Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2016

UENDESHAJI WA VIKAO

Ni jambo zuri kuwa na vikao vya ndugu,jamaa,jumuiya,kikundi,Taasisi n.k Fuatilia somo hili kwa makini. UENDESHAJI WA VIKAO Na, AYOUB LEO VIKAO Ni mazungumzo yanayofuata utaratibu maalum kwa ajili ya kupata azimio/maamuzi ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu/mipango. Uongozi shirikishi una tabia ya kujali vikao ili kuweka mipango na mikakati inayowezesha kundi/jamii kuwa katika umoja.Hivyo uongozi wa kidemokrasia huwa na vikao ili kupata ushauri na maoni ya wajumbe juu ya mipango. SIFA ZA VIKAO ·          Vikao vinatakiwa kuwa na agenda/mada ya kujadili. ·          Viwe na muda maalum wa kuitishwa mfano.Wiki/Mwezi/miezi mitatu na hata mwaka .(Hii hutegemea aina ya vikao) ·          Kuwa na wajumbe( idadi ya wale waliokubalika). ·          Kuwepo na mwenyekiti, katibu na wajumbe wengine. ·          Agenda zifafanuliwe kwa kina kabla ya wajumbe kuchangia.(Taarifa kwa kina itolewe juu ya agenda iliyopo mezani ili kuwapa mwanga wajumbe wajue undani wake) ·  

UJASIRIAMALI

HII NDIO MAANA HALISI YA KUENDESHA BIASHARA KISOMI UJASIRIAMALI Kwanza kabla hatujaenda mbali tambua yafuatayo: Sio lazima mwenye biashara awe msomi ili biashara iendeshwe kisomi Sio kila msomi anaweza endesha biashara kisomi. Kuendesha biashara kisomi sio tuu kufanikisha biashara ipate faida. Kuendesha biashara kisomi ni zaidi ya elimu ya darasani ya biashara Endelea kusoma ufahamu vizuri nini cha kufanya ili biashara iendeshwe kisomi. Ipo hivi,  kuendesha biashara kisomi ni pale unapoamini na kutenda mambo yahusuyo biashara yako kwa imani na mtazamo kuwa biashara yako ipo sio tuu kwa sababu ya kupata faida ili wewe ujinufaishe bali huko kupata faida ni sehemu tuu ya malipo yako ya kukufanya uihudumie biashara yako ifikie kile ambacho kweli haswa ndio lengo lake. Hivyo kwa mtazamo wa kisomi ni kuwa pamoja na kwamba wewe unajiita bosi, kiukweli wewe ni mtumishi tuu wa hiyo biashara.  Itazame biashara yako kama kiumbe ambacho kimekwisha zaliwa, kinahitaj

KISESA YETU

Picha
Hiki ni kilima kidogo kinachopatikana kata ya Kisesa,Kijiji cha Kitumba maarufu kama Mlima wa Astadi.                                           Ubao wa kuingia shuleni ya Sekondari Kitumba                                                                                         Kuingia na kutoka shuleni                 .                                                       Tanki la kuvuna maji ya mvua.                                              Nyuma ya madarasa ya kidato cha kwanza na tatu.                                             Madarasa ya kidato cha kwanza na tatu                                             Madarasa ya kidato cha kwanza na tatu                                         Eneo linalochimbwa mchanga jirani na uwanja wa shule                                        Eneo linalochimbwa mchanga jirani na uwanja wa shule