INJILI
SOMO.NGUVU YA MAONO KATIKA MAISHA YA MKRISTO UTANGULIZI. Tangu mwanzo Mungu aliwekeza raslimali nyingi za thamani ndani ya mwanadamu kama vile Ufahamu,Ujuzi,ubunifu,Ugunduzi,busara,vipaji mbalimbali,mamlaka,uhai,chanzo cha Baraka.Mwanzo 1:26-30,2:7. Mwanadamu anapozaliwa tayari Mungu anakuwa amekamilisha sehemu kubwa ya uumbaji wa mwili,hivyo anapozaliwa huanza kudhihirisha raslimali hizo katika hali ya upekee tofauti na viumbe vingine. a) Mamlaka ya kumiliki vitu vyote Mwanzo 1:26-30,2:7 b) Kujitambua c) Chanzo au chemichemi au chimbuko la Baraka –Kumb 8:18 Zaidi sana mwanadamu anapookolewa , Mungu huwekeza vitu vingine vya thamani katika maisha ya mwanadamu.Vitu hivi humfanya Mwanadamu afanye zaidi ya uwezo wa kuzaliwa nao (uwezo wa kawaida).Raslimali hizo ni a) Huduma,karama na vipawa 1 Kor 12:4-11 b ) Mamlaka ya kumshinda shetani Lk 10:19, 1 sam 17:40-54 c) Ufahamu wa Ki-...