li uweze kufanikiwa, ni lazima kujiwekea misingi imara ya kimafanikio itakayokuwa ikukuongoza kila siku. Bila kuijua misingi hii mapema sitashangaa kuona maisha yako yakibaki kuwa yaleyale bila ya kubadilika sana. Kwa kujiwekea misingi hii, inauwezo wa kufanya maisha yako kubadilika kwa sehemu kubwa sana. Kama misingi hiyo ipo, ni nini kinachokuzuia wewe kufanikiwa sasa? Bila shaka hakuna. Unachohitajika kukifanya ni kutumia misingi hiyo mpaka kufanikiwa. Uwezo na nguvu za kubadilisha maisha yako kwa kadri unavyotaka unao. Kwa kuijua misingi hii, kwako itakuwa chachu ya kukusaidia kuweza kusonga mbele na kujijengea maisha ya mafanikio makubwa:- Je, misingi hiyo ni ipi? Hii Ndiyo Misingi 6 Muhimu Ya Kujiwekea, Ili Kujenga Mafanikio Ya Kudumu 1. Kaa mbali na watu hasi Kama vile ambavyo ilivyo kompyuta inaweza ikaharibiwa na virusi na kuharibika kabisa, hata wewe maisha yako yanaweza kuharibiwa vivyohivyo lakini ikiwa una watu hawa hasi wengi wanaokuzunguka. Unapok...