mara Mungu anatoa maagizo katika madhabahu yake.
Watu hawako tayari kutii
Neno la Mungu,wanataka kwenda wanavyotaka.Binti akiolewa anatakiwa kutii
utaratibu wa ndoa siyo kuishi anavyotaka.
Mungu anataka tuenende kama
anavyotaka.Mungu anasema na watu kwa njia :-
a)
Sauti yake (ndogo)
b)
Neno lake (Maandiko Matakatifu )
c)
Ndoto
Maana ya Kutii ?
Ni
kufanya kile unachotakiwa kukifanya kwa moyo wa kupenda.Ukifanya hivi kinaleta Baraka.
Kutokutii
sauti ya Mungu kunaleta shida.Kunamfanya Mungu akasirike kwa kuwa unaonekana
kama mkaidi.Unaonekama usiyekubali
JAMBO LA PILI : “ KUTOKUFANYA MAPENZI YA
MUNGU” KUMB 28 :1,LK 2:10-15
Kum 28:1”Itakuwa
utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo
yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya
mataifa yote ya duniani”;
Tunapaswa kuzingatia kuyafanya maagizo ya Mungu.Kama
hatutendi/kuzingatia maagizo tunazuia majibu kutokea.
Ushuhuda wa Mchungaji kuishiwa akiba mwisho wa
mwezi.Wakati matangazo ya sadaka yanatolewa.Alisikia sauti ndogo ikimwambia
chakula/sadaka inayotolewa ni kwa ajili ya wajane.Alikabidhi sadaka yote iliyotolewa
kwa wajane na baadae wingu la Roho Mtakatifu likaifunika ibada.Alitokea mtu
mmoja na kuchukua microphone kisha akaagiza kila mwenye Tsh 10,000/= atoe.
Kutii ni bora kuliko dhabihu.Mungu anatamani kukufunulia
utukufu .Unataka Mungu aseme na ninyi kwa namna gani ?Kumbuka Tajiri na Lazaro/Ibrahimu.Tunatakiwa
kuwasikiliza watumishi wa Mungu wanaposema yale waliyoambiwa na
Mungu.Sikilizeni sana watumishi wa Mungu.
UKITII SAUTI YA MUNGU
WEKA KATIKA VITENDO
IPO HATARI MBELE YAKO KAMA HAUTAITII SAUTI YA MUNGU. 1Sam
15:
Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa
cha kabila za Israeli? Naye BWANA akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli. 18Kisha BWANA akakutuma
safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi,
upigane nao hata watakapoangamia. 19Mbona, basi, hukuitii
sauti ya BWANA, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA? 20Sauli akamwambia
Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya BWANA, nami nimemleta Agagi, mfalme wa
Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. 21Ila watu waliteka
nyara, kondoo na ng’ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi
wavitoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, huko Gilgali.
22 Naye Samweli akasema,je!
BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu
Sawasawa
na kuitii sauti ya BWANA?Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu,
Na
kusikia kuliko mafuta ya beberu.
23 # Kum
18:10 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi,
Na
ukaidi ni kama ukafiri na vinyago;
Kwa
kuwa umelikataa neno la BWANA,
Yeye
naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
24 Ndipo Sauli
akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya BWANA, pia na
maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao. 25Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja
nami, nipate kumwabudu BWANA. 26#1 Sam 2:30Samweli
akasema, Sitarudi pamoja nawe;
kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli.
Sauli alifanya
kinyume na maagizo ya Mungu kwa kuleta mfalme wakati alipaswa kumwua siyo
kumleta.Kwa kosa hilo SAULI alikataliwa na ufalme wakke ?
Mara ngapi Bwana
amesimama na kusema na wewe lakini hakuna kinachofanyika.Itafika mahali
utapaswa kutubu lakini toba yako itakataliwa.Kuna watu ukaidi wao unaonekana
kushindikana.UTATAKA KUTUBU NA TOBA YAKO ITAKATALIWA.
Maoni