Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2016

HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA MKUTANO WA NNE WA BUNGE LA KUMI NA MOJA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 16 SEPTEMBA 2016, DODOMA

UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda na kutupa afya njema hadi kutufikisha siku ya leo tunapohitimisha Mkutano wa Nne wa Bunge lako Tukufu tuliouanza tarehe 6 Septemba, 2016. 2. Nitumie fursa hii pia kukupa pole, Mheshimiwa Spika, kwa maradhi yaliyokusibu lakini kikubwa nielezee furaha yangu kwa uponyaji ambao Mwenyezi Mungu amekujalia na hivi sasa tuko pamoja humu ndani. Tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu uendelee kupata nguvu na afya njema. 3. Mheshimiwa Spika, tangu tulipokutana mara ya mwisho, kumekuwepo majanga na matukio mbalimbali ya maradhi, ajali, ujambazi na matukio mengine ambayo yamesababisha vifo na majeruhi kwa Watanzania wenzetu, wakiwemo Waheshimiwa Wabunge. Hivyo, ninatoa pole kwa wafiwa wote na wale wote waliopatwa na majanga kutokana na matukio hayo. Tunawaombea afya njema wale waliopata majeraha na waliopo hospitali. 4. Mheshimiwa Spika, leo tunahi...